Mzimu wa ‘Bunge Live’ watikisa, wananchi watinga mahakamani

Na wewe ni great thinker? Utakuwa ki/laza bila shaka.. vila/za kama nyie ndo mnarudisha maendeleo yetu nyuma, vinginevyo ni bora ukafumba domo kuficha utumbaf wako
Mkuu huyo ni mpishi wa chai ya wanene pale lumumba, hivyo wacha kumaliza nguvu zako kumjibu huyo
 
Hizi ni mbini za viongozi wa chadema kutumia ruzuku ya chama.
Viongozi walishaona kupuuzwa sasa wanatoka na style nyingine.
 
Mtoa maada tafadhali maneno badala ya wanachi,atumie wanachadema ama Ukawa.
Hayupo mwananchi mjanja wa kuhangaika na mikasa kama hii isipokuwa wapuuz wa ukawa.
 
Hivi ninyi mnaopingana na hoja ya kufunguliwa shtaka LA kudai haki ya MTU kupata habari iliyopo kikatiba mpo timamu? Ingezuiliwa mitandao mingine ya kijamii Kama huu tunaoutumia msingepiga kelele? Ondoeni uumini wa vyama muone ukweli juu ya ukanyagaji wa katiba yetu. Leo wanalo LA kuminya Uhuru wa habari na demokrasia. Mnajua kesho watakuja na lipi lingine lenye maumivu makali kuliko haya? Tafakarini kwa makini kwani wanasiasa wanaona poa tu na hawajali mateso yenu. Kuna siku yatazidi Haya na mengine yasiyobagua itikadi zenu yanakuja. Tutalia wote isipokuwa wao walio juu ya sheria. Msisahau kuwa haki hudaiwa na kupiganiwa. Yale ya misri juu ya Uhuru wa habari hayatoshi kutupa somo?
Wewe ndo huna timamu...mbona pamoja na kutokuwa live bado tunaendelea kupata new update?au malengo yenu nyie ufipa ni kutaka tu kushuhudia sarakasi zenu za demokrasia ya kiziba midomo?
Na bado mtaziba mpaka matako lakini ndo kwanza serikali ya hapa kazi inazidi kuwapuuza.
 
mtoa mada ungesema tu specific kuwa ni wana chadema na wana ukwa kwa pamoja wamefungua kesi kuliko kutumia neno wananchi,maana huo mzimu hauwatesi wananchi bali wanaukawa na wanachadema kwa umoja wao...
Wananchi kwa ujumla bila kujali vyama tunahitaji bunge la wananchi liwe live
 
mtoa mada ungesema tu specific kuwa ni wawna wana ukwa kwa pamoja wamefungua kesi kuliko kutumia neno wananchi,maana huo mzimu hauwatesi wananchi bali wanaukawa na wanachadema kwa umoja wao...
Sio kweli, na wanaochukulia suala la bunge kutoonyeshwa live kuwa ni kitu cha kawaida inabidi wapimwe akili!
 
Sasa hivi ilivyo ni vigumu sana kujua mipaka ya serikali, bunge na mahakama ni ipi? ni kama vile hii mihimili imeunganishwa kua kitu kimoja! Mungu atunusuru tu
Sio kama ndivyo ilivyo!
Bungeni kapandikizwa huyo binti anayejifanya kutosikia ya wakubwa.
Mahakamani huko sijui kumewaje ..
Serikali babe babe kiaina
 
Wewe ndo huna timamu...mbona pamoja na kutokuwa live bado tunaendelea kupata new update?au malengo yenu nyie ufipa ni kutaka tu kushuhudia sarakasi zenu za demokrasia ya kiziba midomo?
Na bado mtaziba mpaka matako lakini ndo kwanza serikali ya hapa kazi inazidi kuwapuuza.
haya subiri nafasi yako ya uteuzi wa bwana utakayekwenda kumtumikia. Utatangaziwa baadaye kupitia jf. Hiyo redio sikilizeni wenyewe kwani ni ya kwanza kuwatangazia taarifa za uteuzi. Halafu unaonyesha mwalimu wako alikufundisha bila kutumia zana ndio maana uelewa wako ni hafifu na dhaifu. Tv live inaelimisha.
 
