My Last Ride; Safari yangu ya Mwisho.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
28,983
69,624
MY LAST RIDE; SAFARI YANGU YA MWISHO.
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Episode 01.

Sikumaanisha kuua! Wala sikuwahi kuwaza kuwa kuna siku nitakuja kuua mtu. Kwa kweli ningefanya dhambi zote, zote! Lakini sio dhambi ya kumwaga damu ya Mtu. Haya sasa nini kimetokea? Nani kaniloga! Mungu wangu!

Nimeua! Nimeua! Dimoso Mimi Nimeua!
*********

Jina langu naitwa Dimoso. Wengi huniita D, ukifika hapa kiwangwa hutonipata kama utaulizia Dimoso, ingawaje ni jina langu lakini wengi hawalifahamu. D ndio jina Maarufu zaidi. Hilo Mpaka mtoto mdogo ungemuuliza angekuleta mahali ninapoishi kama angenikosa kijiweni mahali ninapofanyia Kazi ya bodaboda, yaani udereva pikipiki.

Ni Miaka miwili sasa tangu niingie katika Kazi ya ubodaboda. Baada ya kumaliza Masomo yangu ya elimu ya juu katika Masuala ya tehama kwenye IT "Shahada ya information Technology" katika Chuo cha DIT. Nilikula msoto haswa nikiwa napambana huku na huku Kutafuta Kazi katika fani niliyosomea.
Lakini jitihada zangu ziligonga mrama na mipango kwenda kombo baada ya tumaini la Kupata Kazi kuyeyuka Kabisa.

Nilihisi kukata tamaa. Nuru ya mafanikio ilimezwa na wingu jeusi la kushindwa. Sasa nikaanza kulia na kujilaumu. Machozi yangu yangemwagika chini kwenye Udongo huenda miche iliyopo udongoni ingeweza kustawi. Yalikuwa machozi Mengi Sana. Lakini haikuwa hivyo. Upepo WA mashaka uliyapeperusha machozi yangu na kuyakausha bila kuacha alama. Ni kwamba hakuna aliyeyaona machozi yangu. Wala hakuna aliyejua kuwa ninalia. Hakuna aliyekaribu Wala aliyejali hali niliyokuwa naipitia.

Kilikuwa Kipindi kigumu Sana kwangu.

Maisha ya Dar es salaam yakanishinda sikujua kama nikiondoka Dar niende wapi. Kurudi nyumbani Morogoro isingewezekana. Ningerudi vipi nikiwa katika Hali kama Ile. Hali ya kushindwa, kuchoka na kukata tamaa. Wazazi wangu wangenitazamaje Mimi? Wangejisikiaje! Mimi kwao nilikuwa kama Jemadari wa vita waliyemuamini Sana. Shujaa wa ukombozi wao. Ati Leo nirudi kichwa chini Mikono nyuma. Hapana! Hiyo nilikataa.

Nayakumbuka Maneno yangu ya kishujaa niliyowaahidi yakuwa ninaenda Chuo kikuu Dar, nikimaliza nitawapa maisha Mazuri. Nitawabadilishia hali ngumu ya umaskini waliyonayo.

Nakumbuka siku Ile Mama yangu akiwa ananisindikiza kituo cha Magari, naikumbuka siku Ile vyema. Nikamwambia Mama; Wakati umefika Mama kuyala matunda yako. Kitambo kidogo unafurahia Kazi uliyoifanya Kwa Miaka mingi. Ulinisomesha ili uishi Maisha mazuri. Nakuahidi Mama. Jambo hilo halipo Mbali tangu Leo"

Siku Ile Mama yangu alikuwa anatabasamu Muda wote. Uso wake uliozingirwa pande zote na mikunjo ya lishe Duni ilipingana vilivyo na tabasamu lake. Niliona nuru ya tumaini ikichomoza katika macho yake. Akanikumbatia kisha akanong'ona nyuma ya mgongo wangu Akiwa amenikumbatia. Baba yako atajivunia sana. Natamani angekuwepo.

Hayo yote nayakumbuka.
Chaguo pekee nililokuwa nalo wakati huo lilikuwa kwenda Kiwangwa, huko Bagamoyo ambapo rafiki yangu wa Chuo aliniitia Kazi ya ujenzi, niende kama Saidia Fundi. Nikaenda. Huko ndiko maisha nilipoyaanzia.
*"

Ulikuwa Ujenzi wa kiwanda cha Nondo na bati. Ilikuwa Kazi ngumu Sana lakini sikuwa na budi kuifanya ili kunusuru maisha yangu. Tayari Mimi ni mwanaume. Unafikiri nani mwingine angeweza kunisaidia kama nisipojikaza na kujisaidia mwenyewe.
Wakati wote nilikuwa nikiishi kwa rafiki yangu. Nilikaa kwake karibu mwezi na nusu Mpaka pale Ujenzi wa kile kiwanda uliposimamishwa kwa Amri ya serikali.

Pesa niliyokusanya ilinisaidia kununua mahitaji yangu ya kuanzia maisha kama kitanda na godoro pamoja na vitu vingine vidogovidogo. Nilimuaga rafiki yangu. Kwa sababu alinifanyia uungwana Sana. Nilimshukuru kwa ukarimu na Msaada alionipatia kwa Kipindi chote nilichokuwa kwake. Ingawaje kilikuwa chumba kimoja na sebule lakini kwangu ilikuwa kama nyumba kubwa iliyonipa utulivu.

Sasa nikaanza Maisha ya kujitegemea, nikiwa nimechukua chumba na sebule mtaa wa tatu kama sio WA nne kutoka alipokuwa amepanga Rafiki yangu.

Nilitegemea mgogoro uliopo baina ya wamiliki WA kiwanda na serikali ungeisha mapema lakini miezi miwili iliisha mambo yakiwa hayaeleweki. Pesa ya akiba ilikuwa imeisha, Kodi nyingine ilikuwa IPO karibu.
Kichwa kilianza Kupata Moto. Nifanye Kazi gani hapa Kiwangwa. Bahati mbaya au nzuri niseme rafiki yangu yeye alibahatika Kupata Kazi serikalini mwezi Mmoja uliofuata baada ya kiwanda kufungwa. Hivyo yeye aliondoka na kwenda Wilayani Kiteto, huko Manyara. Yeye ndiye alikuwa mwenyeji wangu pale Kiwangwa. Hata hivyo tayari nilikuwa nimeshaanza kupazoea na kuzoeleka na wenyeji wa Kiwanga.

******"****
Sikubaliani na wanafalsafa wanaosema maisha ni uchaguzi wa Mtu binafsi. Nakataa. Kwa sababu kama maisha yangekuwa ni uchaguzi wa Mtu binafsi Mimi Wala nisingechagua maisha haya niliyokuwa nayo. Maisha ya kukimbizana na matatizo baada ya matatizo. Maisha ya Kulala njaa. Maisha ya kusimangwa na wenye nyumba.
Ingekuwa ni Maisha yangu ni uchaguzi wangu binafsi ningeenda kufunga chemchem ya matatizo na mikosi iliyokuwa inayaandama maisha yangu.

Mbele yangu alikuwepo Mzee wa Makamo, mwenye sura ya mzaha lakini ndevu zake alivyoziweka zilikinzana na sura yake. Aliziweka ndevu kama Mtu mtata hivi. Sijui kama unamjua Adolf Hitler jinsi alivyokuwa anaziweka ndevu zake. Kama unamjua basi ndivyo huyu Mzee wa Makamo alivyoziweka. Lakini tofauti yake na Hitler ni kuwa Mzee huyu alikuwa na sura ya mzaha.

tuliingia katika mkataba wa pikipiki. Kwamba Mimi nitachukua pikipiki na kuitumia kwa miezi kumi na mbili kisha itakuwa yangu. Lakini itanipasa kila siku nimpelekee Mzee huyu shilingi elfu kumi za kitanzania. Bila kurusha hata siku Moja.
Ikitokea nimerusha siku Moja basi mkataba nimeuvunja mwenyewe na pikipiki ataninyang'anya.
Kuhusu matengenezo ya pikipiki vyote nitafanya Mwenyewe.

Sikuwa na namna zaidi ya kukubali ingawaje masharti yalikuwa magumu. Muda ule nilichokuwa nawaza ni namna ya kuweza kuishi kwa Muda ule. Kupata chakula na Kupata pesa ya Kodi ya mahali ninapoishi ambapo ilikuwa imebaki mwezi Mmoja tuu.

Nikachukua bike nikarudi nayo nyumbani. Nikajiweka zangu kitandani, kisha nikashusha pumzi nzito unhuu! Nikajilaza kitandani, Mawazo yakaanza kunipitia. Daah! Leo nimekuwa bodaboda! Sijui nitaifanya Kazi hii kwa Muda gani. Lakini Sina namna. Muhimu nifanye nimiliki hiki chombo. Yatakuwa mafanikio makubwa Sana.
Punde simu ikaita. Alikuwa ni Mama. Nikapokea;
" Hello Mama! Shikamoo"
" Marhaba mwanangu. Unaendeleaje huko"
" Nashukuru Mungu Mama" Nikasema nikiwa nimeiweka Sauti yangu kwa namna nzuri kuonyesha Sina tatizo.
" Naomba unitumie hata elfu mbili nikanunue unga nipike. Mboga nilichuma Shambani. Sina hata pesa mwanangu"
Mama aliongea kwa sauti ya unyonge Jambo ambalo liliamsha hisia zangu za ndani.
" Usijali Mama, nakutumia, pole Sana mama kila kitu kitakaa sawa"
Nikasema kisha simu ikakatika, nahisi salio la mama lilikuwa limeisha.
Sikuwa hata na Akiba ya Mia Mbovu.
Kama ni kupekua kwenye mifuko ya suruali Kazi hiyo niliifanya Jana. Hakuna pembe Wala Kona ambayo sikuipekua siku ya Jana nikiwa natafuta hata Mia mbili ili niweze Kupata pesa ya mandazi.

"Niende kwa nani nikamkope?" Nikawa najiuliza huku nikiwa nakuna kichwa. Nilikuwa nimetingwa haswa. Mama yangu alale njaa na Mimi nipo. Hapana.

Nikatoka, nikaenda kwenye Duka ambalo lilikuwa mtaa wa pili tuu. Nilijaribu kumkopa muuza Duka lakini alinikatalia akaniambia anachoweza kunisaidia ni kunikopesha bidhaa zake kama unga au mafuta. Sasa hata kama akinikopesha unga au mafuta nitayatumaje Morogoro kwa Mama.
Nikaondoka zangu, lakini nikasema si bora ningechukua nikayatumie mwenyewe. Nikarudi tena lakini mara hii muuza Duka alikataa kabisa hata kunipa bidhaa hizo.

Nilikasirika Sana. Njiani nilitembea kama Kipofu. Nilikuwa na msongo wa mawazo.
Katika Hali isiyo ya kawaida nikajikuga nimeanguka chini na gari likiwa limenigonga. Nikapoteza fahamu. Sikujua nini kiliendelea.
********

Nimekuja Kupata fahamu ni masaa mawili baadaye. Nikiwa katika kituo cha afya cha Kiwangwa. Napiga kelele. Mama! Mama! Jamani mama yangu!
Anaingia mwanamke aliyevalia nguo nyeupe, baadaye nilijua NI muuguzi.

"Vipi unaendeleaje Dimoso" Yule muuguzi akanisalimu akiwa ameikumjua sura yake kwa tabasamu lenye kuweza kutibu.
" Nataka kuongea na Mama. Tafadhali naomba simu yangu"
" Dimoso, hukuletwa hapa na simu. Waliokuleta hapa Mmoja wapo alisema anaitwa Bihawa, mwanamke ambaye ni Jirani yako akasema unaitwa Dimoso"
" Okay! Anyway naomba simu yako nimpigie Mama. Tafadhali"
" Usijali Dimoso, nitakupa. Nataka Kwanza nikupe matibabu kisha mengine yataendelea "
" Hapana! Mimi naendelea vizuri! Nipe simu niongee na Mama yangu tafadhali"
Hapo nilikuwa nimeamka kitandani, niliongea Sauti ya ukali Sana huku nikiwa nimetoa macho. Nikatoka kuamka lakini mkononi nilikuwa na Dripu. Iliyonitonesha mahali nilipokuwa nimechomwa.
Mtonesho huo uliita maumivu katika Maeneo mengine ya mwili wangu. Nikaanza kuhisi maumivu kwenye Paja la kulia, nyuma ya mgongo na kwenye bega.
Nikagugumia, aaaahh!
" Tulia Dimoso bado hauendelei vizuri. Lala! Haya jiegemeze hapo kwenye MTO"
Muuguzi akasema Sauti yake ikiwa Mbali na upole.
Nikajiegemeza kwenye ule mto wa kile kitanda. Yule muuguzi akaja karibu akanipa simu. Nikaipokea. Nikabonyeza bonyeza namba, kisha nikaweka sikioni. Ikaita lakini haikuwa inapatikana. Nikajaribu tena ikawa haipatikani.
"Shiit" nikasema huku Uso wangu ukionyesha kukata tamaa.
" Vipi haipatikani" muuguzi akaniuliza huku anitazama kwa macho ya kupima hisia zangu. Nikamtazama bila kusema kitu.

"Itakuwa simu yake imezima chaji. Maskini huenda alisubiri mpaka akachoka" nikasema kwa sauti ndogo. Muuguzi akiwa ananitazama. Kisha akachukua kipima mapigo ya moyo na kipima presha cha kisasa akanipima. Kabla hajamaliza Mlango ukafunguliwa Mimi ndiye niliyegeuka muuguzi hakugeuka alikuwa akiendelea kunipima. Alikuwa ni Bihawa ambaye ni mwanamke Jirani yangu.

Bihawa alikuwa amebeba hotpot pamoja chupa la Maji na machungwa. Akawa amesimama huku akinitazama kwa macho ya huruma. Baada ya muuguzi kumaliza kunipima akaniambia ninaendelea vizuri.
Kisha akaenda kwenye meza iliyokuwa mule kwenye Ile wodi akachukua kifuko ambacho bila Shaka alikuwa amekuja nacho. Akatoa Dawa kadhaa kisha akawa ananipa maelekezo;
" Hii ni antibiotics, utakunywa mbili mara tatu. Kila baada ya saa nane.
Hii ni antipain, Dawa ya kutuliza maumivu. Utakunywa nayo hivyohivyo. Kila ukinywa hii antibiotics unameza na hii. Usipishanishe Muda. Sawa.
Nimesahau, wewe ulisema ni mkewe au ?"
Muuguzi akamgeukia Bihawa, mwanamke aliyevalia baibui ambaye harakaharaka utagundua ni mtu mwenye kuipenda Dini yake.
Swali hilo likanifanya nimuangalie Bihawa, naye Bihawa alikuwa akinitazama kisha akamjibu muuguzi huku akiwa ananitazama;
" Aam aa! Ni majirani tuu. Yeye ni jirani yangu"
" Mbona kigugumizi bidada! Okay. Nashindwa kukuachia maagizo. Huyu anaishi na Nani kwani?"
" Nipe tuu maagizo muuguzi"
" Hapana! Nahitaji kumpa maagizo mtu anayeishi naye. Sio kila Jambo ninaweza kukuambia wewe kumhusu Mgonjwa"
" Nimekuambia niambie Mimi. Nani aliyemleta hapa? Sio Mimi niliyemleta? Nani kamletea chakula hapa? Ni Mimi au hunioni?"
Nilipoona wanataka kugombana ikabidi nizungumze.
" Muuguzi, Mimi pale naishi mwenyewe. Mji huu Mimi ni mgeni. Hivyo Bihawa anaweza tuu kusikia unachotaka kumwambia"
" Oooh! Kumbe! Sasa si angesema hivyo. Sina haja ya kumpa maelekezo kukuhusu. Sheria zangu za Kazi haziruhusu. Kama ni Kula kwa wakati nitasimamia Jambo hilo mwenyewe.."
Muuguzi akamaliza kisha akatoka, Muda huo Bihawa akawa anamsindikiza na macho ya chuki.

Alipotoka na kufunga mlango. Bihawa akaachia bonge la msonyo. Kisha akanigeukia.
" Huyu nesi hamnazo huyu. Atakuwa anakutaka sio Bure."
" Mmh! Sidhani. Nafikiri anafanya Kazi yake"
" D huna ujualo kuhusu Sisi wanawake. Tangu nimeingia hapa nimemwona namna anavyokuangalia na anavyokuongelesha"
" Hapana Bihawa! Ni Mtazamo wako tuu"
" Unamtetea si ndio?"
" Simtetei! Haya tuachane na hayo!"
" Kama anataka Umalaya si akafanye huo Umalaya wake. Mtcheeeewwi!" Akasonya.
Kisha akatoa lile hotpot kwenye kikapu na Sahani akapakua chakula. Akanipa, kisha akaendelea kumenya chungwa Muda wote ananiangalia kwa macho ambayo sasa nilianza kuyaelewa kwa namna nyingine Kabisa.

Baada ya kula chakula, akaniaga lakini nilikumbuka kuhusu simu yangu. Nikamuuliza simu yangu iko wapi. Akaniambia alipofika eneo nilipokuwa nimegongwa kulikuwa na watu wengi. Hakunikuta na simu.
Nikajua simu yangu ilikuwa imeibiwa.

Kesho yake niliruhusiwa, aliyenileta nyumbani alikuwa ni Yule muuguzi aliyekuwa ananiihudumia tangu siku ya Kwanza. Jina lake alikuwa akiitwa Cathy.

Tulipofika nyumbani kwangu nilimkuta Mzee Abeid ambaye ndiye mwenye Ile bodaboda. Moyo wangu ukapiga paah! Cathy aliona Hofu yangu tukiwa tunakaribia. Akaniuliza kulikoni nikamweleza kwa kifupi hali ilivyokuwa.
Tayari tulikuwa tumefika, nikamsalimu Mzee Abeid naye akanipa Pole ingawaje nilijua alichokifuata pale.
Nikamwambia ngoja niingie ndani alafu nataka kwaajili ya mazungumzo.
Akaniambia hajaja pale kuzungumza na Mimi.
Nikaingia ndani nikiwa na Cathy. Tulipofika ndani Cathy akatoa noti mbili za elfu kumikumi akanipa.
" Kampatie hizi huyo Mzee" akasema,
Nikatoka nikiwa nimezibeba zile pesa. Nikamkabidhi Mzee Abeid, nikamuona akijichekesha hovyohovyo kisha tukaagana.

********

Miezi mitatu ilipita nikiwa tayari nimezoea Kazi ya ubodaboda. Cathy ndiye aliyekuwa amenilipia shilingi Laki tatu za kujiunga kwenye kijiwe cha bodaboda.
Kila kijiwe cha bodaboda kilikuwa na Ada ya kujiungia kwa mara ya Kwanza kwa dereva bodaboda mpya. Bila kutoa Ada hiyo usingeruhuziwa kukaa kwenye kijiwe au kituo hicho cha bodaboda.

Mahusiano yangu na Cathy yalizidi kuimarika ingawaje hakuna miongoni mwetu aliyemuelezea Mwenzake hisia zake. Hata hivyo mioyo yetu ilikuwa kama sarafu moja. Nilihisi kumpenda Sana Cathy naye alionyesha hivyo.

Cathy alikuwa mwanamke Mzuri Sana. Msomi mwenye elimu ya Shahada ya uuguzi. Macho yake mazuri yenye huruma yalifanania Kazi yake ya kuhudumia wagonjwa. Sura yake ilikuwa nzuri pengine hiyo ilimfanya watu wengi wamuone kama ananyodo. Umbo lake lililopangika lilivutia Sana hasa alipokuwa Amevaa Sare zake za Kazi.

Nilikuwa najua Cathy anasubiri kwa Hamu nimwambie ninampenda kisha safari yetu ya Mapenzi ianze upya.

Ni miezi mitatu sasa imepita. Sijui nianzie wapi kumueleza ukweli wa Moyo wangu Binti huyu. Kipato changu ni Duni. KAZI yangu ya kufukuzana na upepo. Ubodaboda. Nitampa nini mwanamke msomi mwenye Kazi yenye kipato zaidi yangu. Nikifikiria hali yangu hiyo ilinifanya nifute Kabisa Wazo la kumwambia Cathy ukweli.

Kama haitoshi, tetesi na duru za mtaani nilizokuwa nazipata zilikuwa zinasema matajiri wa Kiwangwa walikuwa wakiingia na kutoka wakipigana vikumbo kulipata penzi la Cathy. Nilikata tamaa Kabisa niliposikia tajiri anayemiliki kile kiwanda cha Nondo na bati nilichokuwa nafanyia Kazi pia anamfuatilia Cathy. Embu fikiria hata wewe, ungethubutu.?

Unaweza kuniambia nijaribu, mwanaume kujaribu na kujiamini. Hata Mimi kuna wakati nafikiri kama wewe. Lakini Sauti nyingine hunong'ona masikioni mwangu ikiniambia akinikataa nitakosa hata ule ukaribu mdogo niliokuwa nao dhidi yake.
Nikifikia hapo naghairi.

Bihawa naye hakuwa nyuma, yeye ndiye alikuwa ananiona karibu kila siku kwani alikuwa ni lazima kila jioni aniletee chakula cha usiku. Nilishindwa kumkatalia na ningeanzaje kumkatalia mwanamke ambaye alinisaidia kwa gharama zake Kunichukua nikiwa sijitambui siku Ile ya ajali Mpaka Hospitalini kisha akawa ananiletea chakula na hata gharama za matibabu yeye ndiye aliyetoa. Ningewezaje? Nakuuliza!

Licha ya kuwa Bihawa alikuwa mwanamke Mzuri mwenye stara lakini Moyo wangu haukuanguka kwake. Sikuwa nahisia naye. Lakini nitamlipa nini kwa haya anayoendelea kunifanyia. Kila anapokuja kwangu nahesabu deni linaongezeka juu yangu kwake.

***********
Jioni Moja nikiwa nimetulia ghetto kwangu nilimkumbuka Mama yangu. Ni miezi kadhaa imepita sijawasiliana naye Hali ya majuto na kujilaumu kwa kutokumjali MMA yangu vikaukumba moyo wangu. Haikuwa kawaida yangu Mimi kukaa Muda wote huo bila kuwasiliana na Mama yangu. Kikawaida ilikuwa kila siku lazima niwasiliane na mama. Lakini tangu nilipopata ajali namba yake haikuwa imepatikana tena.

Uzembe nilioufanya ni kuwa namba niliyokuwa naitumia haikuwa namba iliyosajiliwa kwa majina yangu. Hivyo kuirudisha kwa matumizi hata baada ya siku kuibiwa isingewezekana. Nilikuwa najilaumu Sana kwa Jambo hilo.
Msomi mzima mwenye Shahada ilikuwaje sikutambua umuhimu wa kutumia laini iliyosajiliwa kwa majina yangu mwenyewe.
Nilikuwa nawaza nikijilaumu.

Ninakaakiba ka Laki tatu, ikifika Laki tano nitaenda Morogoro chapu kumwona Mama. Atafurahi Sana. Nitambebea na zawadi ya nguo.
Bado nilikuwa nawaza.

Wakati nafikiri hayo, punde anaingia Bihawa akiwa amebeba chakula. Kama kawaida Yale alikuwa amevaa hijabu.
Jambo Moja ujue ni kuwa wakati wote huo tangu wakati wa ajali Mpaka wakati huu Bihawa alikuwa akifanya mambo hayo kwa usiri Mkubwa majirani bila kujua ingawaje baadhi ya watu walishaanza kuhisi mahusiano yetu.

Alikuwa kaleta Wali Samaki, kama kawaida lazima aje na chungwa.
Tofauti na siku zote mara hii Bihawa aliniomba Jambo;
" D samahani naomba kwenda msalani"
Sikuwa na ubishi nikamruhusu. Akaniacha sebuleni akaingia zake chumbani ambapo huko kuna Choo na bafu.
Nikawa nakula zangu lakini huko nje manyunyu yakaanza, kwani ulikuwa msimu wa Mvua.

Mpaka nakaribia kumaliza chakula Bihawa alikuwa hajatokea.
Huko Nje Mvua ilikuwa imeshachachamaa.

Mara Mlango unagongwa, Nani atakuwa anagonga Mlango usiku huu WA saa tatu kwenda Sana nne. Kikawaida Mimi sinaga wageni zaidi ya Cathy, Bihawa au mwenye nyumba.
Na mwenye desturi ya kuja usiku na Bihawa ambaye nipo naye. Cathy' hajawahi kuja usiku hata siku Moja ila akijaga anaondoka usiku mnene tofauti n Bihawa.
Mwenye nyumba yeye Hanaga hayo mazoea na haishi hapo. Majirani zangu wao hatujawahi kusumbuana usiku.

Nikafika Mlango nikauliza Nani.
Mara nasikia Sauti Cathy, " Ni Mimi mpenzi. Fungua Mvua inaninyeshea"

Moyo unapiga Paaah!
Hofu na kuchanganyikiwa kwa pamoja vilinivamia.
"Fungua D nalowa"
Hapohapo kabla sijafungua nasikia Sauti kwa nyuma ikiniambia ni Nani. Nageuka namkuta Bihawa amevaa kanga tuu kaipitisha kwenye makwapa ametoka kuoga. Amesimama katikati ya mlango unaotenganisha Sebule na chumba.
" Fungua Baby nalowa jamani"
Inanibidi nifungue. Nafungua mlango Cathy anapita upesiupesi akiwa amelowa chapachapa Akiwa kavaa nguo zake za kazini.

Inaendelea;

Nini kitatokea..?
Usikose sehemu ya Pili?

Mapenzi au Kazi?
Je Pesa Itakupa furaha?
Ni upi uchaguzi sahihi katika Mapenzi?
Uhalifu usiokusudia unapotokea nani atawajibika?

Mtunzi Robert Heriel
CEO Taikon Publishers,
CEO Taikon Cleaning Services,
+255693322300
 
MY LAST RIDE; SAFARI YANGU YA MWISHO.
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Episode 02

Ilipoishia;
• Cathy kamkuta Bihawa akiwa kwa Dimoso. Akiwa na kanga Moja usiku WA saa nne.
Nini kinajiri?

Endelea;

Cathy hakuamini alichokuwa anakiona mbele yake. Nilimwona kifua chake kikipanda na kushuka kwa nguvu Sana. Akanigeukia na kunitazama kwa macho ya hasira. Kisha anageuka kumtazama Bihawa tena. Hakujua nini afanye.

Nikatembea polepole Mpaka nilipomkaribia kisha nikamshika Mkono.
Akanitoa Mkono wangu kwa nguvu kisha akatoka" niache..!"
" No Cathy sio kama unavyofikiri" Nikasema,
" Vipi ninachokiona?" Cathy akanijibu huku akiendelea kumtazama Bihawa. Mara akanigeukia kwa upesi kisha akanipiga kikumbo " nipishe" akifika Mlangoni akafungua Mlango kisha akatoka na kutokomea kwenye mvua.
Mimi nami nikaunga mkia kumfuata nyumanyuma huku nikimuita "Cathy! Cathy! Subiri Cathy nikueeze"
Lakini Cathy hakuwa na simile, alizidi kukazana nami nikiwa nyuma yake. Alikuwa akitembea huku ameweka Mkono wake usoni Akiwa analia. Mvua kubwa ilikuwa ilikuwa ikiendelea kunyesha huku vimulimuli mara kwa mara vikimulika Hali iliyomfanya Cathy na nguo nyeupe za uuguzi alizozivaa aonekane kama malaika aliyefiwa na mtu aliyekuwa akimlinda siku zote.

"Cathy! Cathy please nisikilize" Niliita lakini haikusaidia. Cathy alipanda kwenye gari ambayo ilikuja mbele yetu na akapakia kwa hasira. Gari ikaondoka.
Kimulimuli kikimulika Nikawa namwona kwenye kioo cha dirisha la gari Akiwa ananitazama kwa uchungu mwingi. Mimi nikiwa nimesimama nikilisindikiza gari kwa macho Mpaka lilipopotea. Nilikuja kushtuka nilipohisi Mkono wangu umeshikwa.

Alikuwa ni Bihawa aliyekuwa amekuja. Akanishika Mkono
"Twende ndani Mvua inanyesha" akasema huku akinivuta. Sikuwa na namna tukarudi ndani. Nilijisikia vibaya Sana kwa kile kilichokuwa kimetokea.
Bihawa aliiona Hali Ile na nilipomtazama alikuwa na hofu.
" Samahani D sikuwa na lengo la kuharibu uhusiano wenu"
Bihawa akasema kwa sauti ya Kinyonge Sana.
Nikamtazama, niliuona Uso wake ukiwa na majuto yaliyopelekana na mashaka.

" Nisamehe! Nimejisikia vibaya D. Nilichokufanyia ni Jambo Baya kweli"
" Hapana! Usijilaumu. Najua hukukusudia"

Bihawa kama mwanamke mwerevu aliona hiyo ndio Nafasi ya kujiweka karibu na Mimi na ikiwezekana kunimaliza. Akanisogelea na kuanza kunigusa gusa kichwa changu huku akijifanya kama ananibembeleza.
Macho yangu yalikosa mhimili pale yalipoona upaja wa Bihawa ukiwa upo wazi. Kanga aliyokuwa ameivaa ilikuwa imeachia uwazi uliotosha Kabisa kuacha upaja wake kwa sehemu kubwa.
Bihawa hakuwa mnene Sana lakini Mapaja yake yalikuwa mazito ya haja. Rangi ya kahawia inayometameta ya Mapaja yake ilipoteza Kabisa Akili yangu katika ulingo WA maamuzi. Sikuwa na uwezo wa kuamua chochote pale. Moyo ulisukuma damu Mbali Sana. Bihawa naye aligundua hivyo baada ya kuona mapigo na joto langu limebadilika.

Hakutaka kunikopesha Wala kunichelewesha akanisogelea Mpaka usoni, kisha akayakaza macho yake ya gololi mbele ya macho yangu kisha akanikalia huku akinitazama kwa kurembua. Bado Akili yangu ilikuwa imepigwa knockout ikiwa chini ya ulingo muamuzi akiwa amepiga kipenga kuwa nimepoteza pambano la uwezo wa kuamua.

Bihawa akalegeza Midomo yake minene kisha nikaona katikati ya Midomo yake ukitoka ulimi wenye udenda wenye uchu hali iliyoongeza maumivu ya utamu mwilini mwangu. Kisha akanipa ule ulimi. Sikuwa na chaguo.
Tuliingia katika dimbwi la mapenzi lenye uzio wa umeme wa Mapenzi.
Bihawa uwezo wake wa kunyumbulika ulikuwa wa kiwango cha mwisho. Alikubwa bingwa na ni kama alionyesha kukamia Sana. Hata hivyo nilimsikia akisema yeye ni Mbondei kutoka Tanga.
Wakati anakatika katikati ya Mchezo akaanza kujiimbisha huku anininengulia kwa madaha;
" Miye tufaa miyee"
Miyee tufaa miyee
Jiliee tufaa jiliyee
Jiliyee tufaa jiliyee
Miyee ooh! Miyee ooh!"
Alikuwa akiimba kwa madeko na kwa kujineng'enesha kana kwamba anasikia utamu wenye maumivu hivi huku akijipeleka kimdebwedo.
Kisha anaanza kwa Kasi harakaharaka na wimbo wake ukienda kwa kufuata mapigo ya anavyokatika. Doooh! Aliniweza Sana Bihawa.

**********

Huo ulikuwa mwezi wa nne. Katika mkataba wa pikipiki. Ikiwa ni miezi tisa kuelekea Kumi tangu nifike Kiwangwa.

Wiki nzima Cathy' hakutaka kuniona. Kila nilipopiga simu aliikata.
Nilipoenda kazini kwake alinifungia vioo na kunipa onyo niache kumfutilia kwenye maisha yake.

Nilikuwa kwenye wakati Mgumu Sana. Nilitaka nionane naye angalau nimwombe Msamaha lakini Cathy hakuruhusu Jambo hilo.
Kiukweli nilimpenda Sana Cathy. Hakuna mwanamke ambaye kwenye maisha yangu aliweza kuuteka Moyo wangu Kiasi kile kama alivyoufanya Cathy.

Mwezi mzima uliisha. Nilikuja Kupata taarifa kuwa Cathy atafanya kasherehe kadogo katika siku yake ya kuzaliwa. Jioni hiyo nilienda katika Makazi ya Cathy. Mazingira yalikuwa yameandaliwa vizuri kisherehesherehe. Palikuwa pamependeza Sana. Watu kadhaa wengi wao wakiwa wafanyakazi wenzake na Cathy pamoja na majirani walikuwepo wakisikiliza Muziki.

Sehemu ya jukwaa niliona Keki kubwa iliyonaksishiwa vyema Kabisa. Nyuma ya Keki kulikuwa na kiti kilichopambwa. Mawazo yangu yaliniambia hapo ndipo angeketi Cathy.

Nikaingia na kukaa kiti cha nyuma nikisubiri sherehe kuanza huku mara kwa mara nikiangalia huku na huko kuona kama nitamwona Cathy. Nilimwona rafiki yake CGhy akinijia alikuwa akiitwa Isabelle. Ni muuguzi Mwenzake. Alinifikia kisha akainama Mpaka kwenye sikio langu na kuniambia niondoke kwani Cathy hataki kuniona na hataki kuharibu sherehe yake.

Akaninyanyua kisha akanikokota Mpaka nyuma Kabisa ambapo hatuuoni ukumbi wa sherehe na hakuna Watu.

Isabella akaendelea kusema;
"Sikia Kijana, usijitafutie matatizo. Nakushauri ni Bora uondoke tuu. Usije ukajiingiza kwenye matatizo. Cathy sio level yako. Alafu mbaya zaidi umemuumiza na kuichezea Nafasi"
Nikataka kuongea akaniziba mdomo;
" Haina haja D. Kila kitu kwako kimekwisha. Cathy hakutaki tena. Unajua viongozi wangapi wanamfukuzia Cathy. Unawajua? Please D nakuomba kama kijana mwenzangu. Rudi nyumbani"

" Alafu wewe ni Kijana mzuri. Wanawake wapo wengi. Utapata mwingine. Haya shika hii uondoke!"

Akatoa kibunda cha Laki Moja akanipa mkononi. Nilijikuta machozi yakinilenga lenga kama mtoto.
" Siondoki! Siondoki! Unafikiri naogopa." Wakati naongea punde nikasikia Sauti kutoka kwenye kipaza Sauti ikiwakaribisha wageni waalikwa kisha ikasema shughuli inaenda kuanza na Cathy mwenye shughuli anatarajiwa kuingia ukumbini. Kisha Sauti Ile ikaacha na Muziki mwororo ukaanza kupiga.

" Shika pesa yako. Kampe Bwanaako"
Nikasema nikimtupia kile kibunda kisha nikatoka Moja Kwa Moja nikaelekea ukumbini.
Nyuma yangu rafikiake Cathy alikuwa akinifuata mbiombio lakini tulipotokea ukumbini akapunguza mwendo.
Viatu vyake virefu na kigauni chake kifupi vilimkatili na kumfanya ashindwe kunifikia kwa haraka.

Niliamua kwenda viti vya mbele Kabisa ili Cathy akija asipate shida kuniona. Nikamwona rafiki yake Cathy akipita mbele yangu huku akiniangalia kwa macho ya chuki kisha akabetua midomo yake na kuongeza mwendo Akiwa anautingisha mwili wake kama sehemu ya kuonyesha kiburi na dharau zake. Akapotelea kwenye Mlango uliokuwa na Maputo unaoingia katika Sebule ya nyumba ya Cathy.

"Dimoso usijefanya Jambo la kipuuzi. Tulia! Utazidi kujiaharibia" Nilifikiri.

"Lady and Gentlemen, kwa shangwe na furaha tusimame kwaajili ya malkia wetu Cathy ndio anaingia ukumbini. Makofi na vigelegele"
Ukumbi mzima unapiga makofi na vigelegele lakini Mimi sikuweza kufanya hivyo macho yangu yalikuwa yanatazama upande ambao Cathy angetokea.

Mara watu wote wakasimama na Mimi pia baada ya kumwona Cathy akitokea katika lango lililopambwa vizuri kwa Maputo na taa za kupendeza.

Cathy alikuwa amependeza Sana. Gauni refu la rangi ya zambarau mpauko lililoshika umbo lake vilivyo, lilimfanya aonekane kama Miss dunia. Viatu vyake virefu Kiasi viliongeza sehemu ya uzuri wake. Nywele zake ndefu zilizokuwa zinaning'inia mgongoni ungesema ni malaika.
Kwa madoido na madaha alikuwa akicheza huku akifuata mdundo wa Muziki uliokuwa unaendelea.
Sisi wote tulikuwa tumesimama nasi tukimuunga Mkono kwa kucheza polepole ingawaje wote ni kama tulikuwa tukistaajabu uzuri wake.

Tayari alikuwa amefika mahali alipokuwa ameandaliwa kwenye kile kiti chake. Nyuma yake na mbele zake walikuwepo marafiki zake watatu hivi wakimsapoti wakicheza naye huku wakiwa wamebeba chupa za Shampein huku wakizitikisa.

Kisha Dj akabadili wimbo ambao nafikiri ilikuwa imepangwa hivyo, ule wimbo ulivyoanza kupiga rafiki zake waliokuwa pale mbele wakaupokea wakiuimba kwa shangwe ya ajabu Sana kama wadada wamjini wenye uzoefu na matukio ya sherehe kama Ile, alafu wakafungua Mifuniko za zile chupa za Shampein shaaaap! Vuuuuuup! Povu jingi liliruka hewani kutoka kwa zile chupa.
Wale rafiki zake Cathy walikuwa mabingwa wa kuzizungusha zile chupa Jambo ambalo lilepovu lilikuwa likiruka hewani huku likichora Maumboumbo Fulani ambapo Kati ya maumbo hayo niliweza kuona umbo la kopa ambalo lilibeba tafsiri ya Upendo.

Umbo Hilo la kopa lilitutenganisha Mimi na Cathy. Yeye alikuwa upande mwingine na Mimi upande mwingine katikati likiwepo umbo la kopa la lile povu lililoundwa na rafiki za Cathy. Kwa sekunde mbili macho yangu na macho ya Cathy yaligongana ndani ya lile umbo la kopa.
Nikamuona Cathy akifumba macho yake polepole kwa madaha huku lile povu la kopa la lile povu la Shampein likiparangangika polepole kama Mchezo Fulani hivi wa kupangwa..

Moyo wangu ulikuwa unapiga. Sikujua kwa nini nilisisimkwa. Hofu haikuwa hofu. Furaha sio furaha. Nashindwa kueleza hali iliyokuwa imenipata.

Tukaambiwa tukae lakini mara kwa mara Cathy alikuwa akinitazama kama Mtu mwenye Mpango wa hasira dhidi yangu.

Cathy alipewa nafasi ya kuzungumza na hapo akasimama, Ile furaha aliyoingia nayo ilikuwa imeyeyuka. Tangu aliponiona pale mbele hakuwa na utulivu. Nililigundua Jambo hilo. Hivyo nikaona isiwe Kesi nikasimama wakati Cathy akiongea. Kisha nikamfuata na kumkumbatia Jambo ambalo watu wengi walibaki wanashangaa hata hivyo Wachache walipiga vigelegele. Nikatoa zawadi yangu niliyokuwa nimemwandalia. Lilikuwa Ua lenye kikaratasi juu Chenye maandishi yanayosomeka, I'm Sorry.
Kisha nikatoka zangu na Moja Kwa Moja nikaelekea kwenye lango la kutokea nikaondoka zangu.

************

Kazi ya bodaboda ni Kazi nzuri lakini pia ni Kazi ngumu. Kuna siku nilikuwa napata pesa nyingi Sana lakini kuna siku nilikuwa nakosa hata Ile elfu kumi ya mkataba ya kumpa Mzee Abeid.
Hivyo ilinipasa zile siku ambazo napata pesa nyingi niweke akiba ambayo itanisaidia siku ambayo hakutakuwa na wateja.

Kilikuwa ni Kipindi cha Mvua hivyo biashara ilikuwa ngumu Sana. Tayari nimefikisha miezi nane na imebaki miezi minne tuu. Mvua ilifululiza wiki nzima. Mchana manyunyu mwanzo mwisho usiku Mvua kubwa.

Nilishatoa akiba yangu yote. Asubuhi ya Leo sikuwa na pesa yoyote. Nje Mvua inanyesha na matope kama yote.
Cathy alishaendelea na maisha yake na Mimi nilishakubali kuwa penzi letu lilikuwa limefikia mwisho.

Niliamua kuendelea na maisha yangu nikiwa na Bihawa.
Bihawa alikuwa ni Single Mother wa mtoto Mmoja aitwaye Kuluthum. Mwanamke mwenye umri upatao Miaka thelasini hivi Akiwa amenizidi Miaka minne hivi. Kwa rangi alikuwa Maji ya kunde mwenye mwili WA wastani lakini mwenye Mapaja mazito na manene. Lakini hayo usingeyaona kutokana na nguo alizokuwa anapenda kuzivaa ambazo zilificha maungo yake.
Kazi yake ilikuwa Mama Ntilie, ambapo alikuwa akipiga katika mgahawa uliokuwa maeneo ya Stendi ya Kiwangwa. Moja ya mgahawa ambao watu wengi wa pale Kiwangwa hasa vijana walikuwa wakiupenda kutokana na mapishi yake ya kitanga.

Asubuhi hiyo niliamua niende kwenye Mgahawa wa Bihawa licha ya kuwa na Mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha.
Nilichukua jacket langu la Mvua na mabuti ya Mvua. Nikatoa pikipiki na Moja Kwa Moja safari ikaanza.

Juu ya mgahawa wake kulikuwa na bango lililosomeka Mapishi ya Tanga. Hii ilikuwa mara yangu ya Kwanza kuingia katika mgahawa wake. Nilipofika mabinti wawili ambao ni wasaidizi wa Bihawa walinipokea kwa ukarimu wa ajabu. Ukarimu ule nisingejidanganya ulikuwa wa burebure. Nilijua wale mabinti watakuwa na taarifa ya uhusiano wangu na Boss wao ambaye ni Bihawa.

Bihawa hakuwepo sijui alikuwa ameenda wapi. Nikiwa ndani ya ule mgahawa ambapo ndani yake kulikuwa na meza za plastic na vitu vyake. Ulikuwa mgahawa mdogo ambao ungetosha watu kumi na mbili kwa pamoja.
Juu nilisoma kibao kilichoandikwa " lipa pesa Kwanza ndipo uagize"
Mfukoni Sina pesa na Bihawa hayupo.

Pembeni yangu niliwakuta wanaume wawili waliokuwa wakinywa supu na chapati. Wao waliendelea na stori Zao ambazo nilizipuuza kwa Sababu sikuziona kama zinamaana.

Punde nikasikia Sauti ya Bihawa yenye lafudhi ya kitanga ikigomba. Bihawa alikuwa akiwafokea wale mabinti kwa nini hawajanihudumia. Nikawaona wale mabinti wakiparangana upesiupesi wakichukua bakuli la supu.

Kisha Bihawa akaja pale nilipokuwa nimekaa Uso wake ukiwa unafuraha Mimi kuwa pale.
" D ni wewe!" Akasema huku akiniangalia kwa macho yake malegevu. Kisha akavuta kiti akakaa karibu yangu.
" Siamini! Leo nitaandika kwenye dayari. Siku zote nakubembeleza uje unakataa"
Hapo akanyamaza alikuwa amesikia Sauti ya Binti Mmoja ikiuliza alete chapati ngapi.
" Lete Tatu" Bihawa akajibu.
Nikataka kumkatisha nimwambie mbili zingenitosha lakini akanizuia.

Supu na chapati zikaletwa. Kama kawaida Yake Bihawa lazima kwenye mlo atakaonipa lazima angeniwekea na chungwa. Akawaambia wale mabinti walete na chungwa Moja. Nikataka kumzuia lakini akanisi nisimzuie.

Ilikuwa supu tamu Sana. Bihawa kweli alistahili kuteka wateja wa pale Kiwangwa. Chakula chake kilikuwa kitamu Sana.

Baada ya kupiga Stori za hapa na pale. Bihasa akaniaga
" D Mpenzi ngoja nisikusumbue mwaya. Kula umalize Mimi niendelee na vijikazi. Si eti mpenzi"
Nikamwambia Sawa haina shida.

Nikaendelea Kula huku wale wanaume wawili wakiendelea kupiga Stori Zao.
Lakini ghafla nilijikuta nikivutiwa na zile Stori Zao baada ya kusikia Jambo lisilo la kawaida.
" Hii biashara tukifanikiwa tutakuwa tumekula bingo. Fikiria Milioni kumi na tano yote itakuwa yako"
Mwanaume wa Makamo aliyevalia jacket jeusi la Mvua na kofia kichwani alikuwa akizungumza huku akimuangalia mwanaume mwingine ambaye hakuwa mtu mzima Sana.
" Ila wewe unachukua nyingi Mzee wangu. Karibu robotatu yote unachukua wewe. Yaani kwenye Milioni hamsini Mimi napata kumi na tano tuu wakati zoezi zima Mimi ndio na ratibu"

" Usiwe na tamaa ndugu yangu. Milioni kumi na tano ni nyingi Sana. Mimi ndiye mwenye mchongo. Wewe mwenyewe ulinipigia simu huna Kazi. Kwa bahati ulikuja wakati muafaka nami ndio nilikuwa nimepewa Kazi hii"

" Hata kama Mzee. Kazi hii ni ngumu na Hatari. Unalijua Jambo hili. Hapa Dili likibumba naenda kufia Jela na wewe najua utaniruka Maili Mia..."
" Basi Tulia! Kula ishirini Basi"
"Hayo ndio Maneno"
Muda wote nilikuwa nakunywa supu huku masikio yangu yakisikiliza mazungumzo ya Mamilioni ya pesa. Hali yangu ya uchumi ilikuwa mbaya Sana. Fikiria Mpaka nakuja kugongea kwa Mama Ntilie wawatu, Bihawa. Sijui siku ya Leo nitapata wapi elfu kumi ya Mzee Abeid. Kodi nimeshalipa lakini pesa ya Mzee Abeid ilikuwa inaninyima usingizi. Ukizingatia nimebakiza miezi minne kasoro hivi kumiliki chombo.

Wakaendelea
" Leo ndio siku nakutana na dealer atakayenipa huo Mzigo"
" Lakini mazingira si unauhakika nayo yapo Salama"
" Mazingira yapo Salama. Tulichagua PF55 Kule Dili litafanyika vizuri Kabisa"
Yule Kijana alisema, nikagundua kuwa Yule Kijana ni mwenyeji wa pale Kiwangwa au ni mtu ambaye yupo Pale Kiwangwa kwa Muda mrefu. Wakati Yule mwanaume wa Makamo Akiwa ni mgeni wake.

" Vizuri! Kama utafanikisha Dili hili basi ninaweza kukuamini kwa ishu zingine. Tutafanya Kazi"
" Amini kwamba hili limeshafanyika. Lakini Mzigo wa kumpa Yule dealer wetu si umekuja nao? Maana amesema hataki ujanjaujanja"

" Ndio nimekuja nao. Upo lodge"
" Sawasawa! Hizi Mvua zinatuweka katika mazingira mazuri ya kufanikisha huu mchongo. Kufikia saa tatu mji wote wa Kiwangwa utakuwa umepoa. Hakutakuwa na movements za watu. Hivyo nishamwambia dealer wetu Sana tano na nusu usiku ndio ishu itakuwa imekamilika.

Wakati wanaongea Bihawa alisimama mbele Yao akachukua vyombo kwani walikuwa wamemaliza. Wakashukuru na kusimama kisha wakatoka.
Nikajikuta natamani kujua mchongo wao unahusiana na nini. Hela walizozitaja ni pesa nyingi kwangu. Tamaa ya Kutaka kuingia kwenye hilo dili ikanivaa kwa nguvu.

Bihawa akaja tena.
" Vipi nikuongeze?"
" Aah! Hapana nashukuru nimeshiba"
" Kweli!"
" Ndio! Labda uniambie unanidai shilingi ngapi?" Nilisema hivyo huku Moyo wangu ukiwa unaomba anipe ofa. Huku nikiapa nafsini nitamlipa kila kitu Bihawa kwa Wema anaonifanyia.
" Wewe tena siwezi kumdai Mume wangu Kipenzi. Deni Lako ni Leo usiku. Ndio maana nimekupa chapati tatu na nyama nyingi. Nataka Leo unifunge tatu bila na bilabila kama Juma nature "
"Hahah! Wanaume family au wanaume Halisi "
Nikamuuliza.
" Nitajua Leo usiku. Na hiki kumvua natamani kukuche"
********

Jioni ilifika. Mpango wangu siku hiyo ulikuwa ni ikifika saa nne na nusu niende eneo la PF55 kutaka kujua biashara iliyokuwa inafanywa na wale wanaume wawili.
Siku hiyo nilipata elfu Saba tuu. Ningelala njaa Hilo kwangu halikuwa tatizo. Ila shida ilikuwa ni Mzee Abeid. Bado elfu tatu ifike elfu kumi ya Mzee Abeid. Hicho ndicho kilichokuwa kinaniwazisha. Kila siku nilikuwa nikimpelekea Mzee Abeid elfu kumi ifikapo saa mbili usiku.
Na ilikuwa imebaki saa moja ifike saa mbili usiku.

Nikaamua nimpigie Bihawa anikopeshe elfu tatu. Akaniambia nimsubiri atakuja nayo lakini nikakumbuka Muda WA Bihawa kuja pale ghetto ni Sana NNE usiku. Nikamwambia Nina haraka nayo Sana. Ndipo akaniambia nikaichukue. Nikaenda na pikipiki chapu nikamkuta bado anahudumia wateja. Akanipa elfu tatu. Nikaenda kumpelekea Mzee Abeid Elfu kumi yake.

Saa nne ilipofika nikawasha pikipiki yangu kuelekea PF55 ambapo ni mwendo wa nusu saa kwa pikipiki.
Nilikuwa nimevaa jacket jeusi la Mvua na buti za Mvua. Lile jacket la Mvua lilikuwa na kofia lake.

Ndani ya nusu saa nilikuwa katikati ya shamba la nanasi kubwa lenye hekta za kutosha linalomilkiwa na kampuni ya PF55 ambapo kirefu chake ni Pineapple Farm 55.
PF55 ilikuwa kampuni kubwa inayomiliki mashamba makubwa ya nanasi ambapo pia hutengeneza juisi ya nanasi na mengine husafirisha Nje ya Nchi.

Kutokana na nanasi kutokuwa na urefu hii inasababisha mtu akiwa Mbali uweze kumwona kama hakutakuwa na vichaka au Moto mingine mirefu.

Bado Mvua ilikuwa inanyesha, saa yangu ilinijulisha ni saa nne na nusu. Sasa nilikuwa natafuta sehemu yenye angalau kichaka kirefu ambacho ningejificha Mimi na pikipiki yangu.

Katika angaliaangalia nikaona kichaka kwa Mbali pembeni ya barabara. Nikaendesha pikipiki Mpaka kwenye kile kichaka. Kisha nikaificha pikipiki yangu humo. Alafu Mimi nikawa nimesimama pembeni ya barabara.

Magari machache yalikuwa yakienda na Mengine yakirudi. Huku eneo lile likiwa Kimya Sana kama gari lisingekuwa linapita. Mara Mojamoja Sauti za chura zilikuwa zikisikika lakini Kwa machalemachale.

Mara simu ikaita, kuangalia alikuwa ni Bihawa. Nilimuelekeza funguo zilipo nikamwambia nimepata Mteja wa Msata hivyo anivumilie nitarudi. Baada ya simu kukatika.

Nikaweka simu mfukoni. Kisha Nikawa nimechoka kusimama ikanibidi nikae pembeni ya barabara kwenye lami. Mawazo Mengi yakawa yananipitia. Nilimkumbuka Mama yangu Kijijini. Ile Laki tatu niliyokuwa nataka niongezee kidogo iwe Laki tano iliishia kwenye kulipa Kodi. Na pale nilipo sikuwa ma pesa yoyote ya akiba.
Nilijikuta natoa machozi ambayo yalibebwa na matone ya manyunyu yaliyokusa yakiendelea kunyesha.

Saa yangu ilinijulisha ni saa tano na dakiki ishirini na tano. Na sikuona dalili yoyote ya ujio wa wale wanaume.
" Sikuwasikia vizuri labda. Au ni upande ule mwingine. Lakini wasingeweza kufika upande ule bila kupita hapa. Njia ni hiihii! Vipi lakini kama moja ya Magari yaliyopita ni yakwao. Kwanza hujui gari Yao"
Nilikuwa nawaza mwenyewe huku saa Muda huo ikionyesha ni saa tano na dakiki ishirini na nane.

Punde kwa Mbali nikaona Mwanga wa taa ya gari ikija kutokea upande wa Kiwangwa Mjini. Moyo ukapiga paah! Huenda ndio wenyewe. Nikawaza. Ikanibidi niingie ndani ya shamba la nanasi Hatua kadhaa, nikalala kujificha. Lile gari likafika pale nilipokuwa likiwa na mwendo mdogo. Polepole. Kisha likaenda umbali wa Mita hamsini hivi. Alafu likasimama.

Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakipiga Sana. Sijui kwa nini nilikuwa nahisi hofu. Macho yangu yalikuwa Makini kuangalia kwenye lile gari. Zilipita sekunde kadhaa gari Ile ikiwa imesimama palepale pasipo Mlango wake kufunguliwa.
Mawazo yangu yakatafsiri Jambo hilo kwamba huenda biashara ndio inafanyika mule ndani. Nikataka kuinuka ili niisogelee Ile gari lakini ghafla Mlango wa nyuma wa Ile gari ukafunguka. Nikainama haraka chini kma mwanzo kujificha huku kichomi cha Hofu kikipita kwenye mbavu zangu.
Punde nikamwona mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa Miaka mitano hivi akashuka. Kisha mlango WA mbele usio WA dereva nao ukafunguka. Kisha akashuka mwanamke Mmoja hivi. Nikawa kama sipumui nikiwa Makini kutazama kilichokuwa kinaendelea.

Yule Binti mdogo akainama, akajisaidia haja ndogo. Kisha Mamaake akampa toilet paper akajifuta. Wakati hayo yanaendelea ghafla nikashtushwa na Mwanga mwingine Mkali kutokea upande wa Kiwangwa Mjini. Nikageuka kuutazama. Ilikuwa gari yenye Mwanga Mkali ambao ulifanya nionekane kidogo.
Ikabidi nijifiche zaidi Ile gari ikiwa bado iko mbali.
Nikakumbuka habari za Ile gari iliyosimama, nikageuka kuangalia nilishtuka kuona imeshaondoka.

Mapigo bado yalikuwa yananipiga haswa. Ile gari yenye Mwanga Mkali iliyokuwa inakuja kutokea Kiwangwa Mjini ikapunguza Mwanga ukawa wakawaida kisha ikawa inakuja kwa mwendo wa polepole kama Ile gari ya Kwanza iliyosimama akashuka Binti mdogo akajisaidia na mwanamke Mmoja hivi.

Nikiwa bado naitazama, ghafla nikashtuka kusikia Sauti ya mtoto anayelia " ng'aa! Ng'aa! Ng'aa!" Nikageuka kwa upesi. Natazama nikamwona mwanamke Mmoja aliyeutanda Uso wake na kilemba, Akiwa amesimama pembeni ya barabara palepale Ile gari ya Kwanza iliposimama.

Ile gari iliyokuwa inakuja tayari ilikuwa usawa wangu ikiwa inapita na mwendo wa polepole huku ikimulika Mwanga wa kawaida ambao ulikuwa unamfikia Yule mwanamke aliyebeba mtoto aliyekuwa analia.

Yule mwanamke alikuwa amevaa Kaunda suti ya kijani, kilemba cheusi alichojifunga Uso wake usionekane vizuri.
Nikakumbuka kutoa simu haraka kisha nikaanza kurekodi lile tukio.

Lile gari likasimama pembeni ya barabara kisha sekunde kadhaa zikapita akashuka mwanaume Mmoja ambaye nilimtambua ndiye Yule Mwanaume wa Makamo aliyekuwa kwenye Mgahawa wa Bihawa. Mikononi make alikuwa amebeba begi la kuwekea pesa. Kisha akamsalimu Yule mwanamke, hayo yote nilikuwa nayaona kupitia simu niliyokuwa narekodia. Kisha Yule mwanamke akamkabidhi Yule mtoto mchanga aliyekuwa analia, akampa Yule mwanaume.
Kabla Yule mwanaume haja kabidhi lile begi kwa Yule mwanamke ghafla simu yangu ikaanza kuitaa. Jambo ambalo liliwafanya wasikie na kugeuka upande niliokuwepo kutazama.

Itaendelea!

Nini kitatokea?
Usikose sehemu ya tatu!
 
MY LAST RIDE; SAFARI YANGU YA MWISHO.
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Episode 01.

Sikumaanisha kuua! Wala sikuwahi kuwaza kuwa kuna siku nitakuja kuua mtu. Kwa kweli ningefanya dhambi zote, zote! Lakini sio dhambi ya kumwaga damu ya Mtu. Haya sasa nini kimetokea? Nani kaniloga! Mungu wangu!

Nimeua! Nimeua! Dimoso Mimi Nimeua!
*********

Jina langu naitwa Dimoso. Wengi huniita D, ukifika hapa kiwangwa hutonipata kama utaulizia Dimoso, ingawaje ni jina langu lakini wengi hawalifahamu. D ndio jina Maarufu zaidi. Hilo Mpaka mtoto mdogo ungemuuliza angekuleta mahali ninapoishi kama angenikosa kijiweni mahali ninapofanyia Kazi ya bodaboda, yaani udereva pikipiki.

Ni Miaka miwili sasa tangu niingie katika Kazi ya ubodaboda. Baada ya kumaliza Masomo yangu ya elimu ya juu katika Masuala ya tehama kwenye IT "Shahada ya information Technology" katika Chuo cha DIT. Nilikula msoto haswa nikiwa napambana huku na huku Kutafuta Kazi katika fani niliyosomea.
Lakini jitihada zangu ziligonga mrama na mipango kwenda kombo baada ya tumaini la Kupata Kazi kuyeyuka Kabisa.

Nilihisi kukata tamaa. Nuru ya mafanikio ilimezwa na wingu jeusi la kushindwa. Sasa nikaanza kulia na kujilaumu. Machozi yangu yangemwagika chini kwenye Udongo huenda miche iliyopo udongoni ingeweza kustawi. Yalikuwa machozi Mengi Sana. Lakini haikuwa hivyo. Upepo WA mashaka uliyapeperusha machozi yangu na kuyakausha bila kuacha alama. Ni kwamba hakuna aliyeyaona machozi yangu. Wala hakuna aliyejua kuwa ninalia. Hakuna aliyekaribu Wala aliyejali hali niliyokuwa naipitia.

Kilikuwa Kipindi kigumu Sana kwangu.

Maisha ya Dar es salaam yakanishinda sikujua kama nikiondoka Dar niende wapi. Kurudi nyumbani Morogoro isingewezekana. Ningerudi vipi nikiwa katika Hali kama Ile. Hali ya kushindwa, kuchoka na kukata tamaa. Wazazi wangu wangenitazamaje Mimi? Wangejisikiaje! Mimi kwao nilikuwa kama Jemadari wa vita waliyemuamini Sana. Shujaa wa ukombozi wao. Ati Leo nirudi kichwa chini Mikono nyuma. Hapana! Hiyo nilikataa.

Nayakumbuka Maneno yangu ya kishujaa niliyowaahidi yakuwa ninaenda Chuo kikuu Dar, nikimaliza nitawapa maisha Mazuri. Nitawabadilishia hali ngumu ya umaskini waliyonayo.

Nakumbuka siku Ile Mama yangu akiwa ananisindikiza kituo cha Magari, naikumbuka siku Ile vyema. Nikamwambia Mama; Wakati umefika Mama kuyala matunda yako. Kitambo kidogo unafurahia Kazi uliyoifanya Kwa Miaka mingi. Ulinisomesha ili uishi Maisha mazuri. Nakuahidi Mama. Jambo hilo halipo Mbali tangu Leo"

Siku Ile Mama yangu alikuwa anatabasamu Muda wote. Uso wake uliozingirwa pande zote na mikunjo ya lishe Duni ilipingana vilivyo na tabasamu lake. Niliona nuru ya tumaini ikichomoza katika macho yake. Akanikumbatia kisha akanong'ona nyuma ya mgongo wangu Akiwa amenikumbatia. Baba yako atajivunia sana. Natamani angekuwepo.

Hayo yote nayakumbuka.
Chaguo pekee nililokuwa nalo wakati huo lilikuwa kwenda Kiwangwa, huko Bagamoyo ambapo rafiki yangu wa Chuo aliniitia Kazi ya ujenzi, niende kama Saidia Fundi. Nikaenda. Huko ndiko maisha nilipoyaanzia.
*"

Ulikuwa Ujenzi wa kiwanda cha Nondo na bati. Ilikuwa Kazi ngumu Sana lakini sikuwa na budi kuifanya ili kunusuru maisha yangu. Tayari Mimi ni mwanaume. Unafikiri nani mwingine angeweza kunisaidia kama nisipojikaza na kujisaidia mwenyewe.
Wakati wote nilikuwa nikiishi kwa rafiki yangu. Nilikaa kwake karibu mwezi na nusu Mpaka pale Ujenzi wa kile kiwanda uliposimamishwa kwa Amri ya serikali.

Pesa niliyokusanya ilinisaidia kununua mahitaji yangu ya kuanzia maisha kama kitanda na godoro pamoja na vitu vingine vidogovidogo. Nilimuaga rafiki yangu. Kwa sababu alinifanyia uungwana Sana. Nilimshukuru kwa ukarimu na Msaada alionipatia kwa Kipindi chote nilichokuwa kwake. Ingawaje kilikuwa chumba kimoja na sebule lakini kwangu ilikuwa kama nyumba kubwa iliyonipa utulivu.

Sasa nikaanza Maisha ya kujitegemea, nikiwa nimechukua chumba na sebule mtaa wa tatu kama sio WA nne kutoka alipokuwa amepanga Rafiki yangu.

Nilitegemea mgogoro uliopo baina ya wamiliki WA kiwanda na serikali ungeisha mapema lakini miezi miwili iliisha mambo yakiwa hayaeleweki. Pesa ya akiba ilikuwa imeisha, Kodi nyingine ilikuwa IPO karibu.
Kichwa kilianza Kupata Moto. Nifanye Kazi gani hapa Kiwangwa. Bahati mbaya au nzuri niseme rafiki yangu yeye alibahatika Kupata Kazi serikalini mwezi Mmoja uliofuata baada ya kiwanda kufungwa. Hivyo yeye aliondoka na kwenda Wilayani Kiteto, huko Manyara. Yeye ndiye alikuwa mwenyeji wangu pale Kiwangwa. Hata hivyo tayari nilikuwa nimeshaanza kupazoea na kuzoeleka na wenyeji wa Kiwanga.

******"****
Sikubaliani na wanafalsafa wanaosema maisha ni uchaguzi wa Mtu binafsi. Nakataa. Kwa sababu kama maisha yangekuwa ni uchaguzi wa Mtu binafsi Mimi Wala nisingechagua maisha haya niliyokuwa nayo. Maisha ya kukimbizana na matatizo baada ya matatizo. Maisha ya Kulala njaa. Maisha ya kusimangwa na wenye nyumba.
Ingekuwa ni Maisha yangu ni uchaguzi wangu binafsi ningeenda kufunga chemchem ya matatizo na mikosi iliyokuwa inayaandama maisha yangu.

Mbele yangu alikuwepo Mzee wa Makamo, mwenye sura ya mzaha lakini ndevu zake alivyoziweka zilikinzana na sura yake. Aliziweka ndevu kama Mtu mtata hivi. Sijui kama unamjua Adolf Hitler jinsi alivyokuwa anaziweka ndevu zake. Kama unamjua basi ndivyo huyu Mzee wa Makamo alivyoziweka. Lakini tofauti yake na Hitler ni kuwa Mzee huyu alikuwa na sura ya mzaha.

tuliingia katika mkataba wa pikipiki. Kwamba Mimi nitachukua pikipiki na kuitumia kwa miezi kumi na mbili kisha itakuwa yangu. Lakini itanipasa kila siku nimpelekee Mzee huyu shilingi elfu kumi za kitanzania. Bila kurusha hata siku Moja.
Ikitokea nimerusha siku Moja basi mkataba nimeuvunja mwenyewe na pikipiki ataninyang'anya.
Kuhusu matengenezo ya pikipiki vyote nitafanya Mwenyewe.

Sikuwa na namna zaidi ya kukubali ingawaje masharti yalikuwa magumu. Muda ule nilichokuwa nawaza ni namna ya kuweza kuishi kwa Muda ule. Kupata chakula na Kupata pesa ya Kodi ya mahali ninapoishi ambapo ilikuwa imebaki mwezi Mmoja tuu.

Nikachukua bike nikarudi nayo nyumbani. Nikajiweka zangu kitandani, kisha nikashusha pumzi nzito unhuu! Nikajilaza kitandani, Mawazo yakaanza kunipitia. Daah! Leo nimekuwa bodaboda! Sijui nitaifanya Kazi hii kwa Muda gani. Lakini Sina namna. Muhimu nifanye nimiliki hiki chombo. Yatakuwa mafanikio makubwa Sana.
Punde simu ikaita. Alikuwa ni Mama. Nikapokea;
" Hello Mama! Shikamoo"
" Marhaba mwanangu. Unaendeleaje huko"
" Nashukuru Mungu Mama" Nikasema nikiwa nimeiweka Sauti yangu kwa namna nzuri kuonyesha Sina tatizo.
" Naomba unitumie hata elfu mbili nikanunue unga nipike. Mboga nilichuma Shambani. Sina hata pesa mwanangu"
Mama aliongea kwa sauti ya unyonge Jambo ambalo liliamsha hisia zangu za ndani.
" Usijali Mama, nakutumia, pole Sana mama kila kitu kitakaa sawa"
Nikasema kisha simu ikakatika, nahisi salio la mama lilikuwa limeisha.
Sikuwa hata na Akiba ya Mia Mbovu.
Kama ni kupekua kwenye mifuko ya suruali Kazi hiyo niliifanya Jana. Hakuna pembe Wala Kona ambayo sikuipekua siku ya Jana nikiwa natafuta hata Mia mbili ili niweze Kupata pesa ya mandazi.

"Niende kwa nani nikamkope?" Nikawa najiuliza huku nikiwa nakuna kichwa. Nilikuwa nimetingwa haswa. Mama yangu alale njaa na Mimi nipo. Hapana.

Nikatoka, nikaenda kwenye Duka ambalo lilikuwa mtaa wa pili tuu. Nilijaribu kumkopa muuza Duka lakini alinikatalia akaniambia anachoweza kunisaidia ni kunikopesha bidhaa zake kama unga au mafuta. Sasa hata kama akinikopesha unga au mafuta nitayatumaje Morogoro kwa Mama.
Nikaondoka zangu, lakini nikasema si bora ningechukua nikayatumie mwenyewe. Nikarudi tena lakini mara hii muuza Duka alikataa kabisa hata kunipa bidhaa hizo.

Nilikasirika Sana. Njiani nilitembea kama Kipofu. Nilikuwa na msongo wa mawazo.
Katika Hali isiyo ya kawaida nikajikuga nimeanguka chini na gari likiwa limenigonga. Nikapoteza fahamu. Sikujua nini kiliendelea.
********

Nimekuja Kupata fahamu ni masaa mawili baadaye. Nikiwa katika kituo cha afya cha Kiwangwa. Napiga kelele. Mama! Mama! Jamani mama yangu!
Anaingia mwanamke aliyevalia nguo nyeupe, baadaye nilijua NI muuguzi.

"Vipi unaendeleaje Dimoso" Yule muuguzi akanisalimu akiwa ameikumjua sura yake kwa tabasamu lenye kuweza kutibu.
" Nataka kuongea na Mama. Tafadhali naomba simu yangu"
" Dimoso, hukuletwa hapa na simu. Waliokuleta hapa Mmoja wapo alisema anaitwa Bihawa, mwanamke ambaye ni Jirani yako akasema unaitwa Dimoso"
" Okay! Anyway naomba simu yako nimpigie Mama. Tafadhali"
" Usijali Dimoso, nitakupa. Nataka Kwanza nikupe matibabu kisha mengine yataendelea "
" Hapana! Mimi naendelea vizuri! Nipe simu niongee na Mama yangu tafadhali"
Hapo nilikuwa nimeamka kitandani, niliongea Sauti ya ukali Sana huku nikiwa nimetoa macho. Nikatoka kuamka lakini mkononi nilikuwa na Dripu. Iliyonitonesha mahali nilipokuwa nimechomwa.
Mtonesho huo uliita maumivu katika Maeneo mengine ya mwili wangu. Nikaanza kuhisi maumivu kwenye Paja la kulia, nyuma ya mgongo na kwenye bega.
Nikagugumia, aaaahh!
" Tulia Dimoso bado hauendelei vizuri. Lala! Haya jiegemeze hapo kwenye MTO"
Muuguzi akasema Sauti yake ikiwa Mbali na upole.
Nikajiegemeza kwenye ule mto wa kile kitanda. Yule muuguzi akaja karibu akanipa simu. Nikaipokea. Nikabonyeza bonyeza namba, kisha nikaweka sikioni. Ikaita lakini haikuwa inapatikana. Nikajaribu tena ikawa haipatikani.
"Shiit" nikasema huku Uso wangu ukionyesha kukata tamaa.
" Vipi haipatikani" muuguzi akaniuliza huku anitazama kwa macho ya kupima hisia zangu. Nikamtazama bila kusema kitu.

"Itakuwa simu yake imezima chaji. Maskini huenda alisubiri mpaka akachoka" nikasema kwa sauti ndogo. Muuguzi akiwa ananitazama. Kisha akachukua kipima mapigo ya moyo na kipima presha cha kisasa akanipima. Kabla hajamaliza Mlango ukafunguliwa Mimi ndiye niliyegeuka muuguzi hakugeuka alikuwa akiendelea kunipima. Alikuwa ni Bihawa ambaye ni mwanamke Jirani yangu.

Bihawa alikuwa amebeba hotpot pamoja chupa la Maji na machungwa. Akawa amesimama huku akinitazama kwa macho ya huruma. Baada ya muuguzi kumaliza kunipima akaniambia ninaendelea vizuri.
Kisha akaenda kwenye meza iliyokuwa mule kwenye Ile wodi akachukua kifuko ambacho bila Shaka alikuwa amekuja nacho. Akatoa Dawa kadhaa kisha akawa ananipa maelekezo;
" Hii ni antibiotics, utakunywa mbili mara tatu. Kila baada ya saa nane.
Hii ni antipain, Dawa ya kutuliza maumivu. Utakunywa nayo hivyohivyo. Kila ukinywa hii antibiotics unameza na hii. Usipishanishe Muda. Sawa.
Nimesahau, wewe ulisema ni mkewe au ?"
Muuguzi akamgeukia Bihawa, mwanamke aliyevalia baibui ambaye harakaharaka utagundua ni mtu mwenye kuipenda Dini yake.
Swali hilo likanifanya nimuangalie Bihawa, naye Bihawa alikuwa akinitazama kisha akamjibu muuguzi huku akiwa ananitazama;
" Aam aa! Ni majirani tuu. Yeye ni jirani yangu"
" Mbona kigugumizi bidada! Okay. Nashindwa kukuachia maagizo. Huyu anaishi na Nani kwani?"
" Nipe tuu maagizo muuguzi"
" Hapana! Nahitaji kumpa maagizo mtu anayeishi naye. Sio kila Jambo ninaweza kukuambia wewe kumhusu Mgonjwa"
" Nimekuambia niambie Mimi. Nani aliyemleta hapa? Sio Mimi niliyemleta? Nani kamletea chakula hapa? Ni Mimi au hunioni?"
Nilipoona wanataka kugombana ikabidi nizungumze.
" Muuguzi, Mimi pale naishi mwenyewe. Mji huu Mimi ni mgeni. Hivyo Bihawa anaweza tuu kusikia unachotaka kumwambia"
" Oooh! Kumbe! Sasa si angesema hivyo. Sina haja ya kumpa maelekezo kukuhusu. Sheria zangu za Kazi haziruhusu. Kama ni Kula kwa wakati nitasimamia Jambo hilo mwenyewe.."
Muuguzi akamaliza kisha akatoka, Muda huo Bihawa akawa anamsindikiza na macho ya chuki.

Alipotoka na kufunga mlango. Bihawa akaachia bonge la msonyo. Kisha akanigeukia.
" Huyu nesi hamnazo huyu. Atakuwa anakutaka sio Bure."
" Mmh! Sidhani. Nafikiri anafanya Kazi yake"
" D huna ujualo kuhusu Sisi wanawake. Tangu nimeingia hapa nimemwona namna anavyokuangalia na anavyokuongelesha"
" Hapana Bihawa! Ni Mtazamo wako tuu"
" Unamtetea si ndio?"
" Simtetei! Haya tuachane na hayo!"
" Kama anataka Umalaya si akafanye huo Umalaya wake. Mtcheeeewwi!" Akasonya.
Kisha akatoa lile hotpot kwenye kikapu na Sahani akapakua chakula. Akanipa, kisha akaendelea kumenya chungwa Muda wote ananiangalia kwa macho ambayo sasa nilianza kuyaelewa kwa namna nyingine Kabisa.

Baada ya kula chakula, akaniaga lakini nilikumbuka kuhusu simu yangu. Nikamuuliza simu yangu iko wapi. Akaniambia alipofika eneo nilipokuwa nimegongwa kulikuwa na watu wengi. Hakunikuta na simu.
Nikajua simu yangu ilikuwa imeibiwa.

Kesho yake niliruhusiwa, aliyenileta nyumbani alikuwa ni Yule muuguzi aliyekuwa ananiihudumia tangu siku ya Kwanza. Jina lake alikuwa akiitwa Cathy.

Tulipofika nyumbani kwangu nilimkuta Mzee Abeid ambaye ndiye mwenye Ile bodaboda. Moyo wangu ukapiga paah! Cathy aliona Hofu yangu tukiwa tunakaribia. Akaniuliza kulikoni nikamweleza kwa kifupi hali ilivyokuwa.
Tayari tulikuwa tumefika, nikamsalimu Mzee Abeid naye akanipa Pole ingawaje nilijua alichokifuata pale.
Nikamwambia ngoja niingie ndani alafu nataka kwaajili ya mazungumzo.
Akaniambia hajaja pale kuzungumza na Mimi.
Nikaingia ndani nikiwa na Cathy. Tulipofika ndani Cathy akatoa noti mbili za elfu kumikumi akanipa.
" Kampatie hizi huyo Mzee" akasema,
Nikatoka nikiwa nimezibeba zile pesa. Nikamkabidhi Mzee Abeid, nikamuona akijichekesha hovyohovyo kisha tukaagana.

********

Miezi mitatu ilipita nikiwa tayari nimezoea Kazi ya ubodaboda. Cathy ndiye aliyekuwa amenilipia shilingi Laki tatu za kujiunga kwenye kijiwe cha bodaboda.
Kila kijiwe cha bodaboda kilikuwa na Ada ya kujiungia kwa mara ya Kwanza kwa dereva bodaboda mpya. Bila kutoa Ada hiyo usingeruhuziwa kukaa kwenye kijiwe au kituo hicho cha bodaboda.

Mahusiano yangu na Cathy yalizidi kuimarika ingawaje hakuna miongoni mwetu aliyemuelezea Mwenzake hisia zake. Hata hivyo mioyo yetu ilikuwa kama sarafu moja. Nilihisi kumpenda Sana Cathy naye alionyesha hivyo.

Cathy alikuwa mwanamke Mzuri Sana. Msomi mwenye elimu ya Shahada ya uuguzi. Macho yake mazuri yenye huruma yalifanania Kazi yake ya kuhudumia wagonjwa. Sura yake ilikuwa nzuri pengine hiyo ilimfanya watu wengi wamuone kama ananyodo. Umbo lake lililopangika lilivutia Sana hasa alipokuwa Amevaa Sare zake za Kazi.

Nilikuwa najua Cathy anasubiri kwa Hamu nimwambie ninampenda kisha safari yetu ya Mapenzi ianze upya.

Ni miezi mitatu sasa imepita. Sijui nianzie wapi kumueleza ukweli wa Moyo wangu Binti huyu. Kipato changu ni Duni. KAZI yangu ya kufukuzana na upepo. Ubodaboda. Nitampa nini mwanamke msomi mwenye Kazi yenye kipato zaidi yangu. Nikifikiria hali yangu hiyo ilinifanya nifute Kabisa Wazo la kumwambia Cathy ukweli.

Kama haitoshi, tetesi na duru za mtaani nilizokuwa nazipata zilikuwa zinasema matajiri wa Kiwangwa walikuwa wakiingia na kutoka wakipigana vikumbo kulipata penzi la Cathy. Nilikata tamaa Kabisa niliposikia tajiri anayemiliki kile kiwanda cha Nondo na bati nilichokuwa nafanyia Kazi pia anamfuatilia Cathy. Embu fikiria hata wewe, ungethubutu.?

Unaweza kuniambia nijaribu, mwanaume kujaribu na kujiamini. Hata Mimi kuna wakati nafikiri kama wewe. Lakini Sauti nyingine hunong'ona masikioni mwangu ikiniambia akinikataa nitakosa hata ule ukaribu mdogo niliokuwa nao dhidi yake.
Nikifikia hapo naghairi.

Bihawa naye hakuwa nyuma, yeye ndiye alikuwa ananiona karibu kila siku kwani alikuwa ni lazima kila jioni aniletee chakula cha usiku. Nilishindwa kumkatalia na ningeanzaje kumkatalia mwanamke ambaye alinisaidia kwa gharama zake Kunichukua nikiwa sijitambui siku Ile ya ajali Mpaka Hospitalini kisha akawa ananiletea chakula na hata gharama za matibabu yeye ndiye aliyetoa. Ningewezaje? Nakuuliza!

Licha ya kuwa Bihawa alikuwa mwanamke Mzuri mwenye stara lakini Moyo wangu haukuanguka kwake. Sikuwa nahisia naye. Lakini nitamlipa nini kwa haya anayoendelea kunifanyia. Kila anapokuja kwangu nahesabu deni linaongezeka juu yangu kwake.

***********
Jioni Moja nikiwa nimetulia ghetto kwangu nilimkumbuka Mama yangu. Ni miezi kadhaa imepita sijawasiliana naye Hali ya majuto na kujilaumu kwa kutokumjali MMA yangu vikaukumba moyo wangu. Haikuwa kawaida yangu Mimi kukaa Muda wote huo bila kuwasiliana na Mama yangu. Kikawaida ilikuwa kila siku lazima niwasiliane na mama. Lakini tangu nilipopata ajali namba yake haikuwa imepatikana tena.

Uzembe nilioufanya ni kuwa namba niliyokuwa naitumia haikuwa namba iliyosajiliwa kwa majina yangu. Hivyo kuirudisha kwa matumizi hata baada ya siku kuibiwa isingewezekana. Nilikuwa najilaumu Sana kwa Jambo hilo.
Msomi mzima mwenye Shahada ilikuwaje sikutambua umuhimu wa kutumia laini iliyosajiliwa kwa majina yangu mwenyewe.
Nilikuwa nawaza nikijilaumu.

Ninakaakiba ka Laki tatu, ikifika Laki tano nitaenda Morogoro chapu kumwona Mama. Atafurahi Sana. Nitambebea na zawadi ya nguo.
Bado nilikuwa nawaza.

Wakati nafikiri hayo, punde anaingia Bihawa akiwa amebeba chakula. Kama kawaida Yale alikuwa amevaa hijabu.
Jambo Moja ujue ni kuwa wakati wote huo tangu wakati wa ajali Mpaka wakati huu Bihawa alikuwa akifanya mambo hayo kwa usiri Mkubwa majirani bila kujua ingawaje baadhi ya watu walishaanza kuhisi mahusiano yetu.

Alikuwa kaleta Wali Samaki, kama kawaida lazima aje na chungwa.
Tofauti na siku zote mara hii Bihawa aliniomba Jambo;
" D samahani naomba kwenda msalani"
Sikuwa na ubishi nikamruhusu. Akaniacha sebuleni akaingia zake chumbani ambapo huko kuna Choo na bafu.
Nikawa nakula zangu lakini huko nje manyunyu yakaanza, kwani ulikuwa msimu wa Mvua.

Mpaka nakaribia kumaliza chakula Bihawa alikuwa hajatokea.
Huko Nje Mvua ilikuwa imeshachachamaa.

