Nadhani kwa mambo yanavyokwenda hatuna budi kumpa pongezi Rais Samia

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
1,349
2,951
Binafsi mimi sio muumini wa siasa za CCM lakini kama haya machache yafuatayo mnyonge mnyongeni haki yake tumpe :-

1. Kuwa msikivu , mama anasikiliza mpaka kelele na maoni ya mitandaoni na ya msingi kuya fanyia kazi .

2. Kuruhusu mikutano ya kisiasa

3. Pasipo kujali nani atanufaika kisiasa zaidi amendelea kwa nguvu zote kukamilisha miradi aliyoanzia mtangulizi wake Hayati Magufuli

Haki yake apewe
 
Mama namuunga mkono kwenye mambo mawili mhimu na pengine ndani ya moyo wake kuna mazuri zaidi, shida ilikuwa ni uamzi tu na sasa kaamua na aache kabisa kabisa kuwasikiliza watu wa msoga!

Kuwatoa kina Nape na Januari na kumruhusu Kinana aachie madaraka, hapa mama apewe mauwa yake!

Bado moja tu namuomba, akilifanya tafadhari naomba aungwe mkono na kila mpigania haki nchini, nalo ni kumuunga mkono Mpina basi!
 
Binafsi mimi sio muumini wa siasa za CCM lakini kama haya mawili machache yafuatayo mnyonge mnyongeni haki yake tumpe :-

1. Kuwa msikivu , mama anasikiliza mpaka kelele na maoni ya mitandaoni na ya msingi kuya fanyia kazi .

2. Kuruhusu mikutano ya kisiasa

3. Pasipo kujali nani atanufaika kisiasa zaidi amendelea kwa nguvu zote kukamilisha miradi aliyoanzia mtangulizi wake Hayati Magufuli

Haki yake apewe
Kwa kweli umeandika kama ambavyo mimi ningeandika pia.
Binafsi nimeanza kumwona yule 'Simba Jike' wa Bunge la Katiba kwa mbaali!
Huyu wa sasa ndo Samia tunayemtaka.
Wa 'hapo katikati' alikuwa copy!
Big up sana mama.
Ukiendelea hivi kura yangu 2025 nitakupa na nitakupigia kampeni.
 
Mama namuunga mkono kwenye mambo mawili mhimu na pengine ndani ya moyo wake kuna mazuri zaidi, shida ilikuwa ni uamzi tu na sasa kaamua na aache kabisa kabisa kuwasikiliza watu wa msoga!

Kuwatoa kina Nape na Januari na kumruhusu Kinana aachie madaraka, hapa mama apewe mauwa yake!

Bado moja tu namuomba, akilifanya tafadhari naomba aungwe mkono na kila mpigania haki nchini, nalo ni kumuunga mkono Mpina basi!
Kweli Mkuu.
Kuna watu wametusababishia ukali wa maisha kuongezeka sana hapo katikati.
Huenda huo ukali unaenda kupungua kwa kiasi fulani baada ya kuwa wameondoka!
 
Mama namuunga mkono kwenye mambo mawili mhimu na pengine ndani ya moyo wake kuna mazuri zaidi, shida ilikuwa ni uamzi tu na sasa kaamua na aache kabisa kabisa kuwasikiliza watu wa msoga!

Kuwatoa kina Nape na Januari na kumruhusu Kinana aachie madaraka, hapa mama apewe mauwa yake!

Bado moja tu namuomba, akilifanya tafadhari naomba aungwe mkono na kila mpigania haki nchini, nalo ni kumuunga mkono Mpina basi!
Hakika
 
Binafsi mimi sio muumini wa siasa za CCM lakini kama haya machache yafuatayo mnyonge mnyongeni haki yake tumpe :-

1. Kuwa msikivu , mama anasikiliza mpaka kelele na maoni ya mitandaoni na ya msingi kuya fanyia kazi .

2. Kuruhusu mikutano ya kisiasa

3. Pasipo kujali nani atanufaika kisiasa zaidi amendelea kwa nguvu zote kukamilisha miradi aliyoanzia mtangulizi wake Hayati Magufuli

Haki yake apewe
Hakika anastahili maua yake ila subiri Nyumbu wa mzee Mbowe na matusi yao
 
Binafsi mimi sio muumini wa siasa za CCM lakini kama haya machache yafuatayo mnyonge mnyongeni haki yake tumpe :-

1. Kuwa msikivu , mama anasikiliza mpaka kelele na maoni ya mitandaoni na ya msingi kuya fanyia kazi .

2. Kuruhusu mikutano ya kisiasa

3. Pasipo kujali nani atanufaika kisiasa zaidi amendelea kwa nguvu zote kukamilisha miradi aliyoanzia mtangulizi wake Hayati Magufuli

Haki yake apewe

Kama angekuwa msikivu na anayelitakia mema Taifa letu, angelifanya jambo moja kubwa kuliko yote:

Angesimamia mchakato wa kupata Katiba mpya. Katiba mpya ina tija kwa kila mtanzania wa leo na kesho, wa kila chama na asiye na chama, wa kila dini na kila kabila, wa bara na visiwani. Lakini kwa bahati mbaya, yeye na Serikali yake na chama chake, ndio wamekuwa kikwazo kikubwa wa kupata katiba mpya. Kwa hilo pekee, hastahili kusifiwa kwa lolote. Ataingia kwenye historia ya viongozi maadui wa ustawi wa Taifa.

Kama angelisimamia mchakato wa kupatikana katiba nzuri mpya, hakika angekumbukwa vizazi na vizazi, na angekuwa ameacha alama kubwa kwa Taifa lake. Lakini anacholifanya sasa ni sawa na fundi wa gari lililoharibika, lisilo na uwezo wa kutembea, lakini fumdi amekazana na kulipaka rangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom