IqraNI
Senior Member
- May 16, 2020
- 142
- 142
Ndugu wanajamii, nawasalimu.
Mimi ndugu yenu nina shida na ninahitaji msaada wenu ili niweze kukabili hii hali inayonisumbua.
Tatizo langu ni kukata tamaa mapema, siwezi kupigania kitu nakipenda na kukihitaji na mpaka sasa naona nitapoteza mwelekeo.
Niko kwenye mahusiano na huyu mwanaume mwaka mmoja sasa, lakini huyu mwenzangu alianza kunikalia kimya ghafla, hajibu ujumbe kwa wakati au anaweza asijibu kabisa na akipiga simu anajambo anataka nimsaidie, nikajua pengine ubize wa kazi lakini hali ikaendelea kama mwezi, nilipomuuliza akanijibu kuwa hakujua kama kwa kufanya hivyo " ananikera."
Nikatafakari na kumuuliza kama kuna chochote nimekosea akasema hakuna, sasa nimeamua kujiongeza tu kuwa hapa hamna kitu na bahati mbaya sana akiwa na shida ndio ananitafuta.
Mtaniwia radhi kwa uandishi lakini Ushauri na msaada wenu unahitajika kwa haraka, natanguliza shukrani.