Madam, umesahau hapo chini kuweka Magufuri oyeeee..
Tamaduni za mtanzania ni kuomba-omba kama mkoma??Anataka tuishi kwa tamaduni zao tuache za kwetu?! Nawewe ukaleta tu huo upuuzi ?
Huyu ni Mkenya fulan tuKwanza haijaandikwa na mtu ambaye English ni first language kwake kuna grammatical errors kadhaa.
As much as sipendi huu utamaduni wa kuchangiana hasa kwenye harusi ila huwa nachanga pale napojisikia kuchanga. Ni utamaduni. Ni kazi sana kubadilisha tamaduni ya mtu kama imezoeleka. Tanzania bado ni nchi ya ujamaa na kusaidiana ni jadi yetu ubaya tu ni kwamba tunasaidia kwenye mambo yasiyo ya msingi ila yale ya msingi hatuchangi. Leo ukiomba pesa upeleke Mtoto shule hamna mtu atatoa, au mgonjwa yupo hospitali watu hawachangi ila akifariki wanachanga misibani. Ingependeza kama tungeredirect michango yetu
Kweli, mtu unapewa kadi kama tano hivi halafu wanakwambia single 50,000 double 100,000 usipochanga watu wanakununia.
Tubadirike aisee Mzungu kaandika point mwanzo mwisho.
Mshahara laki saba unataka kufanya harusi ya milioni 20.
Mtoto anapata kipaimara mnaanza kusumbua watu na kadi za michango ya Elfu 50. (Mbona zamani kwenye vipaimara sherehe tulikuwa tunafanyia sebureni tu).
Tubadirike, Mtu akitaka kufanya sherehe kubwa akakope CRDB watu tushachoka na michango.
Kuna mshikaji tunasoma naye chuo sasa ameamua kuoa halafu anaomba mchango Wa harusi kwetu wanafunzi tumchangie, watu wameahidi sasa kwa unafiki nikaahid elfu ishirini watu wote wametoa nimebaki Mimi na sitoi hata senti kwa sababu huu ni ujinga sana, mwaka jana tena kuna mshikaji hapahapa kaniomba elfu arobaini na wakaniweka kwenye kamati ya harusi bila kunishirikisha hawakuniona hata siku moja kwenye kikao.
Vyovyote vile mkuu, lakini huo ndo ukweli wenyewe!!!!! Wabongo tumezidi, na hasa wanawake hupendi sana mambo ya sherehe kubwa kubwa... Inakera sana aisee.......Huyu ni mzungu kweli au mtanzania aliyekaa nje ya nchi au wa hapa hapa ndani ameamua kutapika nyongo kwa lugha ya malkia ili hasijulikane?
Hai nguruka karibu mbona wwngine wanatoka Titye, au Muhunga huko..harusi inafanyika Dar...Sipendi sana issue ya michango michangi aisee, ukileta kadi huwa naweka kwenye droo. Huu utamaduni kweli watanzania unatuaibisha saaaaana! Mie mahari na harusi yote ilikuwa kwangu, na nilienda kijijini kwa wazazi kufanyia huko nikaachana na ulimbukeni wa watu kwao nguruka wanaenda kufanyia harusi Dar, kisa Dar kuna shangazi yake!
Hahahaaaa, wanatoka Muyama, herushingo, kitanga au kagerankanda lakini wanataka kufanyia Dar kwa Shemeji zao waliooa dada zao!Hai nguruka karibu mbona wwngine wanatoka Titye, au Muhunga huko..harusi inafanyika Dar...