TANZIA Mzee Nicodemus Manase Banduka afariki dunia hospitali ya Mloganzila

Wapendwa! Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Banduka inasikitika kuwatangazia kifo cha Mhe. Nicodemus Manase Banduka kilichotokea ghafla jana, Ijumaa jioni, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mloganzila.

Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwake Kibaha - kwa Matias. Taarifa kamili ya mazishi itatolewa baada ya mipango kukamilika.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen

Pia soma > Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka?

Nicodemus M. Banduka alikuwa mwanasiasa na kiongozi mashuhuri nchini Tanzania. Alishika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia Juni 1998 hadi Februari 2003.

Kabla ya hapo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera.

Shule ya sekondari inayoitwa Nicodemus Banduka Secondary School ipo, ikionesha heshima kwa mchango wake katika jamii.

View attachment 3229192
Mzee Nocodemus Banduka wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na Wajumbe 18 kati ya 20 wa Tume ya watu 20 iliyotayarisha Katiba ya CCM​
Duuh
 
Pole Kwa familia na Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu

Huyu na Mzee Stephen Mashishanga ni miongoni mwa wale walionyooshwa kwa kipindi chote cha miaka 10 cha Mzee wa msoga,inasemekana walikuwa kwenye kambi ya Sumaye.
Pia kulikuwa na msanii mmoja wa ngonjera aliitwa Salum Tambalizeni yeye alikuwa anampigia chapuo Salim Ahmed Salim kwa muda wote wa Mzee wa msoga hakuwahi kuitwa kutumbuiza kwenye kikao chochote cha CCM na hali yake ya maisha ikawa ngumu kabisa.
Kuna watu wana visasi vya hatari.
 
Umeshachanganya madesa
 
Back
Top Bottom