Muasisi wa klabu ya simba na Red star ambaye pia ni mmoja wa wadhamini wa klabu ya Saigon Mzee Issa Ausi amefariki atazikwa Jumatano kwenye makaburi ya Ndugumbi magomeni saa 7 mchana. Tar 7/5/2017.
Marehemu Mzee Issa Athuman Ausi!
Umma wa Wana Dsalaam umemiminika leo ktk mazishi yake licha ya mvua kubwa iliyonyesha! Jeneza lake limepelekwa kwa miguu toka Msikiti wa Idrissa kariakoo hadi makaburi ya Ndugumbi Magomeni Makuti! Haya yamefanyika kwa mapenzi ya vijana wa kariakoo licha ya magari zaidi ya hamsini kuwepo!Msafara huo umepokezana jeneza mkono kwa mkono hadi makaburini!