Naibu Katibu wa Bunge:Hakuna kanuni za Bunge zinazozuia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa

Mtu ni yuleyule aliyefanya kosa lilelile mahala palepale muda uleule.... adhabu kapewa ya kutenguliwa uteuzi wake (kufutwa kazi) vipi bunge nalo litaamuaje? Wananchi nao wataamuaje? Kama kosa lile adhabu ni kufukuzwa kazi, kwanini ubunge wake usitenguliwe pia?....
 
Kuna wanaodai kwamba kitwanga hakunywa chochote zaidi ya chai ya rangi , ila alijifanya kalewa ili dili litimie ! ( tuichukulie kama tetesi kwanza ) , nina nzi wawili , mmoja bungeni mwingine home affairs .
Nchi hii kila kitu kinawezekana.
 
Siku za yeye kuwa waziri zilikuwa zimekwisha, amshukuru Mungu kumuachia uhai wake
Umenena vema....haya majadiliano yanaweza kuchukua mwaka ila itoshe kusema hakuna kanuni inayosema ukiwa waziri lazima umalize miaka 5 madarakani.Ni zamu ya mwingine sasa.
 
Tatizo Sheria zao ni za kulindana, wanalindana mpaka ulevi wanashindwa kuuweka kwenye Kanuni, sijui hawajui tofauti ya unywaji na ulevi?! Poor tanzania
 
Akiingoe na gazeti la Nipashe,Naibu Katibu wa Bunge,John Joel amesema hakuna kifungu chochote cha kanuni za Bunge zinazomzuia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa.

"Kanuni zinahusiana na uendesha wa shughuli za Bunge,hizi za Maadili ni kanuni za Maadili ambazo zinatakiwa kutungwa ili kudhibiti hali hiyo ",alisema Joel.

Chanzo:Nipashe online

Kwa mujibu wa habari hii,mbunge wa Sumve, Richard Ndasa alimsihi mara tatu Kitwanga asiingie Bungeni kwasababu alikuwa na kila dalidali za kulewa lakini Kitwanga alikataa na hata baada ya kikao cha Bunge kwisha, Ndasa alijaribu kumshika mkono Kitwanga ili amuondoe katika viwanja ya Bunge lakini Kitwanga alimkimbia.

Kwa mijibu wa maelezo ya Ndassa katika habari hii,baada ya Kitwanga kumkimbia,Ndasa alimfuata dereva wa Kitwanga na kumwambia amuondoe Kitwanga katika viwanja vya Bunge ila Kitwanga alikataa kuingia ndani ya gari.Ndasa ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Mwanza.

Baada ya kusoma haya maelezo ya Ndasa naanza kujiuliza hivi Kitwanga ni nini kilimsibu mpaka kufanya haya yote au alifanya tu makusudi ili haya yatokee?Mbona hii kitu haingii akilini?
Ben nkapa alihutubia jangwani kwenye kampeni na kutukana mbona walishangilia sana pamoja na jpm?
 
Back
Top Bottom