Nahitaji kujua nini ili niwe Hacker?

Ni kweli kila mtu anaweza kujifunza kuhack, lakini si kila mtu anaweza kuwa hacker!
Si kweli hacking ni illegal,bila hackers kusingekua na internet,world wide web isingefanya kazi,Unix system isingefika hapa ilipo nk nk!utasemaje hacking ni illegal?ni sawa na kusema kuendesha gari ni illegal,ni illegal pale tu utapokeuka sheria za barabarani,yaani ni illegal kuvunja sheria za barabarani na sio kuendesha gari!
People should learn to understand this aisee!


Aisee!hapa umemaanisha nini exactly?
kuna process tano. 1.footprinting au inaitwa social engineering. 2. inaitwa Scanning. 3. vulneri.bility 4. penetration 5. Hacking. hizi mbili za mwisho, siyo ethical.
 
Tujaribu kukimbizana na Dunia nahitaji kuwa hacker naomba uzi huu utumike kunifundisha ili niwe hacker,kwa kuanza nataka nianze kwa kuwa simple hacker nahack vitu vidogo vidogo kama account ya mtu insta,na vitu vingine vidogo vidogo

Mahitaji yake ni nini? Najua google masomo kama haya yapo ila uelewa nao unachangia inabidi uwe mjuzi kidogo na lugha pia!

Najua hapa kuna Mahacker wazuri tuu

Karibuni
Soma vipo vitabu acha uvivu
 
kuna process tano. 1.footprinting au inaitwa social engineering. 2. inaitwa Scanning. 3. vulneri.bility 4. penetration 5. Hacking. hizi mbili za mwisho, siyo ethical.
Aisee!!!kumbe hizi ndo process tano!ebwana eeh!Mkuu ndo unajipanga kufundisha kabisa!???Aiseee!kwaio hizi mbili 'Penetration na Hacking' ndo sio ethical sio!aisee!nilikua sijui kabisaa yani kuhusu hizi process,na sidhani hata kama kuna mtu yeyote kwenye community nzima anajua hili!Naomba niishie hapa tu aisee!Kila la heri mkuu katika ufundishaji wako.
 
Nauliza tu.., hacker ni kwa watu wa IT tu au?

Na je kwa umri flani tu?

Na je naweza mwajiri hacker kama security experts kwenye code zangu?
 
Nauliza tu.., hacker ni kwa watu wa IT tu au?

Na je kwa umri flani tu?

Na je naweza mwajiri hacker kama security experts kwenye code zangu?

Hapana hata mtu wa la saba anaweza kuwa hacker..
Umri wowote
Security expert lazima asome ethical hacking ..inampa tu urahis wa kuwa competent hacker lakin sio kila hacker mzur alisoma system security
Hacker ni penetration taster,just imagine software kama ukuta wa matofari...kazi ya hacker ni kutafuta ufa kwenye ukuta ili aone upande wa Pili wa ukuta..yawezekana lengo lake la kutafuta ufa ni ili amsaidie mjenzi(programmer/developer) kujua wapi kuna ufa ili arekebishe huyu ndio Ethical hacker
au lengo lake laweza kuwa ni kutafuta ufa ili akiupata aongeze uwe hole apenye huyu ni Black Hat hacker
ikitokea haoni ufa atausababisha kwa makusudi huyu ni Cracker
 
Nauliza tu.., hacker ni kwa watu wa IT tu au?

Na je kwa umri flani tu?

Na je naweza mwajiri hacker kama security experts kwenye code zangu?
Najibu tu..,Hacking si kwa watu wa IT tu but ni lazima uwe na some IT knowledge ili ujue kuhack!(assuming swali lako limelenga watu ambao hawapo related na Tech field)

Umri wowote ule,minimum requirement ni uwe unafikiria Logically!

Hacker ni security expert!either awe na nia mbaya au nzuri au awe mbomoaji au mjengaji.Hacker aliyepewa authority anaitwa 'white/ethical hacker/pen-tester ',kwaio jibu ni NDIO,unaweza muajiri Penetration tester/Ethical Hacker/White Hacker (Unaweza kumpa kibarua Gray pia kwa makubaliano husika)
 
Daaah.... napenda sana mambo ya IT....hi mivitu ya programming....wanaandika vitu hata havisomeki ila vina fanya kazi, hasa nikionaga kwa movie huwa roho yangu kwatu, Sitaki mtu aseme nikasome mambo ya excel na word hapa. Nahitaji kujifunza nami....:(:(:(:(
 
Duh haya bwana naona nmekukaa sana kichwani, all in all jamani watu mnaotaka kuwa hackers a.ka. wadukuaji, it is illegal kufanya hivi vitendo na wala siwapotoshi maana sheria za cyber crime zipo mwaweza kuzipitia
Duh, yaani umekaa ukawaza kuwa hacking ni illegal!? Au umekaririshwa kuwa hacking ni illegal!? Pole sana mkuu
 
Hacking ni knowledge ambayo mtu yoyote anaweza kujifunza awe tu na Basics knowledge ya computer hardware, Compter networking na Web component development ,pia awe na basics knowlege jinsi Operating systems zinavyofanya kazi,esp. Window na linux . lakini kisheria duniani Hacking ni illegal activities , isipokuwa mtu yoyote anayetaka kujifunza hacking kisheria, anaitwa Ethical hacker ,nchi za wenzetu Mtu yoyote anayetaka kujifunza Ethical hacking lazima .awe screened. Na chuo kinachofundisha lazima kipewe kibari na serikali ili hiyo kozi iweze kufundishwa na chuo hicho . kuna process tano kwenye Hacking process. Kisheria Mwanafunzi anayetaka kujifunza Ethical hacking anafundishwa process tatu tu. hizo mbili zilizoback haurusiwi kisheria. utakapojifunza hizo mbili utakuwa sasa wewe siyo ethical hacker,Na makampuni mengi wanapotatafuta mtu wa kumuajili kama hacker. wanaaminisha wanamtafuta Ethical hacker huyu muda mwingine anaitwa WHITE HACKER .MiMi ni mwalimu wa Ethical Hacking, naweza kukufundishaTools zote na Technics zote za Ethical Hacking. Nipo mbioni kufungua Chuo hapa Dar es salaam. ambacho kitashirikiana na chuo kimojawapo cha marekani nipo kwenye hatua za mwisho ,international procedures tayari nimezimaliza ,kwa sasa natafuta kibari wizara ya mambo ya Ndani, ndiyo nachelewa kukipata. hiki chuo kitakuwa pia ni prometric centre ya Ethical hacker certification . Mwanafuzi atayesoma hapa atapata international Certification.
Kuna hatua tano za hacking
1.Reconnaissance
2.Scanning and Enumeration
3.Gaining Access
4.Maintaining Access
5. Covering tracks (Hiding digital Footprints)
From EC-Council, official course ya CEH blueprint.
1.Ni stage gani ambazo White Hat Hacker hafundishwi kati ya hizo??
2. Huoni Black Hats watakuwa na advantage over you (White Hat), kama unapewa knowledge nusu nusu??
Mtazamo wangu "If you want to be the best white hat think like a black hat".
 
Kuna hatua tano za hacking
1.Reconnaissance
2.Scanning and Enumeration
3.Gaining Access
4.Maintaining Access
5. Covering tracks (Hiding digital Footprints)
From EC-Council, official course ya CEH blueprint.
1.Ni stage gani ambazo White Hat Hacker hafundishwi kati ya hizo??
2. Huoni Black Hats watakuwa na advantage over you (White Hat), kama unapewa knowledge nusu nusu??
Mtazamo wangu "If you want to be the best white hat think like a black hat".
A hat is a hat don't forget, ONLY BLACK is not a Chamelion.
 
Back
Top Bottom