Nadhani kwa mambo yanavyokwenda hatuna budi kumpa pongezi Rais Samia

Kwa kweli she is good. Wakimuacha afanye kazi mwenyewe wasipomuingilia yuko vizuri sana. Tatizo inaonyesha kuna watu wana maslahi binafsi na wanamsumbua tu mama yetu. Hawa hawatakaa wakaridhika hata wapewe nini.

Mama fanya kazi hao wajinga wote timua wasikusumbue. Mama Samia@2025-2030
 
Kama angekuwa msikivu na anayelitakia mema Taifa letu, angelifanya jambo moja kubwa kuliko yote:

Angesimamia mchakato wa kupata Katiba mpya. Katiba mpya ina tija kwa kila mtanzania wa leo na kesho, wa kila chama na asiye na chama, wa kila dini na kila kabila, wa bara na visiwani. Lakini kwa bahati mbaya, yeye na Serikali yake na chama chake, ndio wamekuwa kikwazo kikubwa wa kupata katiba mpya. Kwa hilo pekee, hastahili kusifiwa kwa lolote. Ataingia kwenye historia ya viongozi maadui wa ustawi wa Taifa.

Kama angelisimamia mchakato wa kupatikana katiba nzuri mpya, hakika angekumbukwa vizazi na vizazi, na angekuwa ameacha alama kubwa kwa Taifa lake. Lakini anacholifanya sasa ni sawa na fundi wa gari lililoharibika, lisilo na uwezo wa kutembea, lakini fumdi amekazana na kulipaka rangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumpe muda
 
Binafsi mimi sio muumini wa siasa za CCM lakini kama haya machache yafuatayo mnyonge mnyongeni haki yake tumpe :-

1. Kuwa msikivu , mama anasikiliza mpaka kelele na maoni ya mitandaoni na ya msingi kuya fanyia kazi .

2. Kuruhusu mikutano ya kisiasa

3. Pasipo kujali nani atanufaika kisiasa zaidi amendelea kwa nguvu zote kukamilisha miradi aliyoanzia mtangulizi wake Hayati Magufuli

Haki yake apewe
Hiyo no 1 .km ni kweli amrudishe slaa ardhi
 
Back
Top Bottom