Nabadili gia angani: Nitapiga kura

Kingdom123

Member
Aug 13, 2020
25
49
Kwa mwenendo ulivokuwa hapo nyuma wa siasa katika nchi yetu, sikuona kabisa umuhimu wa kwenda kupiga kura katika uchaguzi ujao. Nilikata tamaa kabisa ya kura yangu ya mabadiliko kuheshimiwa.

Ila sasa nabadili gia, natamani hiyo siku ifike haraka nikapige kura tena kuyatafuta maendeleo ya kweli ya Taifa langu.

Kama nawe ulikuwa kama mimi hapo mwanzo, nakusihi siku hiyo hata kama ulijiandikisha mbali safiri nenda kapige kura. Kumbe inawezekana tena.

Ahsanteni sana Watanzania.
 
Mchezo kama vile ndo umeshapata mshindani. Gemu ilikuwa mbovu huku timu pinzani ikijivunia rafu na washindani underdogs. Muda umefika mwanaume karudi mchezoni na hapo ndo patamu. CALL OF DUTY twende tukamalize kwa ari mpya na nguvu mpya.
 
Sio wewe peke yako. Kiukweli watu wengi walikata tamaa. Ukitafakari zile chaguzi za marudio, serikali za mitaa, mabomi, vitisho, wasiojulikana, unakata tamaa kabisa.

Hata hivyo Mungu alijisazia watu bora kabisa wenye kuleta tumaini jipya
 
Chadema mlishawishiana msijiandikishe kwenye dafatari la wapiga kura sasa sijui Lissu atashindaje

Tuna vitambulisho mkononi, tunataka mshinde kihalali basi. Hapo tutajua uwezo wenu wa kushinda kihalali.
 
Chadema mlishawishiana msijiandikishe kwenye dafatari la wapiga kura sasa sijui Lissu atashindaje
Kwani Kuna kujiandikisha mala ngapi? Wengine walijiandikisha mwaka 2015, wengine mwaka Jana wengine mwaka huu kwani Kila mtu ni mtoto mpaka ajiandikishe mwaka huu.

JPEG_20200819_203345_3573860281553247608.jpg
 
Ni wewe pekaako mkuu wenzio kina tindo walikuwa wanahamasishana hawaendi mpaka ikafika hatua wakakejeli viongozi wao waliotoa wito wa kwenda kujiandikisha.

Wapiga kura kwa mujibu wa idadi ya kupika wako 29m, je ulitaka wawe wangapi ili ujue ni idadi sahihi? Wapiga kura 2010 walikuwa 15m+ waliopiga ni 10m+, 2015 walikuwa 22m+ waliopiga ni 15m+, safari hii msema ni 29m. Hiyo ina maana kila baada ya miaka mitano wanaongezeka wapiga kura 7m+. Kwa mtiririko huko kuna wastani wa watu 5m+ wasiopiga kura kila uchaguzi. Hiyo maana yake wapiga kura safari hii hawatazidi 24m. Kwa maneno marahisi wapiga kura 22m waliojiandikisha 2015 ni 90+ ya wapiga kura wa mwaka huu.

Sasa kama kila uchaguzi wanaojiandikisha kupiga kura ni wastani wa 7m, na ndio idadi mliyoleta. Hapo ndio mtafurahi kwa idadi ya kupika. Tunataka tujue hao wapiga kura waliongezeka ni wanaccm tu? Tunataka mshinde kihalali, kisha tutaona vizuri idadi ya wabunge wenu, na kura za rais ili tuone huo ushindi wenu wa 90%+. Ile kuleta mabox yenye kura za ccm yatakaa wazi safari hii.
 
Kwa mwenendo ulivokuwa hapo nyuma wa siasa katika nchi yetu, sikuona kabisa umuhimu wa kwenda kupiga kura katika uchaguzi ujao. Nilikata tamaa kabisa ya kura yangu ya mabadiliko kuheshimiwa.

Ila sasa nabadili gia, natamani hiyo siku ifike haraka nikapige kura tena kuyatafuta maendeleo ya kweli ya Taifa langu.

Kama nawe ulikuwa kama mimi hapo mwanzo, nakusihi siku hiyo hata kama ulijiandikisha mbali safiri nenda kapige kura. Kumbe inawezekana tena.

Ahsanteni sana Watanzania.
Hongera sana kumbuka kupiga kura ya mabadiliko!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom