Mzee Cheyo: Inaonekana Serikali haina nia ya dhati kwenye suala la Katiba Mpya

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
14,373
53,829
Akiongea kwenye kikao cha wadau wa masuala ya siasa nchini.

Amesema kuwa hoja za serikali za kutaka watanzania wapewe elimu kwanza ndo tuanze kujadili habari za katiba ni chenga ya kutotaka wananchi wapate katiba mpya

1. Kahoji ni elimu gani ya katiba inayohitajika ambayo haikutolewa na Jaji Nyalali, Jaji Kissanga na tume ya Jaji Warioba?

2. Kahoji inakuwaje serikali inataka kutapanyatapanya hela za wananchi wakati walishatumia mapesa mengi ya bunge la katiba miaka kadhaa iliyopita?

3. Kahoji kuwa iweje mchakato uanzishwe kwa mamlaka ya rais wa awamu ya nne halafu rais wa awamu ya sita aone hilo suala halina maana?

4. Kahoji kuwa inakuwaje rais anayesema hatuwezi kuanzisha mchakato wa katiba mpya mpaka watanzania wapate elimu, lakini rais huyohuyo ndiye aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba?

5. Kahoji kuwa Wazanzibar waliandika katiba yao mwaka 2010 amabyo waliifanyia mabadiliko makubwa katiba yao ya mwaka 1984, ni elimu gani waliyopewa Wazanzibari kabla hawajaandika hiyo katiba?

6. Kisha mzee Cheyo akatoa usia wa kiutu uzima kuwa SERIKALI IINVEST KATIKA AMANI. akimaanisha kuwa kuchezeachezea mahitaji ya msingi ya wananchi kama katiba bora ni kuchezea amani.

Unaweza kumsikiliza hapa:


View: https://youtu.be/WyCGGV88fbc?si=ufm0PvbNtiZZfDFp
 
Ukiona mdau wa CCM kindakindaki anaongea hivyo,ujue kuna ukweli wa 100%🤔
 
CCM bila katiba ya 1977 ni chama mfu
 
Baada ya mkataba wa Bandari, issue za kuhamisha wamasai ngorongoro,mkataba na hili la katiba na mengineyo haya ndio makaburi ya bi kidude, 😁😁
 
Samia alikuwa msaidizi wa Kikwete aliyeanzisha mchakato wa katiba mpya, Leo Samia huyohuyo anaona Samia yule aliyeunga mkono mchakato wa katiba mpya hadi akawa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba ni Samia tofauti na yeye.

Power corrupts, absolute power corrupts absolutely!
 
Hawa ndio wale kila kitu jogoo kaona jogooo
 
Yarabi
Samia anatupeleka pabaya
 
Unakunya mavi kisa yananuka unasema hayajatoka tumboni kwangu ndo huyu saramila sasa,,,,,?mama mwehu huyu
 
Mzee wa mapesa toa neno "Inawezekana" nia ya dhati Hakunaga!! Ni mwendo wa danadana kila atakaeingia!!
 
Huyu mzee huwa ni geukageuka kama upepo, hivi si ndiye aliungana na Chapa ya Jogoo Magomeni Usalama kuwaponda wapinzani wenzao huyu!!
 

Mzee ana akili huyo, maoni yake note taken
 
Akina Lissu waliona mbali... acha wauze sura mwisho wa siku wadake Posho hapo wameenda kudhalilika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…