Mzee wangu ananiambia Choo cha ndani Haramu, wakati mi ndicho nakitaka, nifanyeje?

Hbr Za Jioni Wana Great Thinkers.Baada Ya Kusota Sana Na Kupanga Nimeamua Kujenga Room Moja Self Na Sebule Nikivuta Nguvu Za Baadae.Tatizo Mzee Wangu Anasema Choo Cha Ndani Haramu Ananipinga Kabisa Kila Akija Site Ni Kupinga Tu.Nifanyeje Na Mimi Sitaki Kutoka Usiku Na Panga Kwenda Chooni?
Unakaa kibiti au mkuranga?
 
Hbr Za Jioni Wana Great Thinkers.Baada Ya Kusota Sana Na Kupanga Nimeamua Kujenga Room Moja Self Na Sebule Nikivuta Nguvu Za Baadae.Tatizo Mzee Wangu Anasema Choo Cha Ndani Haramu Ananipinga Kabisa Kila Akija Site Ni Kupinga Tu.Nifanyeje Na Mimi Sitaki Kutoka Usiku Na Panga Kwenda Chooni?
Hana maana hiyo
 
Shida ni kuchambia majani....Ameshindwa kukuambia tu kwamba cha ndani unatumia maji
 
Nahisi labda mzee wako anaisi utachimba shimo ndani anaofia harufu na wewe kukosa pa kulala, mweleze aina ya choo na ubora wake, Fanya hayo ukiwa tiari na vifaa vyote vipo hapo site.
 
Mara nyingine lazima tuige wazungu katika mambo ya uamuzi wa maendeleo, maana kuna wazazi wengine wanawaonea uwivu watoto wao, hataki wawa shinde kimaendeleo! Mimi naona usimpeleke tena kwenye site yako! Na usiwe una discuss naye maendeleo yako! Nimeyaona hayo mambo! Alafu sisi watoto eti tunasikiliza, dadeki walahi! Umasikini unakuwa hauondoki!
Jitenge fanya maendeleo yako kimya kimya!
Ubarikiwe ndugu yangu!
 
Kuna aina ya mashetani yanapenda sana kuishi chooni, sasa kujenga choo ndani ya room ya kulala ni sawa na kuishi na hao jamaa wasio na mwili wala sura.
 
Mzee wako yupo sahihi kwan vyoon ndio makazi ya majin, mashetan na jamii zao hivyo si vyema kuiga ustaarabu wa wazungu bila kujua faida na hasara ya unachotaka kukiiga...wallah ahlam
 
Kwanza nakupongeza kwa kufikia hapo pa kuanza kujenga.
La pili ni kuhusu mzazi
Yeye yupo sahihi kwa maana ifuatayo.
Hapajawahi kutokea duniani choose pakawa ni sehemu salama kwa kuzingatia aina ya matumizi.
(1) Choo chako itakuwa kero kwa wengine watakapohitaji hitaji kukitumia
(2) Kitakuwa kero kwako binafsi itakapotokea wengine kukitumia kinyume na utaratibu wako
(3) Vyoo vya ndani vinahitaji usafi wa kutosha ktk utunzaji.Kwa kuwa unachumba kimoja,inawezekana ukawa unahamisha au unapitisha najisi/ uchafu ktk chumba bila kujijua.Mfano wakati mtu amezidiwa na haja ndogo anaweza kudondosha chachizo ndani ya chumba na asifanye Usafi na wewe kukanyaga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom