hermanthegreat
JF-Expert Member
- Mar 2, 2021
- 1,194
- 3,024
Habari wanajf.
Leo nimeona sio mbaya namimi nikishare na nyinyi story yangu fupi nilipokuwa shule.
Hatimaye matokeo yakatoka nimefaulu kwenda sekondari.
Nilkuwa si mtu wa kujichanganya sana hivyo sikuwa famous kabisa pia nilkuwa mtiifu sana nafanya kila kitu kwa mda.
Nikiwa form one bado mwezi wa tatu tulifanya mtihani wa English course, matokeo yakatoka nikawa mtu wa pili kati ya watu 300.
watu wakaanza kunifatilia, basi tukafunga shule.
Shuleni kulikuwa na utaratibu wa kutoa morning speech kila jumatatu.
Shule ilipofunguliwa mwezi wa nne nakumbuka siku moja tukiwa parade niliitwa kwa kushtukizwa na academic prefect nitoe morning speech.
Nilishangaa sana kwakuwa sikuwa nimejiandaa na ukizingatia bado Niko form one na sijawahi kuzungumza mbele za watu.
Nilitumia kama dakika 10 kuzungumza nilisimulia story kuhusu safari ya Musa na wana Israel kwa kiingereza na hapo ndio ilikuwa mwanzo wangu wa kuwa famous zaidi pale shule.
Nikaanza kushirikishwa pia kwenye midahalo mbalimbali pale shule.
Mwezi wa 8 ulipofika ndio ilikuwa mwezi wa uchaguzi , madam wangu wa English alinishawishi nigombee uongozi kitengo Cha English Promoter.
Nilikubali na kuanza harakati zangu za kugombea, kila darasa nililokuwa napita nilikuwa nashangiliwa sana ukizingatia nilikuwa naonekana mdogo ki umri watu walinikubari sana, nilitembea madarasa yote form one hadi form four na nilkuwa na ushawidhi mkubwa sana,
Wapinzani wangu wawili walikuwa wanatokea madarasa ya form three.
Matokeo ya kura yalitoka na nilikuwa mshindi wa pili kwa wingi wa kura. Mwisho wa siku tuliapishwa hao washindi wawili na kuanza kazi.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuchukiwa. Niliwadeal watu hasa nikiwa kama English Promoter kila nilipopita nikiwa shule watu walikaa kimya kwa kuhofia kuzungumza kiswahili
Kila siku jioni majina ya swahili speakers yalikusanywa kutoka kwa viongozi wa madarasa kisha yanasomwa pale mbele parade nawapatia adhabu.
Nakumbuka kaka angu alikuwa monitor wa form two, kuna siku nikiita viongozi wa madarasa wanipatie majina kama hawana wanakula adhabu viongozi hao akiwemo na yeye akaanza kunichukia hadi leo.
Waliokuwa wananikubali na kunishangilia wakaanza kunichukia. Siku zikakata hatimaye form two.
Uchaguzi ukafika, nikatuma maombi ya kugombea àa tena , mda huu niliomba nafasi ya kuwa academic prefect.
Majina yakakusanywa walimu wakakaa kikao kupitia majina ya tulioomba nafasi mbalimbali za kugombea wakatoa list yao baada ya kuwa wametufanyia interview wakabandika kwa school board majina ya waliopitishwa kufanya campaign.
Nilipoenda kucheck jina langu nilishangaa nilipokuta sijawekwa kugombea kama Academic prefect baadala yake niliwekwa top kugombea nafasi ya Head boy..
Nilijua kabisa sitopata kula za kunitosha kuwa kiongozi kwasababu watu hawanitaki Tena.
Sikupiga campaign, katika nafasi hiyo tulikuwa watu wawili, mimi na jamaa wa form three aliyekuwa general Secretary katika uongozi uliopita.
Matokeo ya uchaguzi yalitoka nimeshindwa katika nafasi ya kuwa Head boy hivyo , utaratibu uliokuwepo enzi hizo ni kwamba ukishindwa kuwa Head boy unakuwa General Secretary (GS)
Basi nikateuliwa kuwa GS nikaapishwa nikaanza kazi
Mda huu nilipiga sana kazi kwasababu secretary ndio mtendaji mkuu katika serikali ya wanafunzi.
Nilikuwa mpole lakini kuogopwa na kuchukiwa sana.
Miezi ikasonga hatimaye form three, uchaguzi ukafika mda huu sikuwa na uhakika wa kupata hata kula moja pale shule mbali na kuwepo kwa wanafunzi zaidi ya 1000,
Watu wakatuma maombi ya uongozi na mimi nilituma maombi ya kugombea nafasi ya Head boy.
Nikaitwa Interview walimu zaidi ya 40 wananitazama na kuniuliza maswali, lakini sikuogopa niliwajibu vema kabisa.
Hatimaye wakatoa majina ya watu waliopita kwenye interview, nilichek jina langu nikakuta nimepitishwa lakini nilipotazama vizuri niligundua nipo peke angu kwenye list ya wanaohitajika kugombea nafasi ya Head Boy yaani ni either u vote Yes au No ila mtu ni mmoja tu.
Nilipita uchaguzi japokuwa 98% ya kura zilikuwa No.
Na hiki ndicho kipindi ambacho sitokisahau maana nilkuwa kiongozi asiyekuwa na huruma.
Niliwahi kumchapa viboko dogo mmoja wa form one baada ya kumuita akakataa kuja , na kwa vile alikuwa mgeni alikuwa hanifahamu, niliwaagiza mascout wamkamate dogo Kisha wamuingize darasani wakaleta na viboko vingi nikafunga mlango nilimcharaza sana mboko yule mtoto hadi namwachia alitoka mbio anakimbia Hadi kwao , kumbe alikuwa mtoto wa Padre, siku iliyofuata kesi ililetwa shule , ila headmaster aliimaliza kimtindo akanionya kuchapa wanafunzi viboko.
Niliwahi kuwapigisha push ups form four (akiwemo kaka angu) kuanzia asubuhi hadi mchana kwa kosa la kupiga keleke parade.
Nilikuwa naogopwa sana kipindi hiki, nilipoteza marafiki, niliishi maisha ya upweke sana.
Nilitishiwa sana mtaani, nilipokea vitisho vingi vya kurogwa lakini hakuna kilichotokea
Hatimaye nikahitimu kidato Cha nne, kwenye mahafari nilipokea vyeti vitano, yaani cheti Cha uongozi, taaluma (nilikuwa wa kwanza kwenye mitahani yote kuanzia form one mwishoni Hadi form four), cheti cha physics, Chemistry na English.
Nilipoenda A, level kwa mara ya kwanza nipo form 5 natoa maoni kwenye school baraza nilishangaa watu wananikubali nikaanza kupata wafuasi , sikutaka kabisa story ijirudie nikaanza kuishi maisha yangu mwenyewe nikajiweka mbali kabisa na maswala ya uongozi.
Maisha niliyoyaishi nilipokuwa sekondari naziona athari hadi leo, yalifanya nizoee maisha ya kujifungia ndani mwenyewe, kuishi bila marafiki, kuhisi kila mtu ananichukia, japokuwa naona kama nguvu ya ushawishi bado ninayo.
Nazidi ku recover mdogo mdogo na maisha yanaendelea.
Karibu nawewe usharee visa ulivyokumbana navyo ulipokuwa kiongozi shuleni.