HATUA ya serikali kuzuia kurusha moja kwa moja mjadala wa vikao vya Bunge kama ilivyokuwa awali, bado inaumiza wananchi

Safari hii wananchi wametinga mahakamani na kwamba leo wamefika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufungua kesi ya kuitaka mahakama hiyo kutengua agizo la serikali la kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Januari mwaka huu, Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Michezo na Sanaa alilieleza Bunge hatua ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya chombo hicho kama ilivyokuwa awali.

Miongoni mwa sababu alizotoa ni kwamba, serikali imekuwa ikibeba mzigo mkubwa wa gharama katika kuendesha matangazo hayo pia watumishi wa umma kutumia muda mwingi kuangalia Bunge badala ya kufanya kazi.

Hatua ya serikali kuzuia kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja imeibua mjadala mkubwa kitaifa ambapo kada mbalimbali nchini zimekuwa zikipinga hatua hiyo.

Katika kesi iliyofunguliwa leo, ina walalamikaji 10 ambao ni Azizi Himbuka, Perfect Mwasililwa, Rose Moshi, Penina Nkiya, Andrew Mandari, Hilda Sigara, Juma Uloleulole, Kubra Manzi, Ray Kimbito na Ben-Rabiu Saanane.

Kesi hiyo imesikilizwa na Profesa Ferdinand Wambari, Jaji Kiongozi katika mahakama hiyo, na jaji mwengine katika kesi hiyo Sakieti Kihiyo, hata hivyo hakuwepo mahakamani leo.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Nape pamoja na George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo Abubakari Mrisho, ndio wakili wa upande wa walalamikiwa.

Kwa upande wa walalamikaji unasimamiwa na Peter Kibatala na Omari Msemo ambao ni mawakili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kesi ya msingi iliyofunguliwa ni kuitaka mahakama kutengua uamuzi uliotolewa na Nape ambaye aliwasilisha kauli ya serikali bungeni.

Walalamikaji wanaitaka mahakama itangaze kuwa, Raia wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wana haki ya kikatiba ya kujua majadiliano yanayoendelea bungeni kwa mujibu wa ibara ya 18(B), (d) na 29 (1).

Pili walalamikaji wamedai kuwa, serikali imekiuka haki ya kikatiba kwa kuzuia bila kuwa na sababu za msingi haki ya wananchi kusikia majadiliano ya Bunge kwa kuzuia kurusha matangazo ya moja kwa moja.

Tatu, walalamikaji wameitaka mahakama kuilekeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejesha haki ya kikatiba ya wananchi kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Nne, walalamikaji wamedai kuwa, matokeo ya kuzuia matangazo hayo ni kunyimwa kwa haki za Watanzania kutokana na kushindwa kuwasimamia pia kuwafuatilia wabunge na mwenendo wao bungeni.

Tano, walalamikaji hao wamedai kuwa, sababu za kuzuia matangazo hayo hazijitoshelezi hivyo Watanzania na walalamikaji wanayo haki ya kupata taarifa ya vikao vya Bunge kwa maslahi ya taifa.

Hata hivyo upande wa utetezi ulidai kuwa, walichelewa kupata taarifa ya mashtaka hayo hivyo hawakupata muda wa kutosha wa kuaandaa majibu. Kutokana na hivyo, mahakama iliuambia upande wa walalamikiwa kwamba, watajibu mashtaka hayo 15 Julai siku ambayo kesi hiyo itatajwa.
mbarikiwe watanzania wa kweli kwa kudai haki ya msingi dhidi ya hili dikteta linaloamua chochote kinachokuja akilini mwake
 
Perfect ni kiongozi wa Chadema Ubungo.... Hiyo kesi imefunguliwa na Chadema ..


