Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupewa tuzo ya mwanamke shupavu wa Mwaka

Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajivunia kupata kiongozi shupavu na mahiri ambaye kwa kipindi kifupi cha uongozi wake kwenye bunge hili ameonyesha haya
1. Uhodari wa kusimamia na kutumia kanuni za kudumu za bunge ambazo kwa miaka mingi zilikosa watu wa kuzisimamia
2. Uwezo wa busara zake wa kufanya rejea ya maamuzi yaliyowahi kufanya na viongozi wa mabunge yaliyopita huko nyuma kufanyia maamuzi.
3. Ameonyesha uwezo na nguvu ya kiti cha spika ambazo wengi wetu tulikuwa hatuzifahamu kwa miaka mingi kama spika anapo simama wabunge wote wakae chini .
4. Uwezo wa kusilikiza maoni na hoja za wabunge huku akiandika (umakini wa hali ya juu)
5. Wapinzani kuliogopa bunge na kulikimbia hali ya kuwa waliomba ubunge bila kujiandaa.
my take heko Dr tuliza endelea go tulia , TULIZA wetu...
ameonyesha uwezo kuliko waliotangulia?
 
Asiyekua na makundi ndani ya bunge na haingiliki kwa hoja za uonevu
 
Walizoea ujinga kidogo wanasusa wanaitwa magogoni kwenye kamati ya maridhiano sasa hakuna ujinga huu,raid atosha,spika atosha na nchi itake isitake itaenda tu
 
hiyo picha inajieleza vizuri kuliko maelezo uliyoweka hapo,kama ni kwa hayo anayofanya anastahili tuzo
 
Kuna afisa mmoja hivi alishuhudia kwa macho yake kuuwawa kwa Mwangosi kule Nyororo Iringa na bila kutoa msaada wowote ule, baada ya siku chache hivi akapewa bonge la ubosi zaidi. Such things happen under this sun.
Nampongeza lakini..................................................
Huyo ni kamuhanda wala hakuna siri hapo
 
Ubora wa kiongozi hutokana na uwezo wake wa kuunganisha makundi anayoyaongoza. Mpasuko baina ya unaowaongoza ni dalili za kutokuwa na uwezo huo. Hizi taasisi za tuzo nazo ni za kutilia mashaka. Kiongozi aliyestahili tuzo tena ya nobel Tanzania ni rais mstaafu wa Zanzibar ndugu Aman Karume basi.
 
Taasisi ya kimataifa ya EAWRA inatarajia kumpa tuzo mwanamke shupavu kwa ukanda wa Africa Mashariki, ambapo safari hii kwa mara ya kwanza tuzo inakuja Tanzania. Ni baada ya Naibu Spika kupita mchujo na kuibuka mshindi wa jumla..

Hii inatokana na msimamo wake, umahiri wake, na ushupavu wake katika kulisimamia mhimili wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na ueledi wa hali ya juu.... Tuzo hizo zitatolewa tarehe 4, July, 2016....

Mytake. Kwa hakika taasisi hii haijakosea. Dr. Tulia amekuwa mwanamke shupavu kwa sasa, na ambalo taifa hili linajivunia kuwa naye....
Mwl.Julius Nyerere alisema "Nikiona wazungu wananisifia nitajiuliza nimekosea wapi"
 
Back
Top Bottom