Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 14,365
- 53,814
Akiongea kwenye kikao cha wadau wa masuala ya siasa nchini.
Amesema kuwa hoja za serikali za kutaka watanzania wapewe elimu kwanza ndo tuanze kujadili habari za katiba ni chenga ya kutotaka wananchi wapate katiba mpya
1. Kahoji ni elimu gani ya katiba inayohitajika ambayo haikutolewa na Jaji Nyalali, Jaji Kissanga na tume ya Jaji Warioba?
2. Kahoji inakuwaje serikali inataka kutapanyatapanya hela za wananchi wakati walishatumia mapesa mengi ya bunge la katiba miaka kadhaa iliyopita?
3. Kahoji kuwa iweje mchakato uanzishwe kwa mamlaka ya rais wa awamu ya nne halafu rais wa awamu ya sita aone hilo suala halina maana?
4. Kahoji kuwa inakuwaje rais anayesema hatuwezi kuanzisha mchakato wa katiba mpya mpaka watanzania wapate elimu, lakini rais huyohuyo ndiye aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba?
5. Kahoji kuwa Wazanzibar waliandika katiba yao mwaka 2010 amabyo waliifanyia mabadiliko makubwa katiba yao ya mwaka 1984, ni elimu gani waliyopewa Wazanzibari kabla hawajaandika hiyo katiba?
6. Kisha mzee Cheyo akatoa usia wa kiutu uzima kuwa SERIKALI IINVEST KATIKA AMANI. akimaanisha kuwa kuchezeachezea mahitaji ya msingi ya wananchi kama katiba bora ni kuchezea amani.
Unaweza kumsikiliza hapa:
View: https://youtu.be/WyCGGV88fbc?si=ufm0PvbNtiZZfDFp