Haina mashiko.....
 
Hivi ninyi mnaopingana na hoja ya kufunguliwa shtaka LA kudai haki ya MTU kupata habari iliyopo kikatiba mpo timamu? Ingezuiliwa mitandao mingine ya kijamii Kama huu tunaoutumia msingepiga kelele? Ondoeni uumini wa vyama muone ukweli juu ya ukanyagaji wa katiba yetu. Leo wanalo LA kuminya Uhuru wa habari na demokrasia. Mnajua kesho watakuja na lipi lingine lenye maumivu makali kuliko haya? Tafakarini kwa makini kwani wanasiasa wanaona poa tu na hawajali mateso yenu. Kuna siku yatazidi Haya na mengine yasiyobagua itikadi zenu yanakuja. Tutalia wote isipokuwa wao walio juu ya sheria. Msisahau kuwa haki hudaiwa na kupiganiwa. Yale ya misri juu ya Uhuru wa habari hayatoshi kutupa somo?
Mwenye akili na asikie!. Ubishi wenu wa kutetea uvunjaji wa sheria unaofanywa ktk kipindi hiki mkome.
Mimi nilishawahi kusema humu ndani, naomba nikumbushie usemi wangu tena:
CCM wanafahamu fika kuwa kitendo cha kuzuia matangazo ya bunge live walikurupuka na wantambua wazi kuwa wananchi walio wengi ndani ya CCM na nje ya ccm wanataka wawakilishi wao waonekane live.
Kuna usemi katka kiswahili kuwa '' Mkubwa hakosei, na hata ikitokea kakosea basi huwa hakosei sana kama mtoto mdogo''. Hivyo basi namna pekee ya kurekebisha makosa yao watakuja kuachia matangazo ya bunge live Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ama miezi michache kabla ya uchaguzi ili kutafuta kura.
Hii ya kuruhusu matangazo moja kwa moja kupitia redio ni mbinu tu ambayo ni sawa na kubadili gia ili gari lisogee barabarani liendeleee na safari.
 
1. Nani na lini alianzisha utaratibu wa bunge kuonyeshwa live kupitia TBC1?
2. Jee utaratibu huo ulitokana na sheria mahasusi iliyopitishwa na bunge la kutaka bunge lionyeshwe live na TBC?
3. Kuna kipengele kwenye katiba yetu ya 1977 kinachosema specifically kwamba bunge litaonyeshwa live kupitia luninga ya taifa?
Kumbuka katiba ni sheria mama na kama haijatamuka specifically jambo hili, ni sheria za nchi ndizo zinaangaliwa zinavyosema kuhisu jambo hilo linalolalamikiwa.
4. Kama kipengele hicho cha katiba kipo kwa nini serikali ya awamu ya 3 ya Mzee Mkapa na ile ya 2 ya Mzee Mwinyi hazikufanya hivyo wakati luninga ya Taifa ilikuwapo?
5. Siyo kweli kwamba utaratibu wa kuonyesha bunge live kupitia luninga ulianzishwa katika serikali ya 4 ya Mzee Jakaya? Kama ndivyo jee serikali ya awamu ya 5 ilalazimika kufuata yote yaliyofanyika katika awamu ya 4 hata kama ni mazuri?
5. Aliyeanzisha utaratibu huo (kwa hiari yake) anabanwa na sheria ipi ya kuamua kusitisha utaratibu huo? Serikali ndiyo ilianzisha utaratibu huu kwa hiari yake, sasa kwa nini ibanwe inapoamua kuusitisha kwa sababu yo yote ile?

Nina uhakika majibu ya masuala hayo kwenye Cross examination yatamwezesha hakimu kuamua kama kuna kesi ya kujibu kwa mlalamikiwa au hakuna.

Nisieleweke naingilia suala ambalo liko mahakamani kwani nanyi mmefanyanya hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom