Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,936
Wapendwa! Kwa masikitiko makubwa, Familia ya Banduka inasikitika kuwatangazia kifo cha Mhe. Nicodemus Manase Banduka kilichotokea ghafla jana, Ijumaa jioni, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mloganzila.
Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwake Kibaha - kwa Matias. Taarifa kamili ya mazishi itatolewa baada ya mipango kukamilika.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen
Pia soma > Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka?
Nicodemus M. Banduka alikuwa mwanasiasa na kiongozi mashuhuri nchini Tanzania. Alishika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuanzia Juni 1998 hadi Februari 2003.
Kabla ya hapo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera.
Shule ya sekondari inayoitwa Nicodemus Banduka Secondary School ipo, ikionesha heshima kwa mchango wake katika jamii.
Mzee Nocodemus Banduka wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na Wajumbe 18 kati ya 20 wa Tume ya watu 20 iliyotayarisha Katiba ya CCM