ZILLAHENDER MPEMA
JF-Expert Member
- Apr 4, 2015
- 2,055
- 4,243
Acha uongo wewe mbona alikuwa mbunge kabla lowasa ajajiunga na Chadema...? Chadema mmepoteza uelekeo baada ya kumkaribisha lowasa...Watu wote makini watakimbia...Zito ndio mpinzani pekee mwenye heshima nchi hii
Hauhitaji kuwa na kipaji cha kukariri urefu wa km za barabara,idadi ya samaki wenye mimba nchini wala kupiga push-ups jukwaani ndiyo ujuwe nguvu ya upinzani nchini.Waulize "mabwana zako" wa Lumumba wanaotumia vikosi kazi vyote kuanzia vya chama,bunge na serikali kuuzima moto wa upinzani kupitia kile wanachokiita "Taarifa za kiintelejensia",wao watakuambia kama upinzani hauna nguvu kwa nini hawataki kuwapa nafasi ya kufanya siasa.
Ni aibu sana kwa jukwaa letu kuwa na mtu mwenye uelewa duni kama wako,hivi wewe ni mzima au umekufa?R.I.P,aliye hai hawezi kuwa na hoja za kipuuzi kama hizi.
Hakuna hata mmoja huko serikalini asiyejuwa nguvu kubwa ya wapenda Demokrasia waliyopo nchini,kutokana na hila walizozifanya kupata nafasi walizonazo,hawaamini hata mamlaka waliyonayo na ndiyo Maana wakalazimika kuzuia shughuli za kisiasa,halafu wewe unakurupuka kusema eti upinzani hauna nguvu?Kama hauna nguvu kwa nini jumuia mpya ya ccm iitwayo " policcm"inapambana usiku na mchana kuwazingira na kuwahoji wanaoonekana kuwa mwiba kwa serikali?