Mara Mlango unagongwa, Nani atakuwa anagonga Mlango usiku huu WA saa tatu kwenda Sana nne. Kikawaida Mimi sinaga wageni zaidi ya Cathy, Bihawa au mwenye nyumba.
Na mwenye desturi ya kuja usiku na Bihawa ambaye nipo naye. Cathy' hajawahi kuja usiku hata siku Moja ila akijaga anaondoka usiku mnene tofauti n Bihawa.
Mwenye nyumba yeye Hanaga hayo mazoea na haishi hapo. Majirani zangu wao hatujawahi kusumbuana usiku.

Nikafika Mlango nikauliza Nani.
Mara nasikia Sauti Cathy, " Ni Mimi mpenzi. Fungua Mvua inaninyeshea"

Moyo unapiga Paaah!
Hofu na kuchanganyikiwa kwa pamoja vilinivamia.
"Fungua D nalowa"
Hapohapo kabla sijafungua nasikia Sauti kwa nyuma ikiniambia ni Nani. Nageuka namkuta Bihawa amevaa kanga tuu kaipitisha kwenye makwapa ametoka kuoga. Amesimama katikati ya mlango unaotenganisha Sebule na chumba.
" Fungua Baby nalowa jamani"
Inanibidi nifungue. Nafungua mlango Cathy anapita upesiupesi akiwa amelowa chapachapa Akiwa kavaa nguo zake za kazini.

Inaendelea;

Nini kitatokea..?
Usikose sehemu ya Pili?

Mapenzi au Kazi?
Je Pesa Itakupa furaha?
Ni upi uchaguzi sahihi katika Mapenzi?
Uhalifu usiokusudia unapotokea nani atawajibika?

Mtunzi Robert Heriel
CEO Taikon Publishers,
CEO Taikon Cleaning Services,
+255693322300
Ongeza juhudi kijana, umfikie UMUGHAKA
 
MY LAST RIDE; SAFARI YANGU YA MWISHO.
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Episode 03
Ilipoishia
• Simu ya Dimoso inaita. Yule mwanamke na Yule Mzee wa Makamo ambaye kapewa mtoto mchanga wanageuka upande Sauti ya simu inapotokea. Hawajui Dimoso alikuwa anawatazama.

ENDELEA

Mambo yalikuwa yameharibika. Simu ilinikatili Sana. Mapigo ya moyo yalianza kuchanganya, niliogopa Sana. Nikawa najificha huku nikikazana kuikata simu ili isiendelee kuita. Kitendo hicho kiliwafanya Yule mwanaume wa Makamo na Yule mwanamke kuona Mwanga wa simu ingawaje nilikuwa umbali wa Mita kama hamsini hivi.
Mara nikamwona Yule mwanaume wa Makamo akitoa bastola yake aliyokuwa ameificha nyuma ya mgongo kiunoni baada ya kulipangua koti lake jeusi la Mvua.

Nisingeendelea kusubiri Kifo. Nilielewa kuwa biashara iliyokuwa inafanyika ilikuwa ni kumnunua Yule mtoto mchanga. Kwa upesi nikaamka nikiikimbilia pikipiki yangu ilikuwa kwenye kichaka huku Mvua ikiendelea kunyesha. Kabla sijaifikia pikipiki niliteleza mara mbili na kuanguka chini kutokana na matope.
Wakati huo nilimsikia Yule mwanaume wa Makamo akifoka;
" Simama! Simama wewe Mbuzi! Nitakumwaga Ubongo"
Sikutaka Kumsikiliza, nikanyanyuka na kuiwahi pikipiki yangu kisha nikapanda juu ya pikipiki. Ghafla nikasikia milio wa risasi. Kitete na kutetemeka vikaniingia. Nilipagawa haswa. Mara nipige starter mara niingize Mkono mfukoni kuchukua funguo ili niwashe pikipiki.
Ni Mpaka risasi ilipopiga kwenye bampa la Mbele la tairi nipo Akili yangu ilipofyatuka.
Nikawasha pikipiki kisha nikaondoka kwenye kile kichaka kama mshale.

Yule mwanaume nikamwona kupitia kioo cha pikipiki akinikimbiza kwa Miguu huku akifyatua risasi lakini alikata tamaa. Nyuma yake nikamwona Yule mwanamke aliyebeba mtoto akichukua picha, nikazima taa ya nyuma ya pikipiki ili plate number isijechukuliwa na camera ya yule Mwanamke. Sijui kama nilifanikiwa kuzuia Mpango wake.

Nikatokomea nikiwaacha kwenye Giza Nene huku Mvua ikiwanyeshea wakitazama upande wa Kiwangwa nilipopotelea.

************
Nilimkuta Bihawa akiwa yupo mtandaoni anaperuzi.
"Honey umerudi!"
Bihawa aliongea huku akinyanyuka kwenye sofa. Huku akinitazama machoni.
" No! No! Usisumbuke, endelea na ulichokuwa unafanya." Nikasema huku nikijaribu kumzuia Bihawa asije pale Mlango nilipokuwa naingiza pikipiki. Sikutaka aone jinsi Digadi la Mbele la pikipiki lilivyoshambuliwa na risasi.
Bihawa akabaki ananitazama huku akinidadisi,
Nikaicha pikipiki pale Mlangoni kisha nikamfuata huku nikijisemesha
"Oooh! Baby, I'm sorry! Najua unanijali Sana. But sipendi uhangaike. Sawa Bebe!"
Niliyasema hayo tayari nikiwa nimemkumbatia kisha nikambusu mdomoni.
" Oooh! Sorry! Nimekulowanisha na hili koti langu lililolowana kwa Mvua"
"Usijali Mpenzi, hata hivyo tunaenda kuoga wote" Bihawa akasema kwa madeko!
" Kwamba Muda wote ulikuwa haujaoga, ulikuwa unanisubiri Mimi ?"
" Sio kuoga tuu hata Kula sijala. Nilikuwa nakusubiri wangu wa ubani. Nikioga mwenyewe bila ya wewe sitakati na Nikila chakula bila wewe hakishuki"
" mambo hayo " nikasema kisha nikambusu.

Alafu nikamuagiza akaweke Maji ya kuoga. Akatoka akaenda kuweka. Nimatumia Nafasi hiyo kuiingiza ndani pikipiki kisha nikaifunika na lile koti jeusi nililokuwa nimelivaa.

Tukaoga wote kisha tukala chakula. Alikuwa ameleta Mtori wa nyama, kama kawaida na chungwa lilikuwepo.
Baada ya kula tulienda chumbani, Bihawa akaniambia siku hiyo atalala kwangu. Mmmh! Kidogo nimkatalie ukizingatia nilikuwa nimepanga asubuhi ningebadilisha lile Digadi la Mbele la pikipiki lilipopigwa risasi.
Lakini nikashindwa kumzuia.

Nilikuwa nimechoka Sana. Hivyo hata wakati wa kupeana tendo nilifanya chini ya kiwango. Tukalala yapata usiku wa saa sita hivi kwenda Saa Saba.

Bihawa akalala akaniacha Mimi nikiwa naperuzi mtandaoni. Nilipochoka. Mawazo yakanijia kuhusu tukio la Kule PF55. Nikaifungua Ile video niliyokuwa narekodi tukio la wale majambazi waiba Mtoto Kule PF55.
Video haikuwa inaonyesha vizuri kutokana na Giza pamoja na Mvua. Yule mwanaume wa Makamo pamoja na Yule mwanamke sura Zao hazikuwa zinaonekana vizuri. Nguo Zao pekee ndizo zilizokuwa zinaonekana vizuri.

"Hivi kama wangenikamata nini kingetokea? Vipi Ile video aliyokuwa anarekodi Yule Mwanamke. Dimoso umejiingiza kwenye matatizo yakujitakia. Sasa ndio nini hii! Vipi kama watanifuatilia" nilikuwa nawaza nikiwa nimelala kitandani. Muda huo Bihawa alishakuwa amesinzia kitambo.

Saa kwenye simu ilionyesha ni saa Saba inaelekea saa nane za usiku.
"Hapa nikafungue lile Digadi la Mbele lililohapigwa risasi" nikawaza huku nikiamka kutoka kitandani.

Nikafika sebuleni mahali ninapoiwekaga pikipiki. Nikakumbuka natakiwa vifaa vya kufungulia nati zilizoshikilia Digadi kwenye tairi. Nikarudi chumbani. Nilikuwa nimeweka vifaa hivyo chini ya uvungu wa kitanda. Nikavichukua na kurudi sebuleni.

Wakati nahangaika kufungua ghafla nikasikia Sauti kutoka nyuma yangu.
" Baby! Twende Kulala. Utafanya Kazi hiyo Kesho" alikuwa ni Bihawa.
Muda huo nilikuwa nimeshalifungua.
" Usijali! Hata hivyo nimeshamaliza. Kesho asubuhi kuna Mteja aliniambia nikamchukulie Mzigo Makurunge. Ndio maana nimeona nifanye Kazi hii usiku huu ili asubuhi nikiamka ni kuwasha na kuondoka"
Bihawa akanitazama kwa macho ya uchovu wa usingizi huku akiwa ameshika kiuno chake na Mkono wa kushoto, Mkono WA kulia ukiwa umeegemea muimo wa Mlango. Kanga aliyokuwa ameivaa ikiwa imekaa kihasarahasara.

" D wewe ni Kijana mchapakazi Sana. Ni tofauti na vijana wengi wa siku hizi. Unafanya Kazi usiku na mchana bila kuchoka. Jua Lako Mvua yako. Nimekuvulia kofia mpenzi" Bihawa akasema huku Midomo yake ikimkatisha akaachia mwayo mrefu ulimfanya atoe vimachozi kwenye macho yake.

"Twende tukalale mpenzi" nilikuwa nimeshamaliza nimelibeba lile Digadi kwa kifichoficho ili asilizingatie na kuona lile Tundu la risasi. Nikamshika kwenye kiuno chake laini alafu tukaingia chumbani. Lile Digadi nikalitupia chini ya uvungu.
Kisha nikajitupa kwenye kitanda na kumrukia Bihawa aliyekaa kimzagao ili kunilaki pale kitandani.
Hatimaye nikalala!

****
Asubuhi kumekucha simwoni Bihawa kitandani. Nakurupuka upesiupesi nikaenda Sebuleni nikamkuta anaandaa chai, tayari alikuwa ameshaweka vitafunio vya maandazi juu ya stuli iliyokuwa mule ndani kwani sikuwa nimenunua meza.
" Umeamka! Pole na uchovu Bebe. Nilijua kwa ulivyochoka Jana usingeweza kuroka asubuhi Asubuhi"
" Kwa sasa hivi ni saa ngapi?"
" Hujachelewa Sana. Saa mbili na nusu hivi"
" Haah! Saa mbili? Mungu wangu! Muda huu ndio ningetakiwa niwe ninarudi kutoka Makurunge "
Nikawa naingia ndani chumbani ni kama Bihawa akajua naifuata simu.
" Simu hii hapa mpenzi" Moyo ukapiga Paah! Nikabaki nimesimama nikiwa nimetazama Mlango wa chumbani nikiwa nimempa Bihawa Mgongo.
Alafu nikageuka nikamtazama kwa macho ya kumsaili kujua kama aliifungua Ile video.
"Kwani vipi? Mbona unaniangalia hivyo?"
Akasema, sikumjibu nikabaki namtazama.
" D vipi! kuna tatizo?"
" Hapana!"
Nikamjibu huku nikimfuata na kuchukua simu yangu. Akawa ananiangalia, nami nikabonyeza bonyeza simu kama sekunde kadhaa kisha nikatamzama bila kusema kitu naye akawa ananiangalia kwa wasiwasi.
Kisha kwa ghafla nikacheka kwa nguvu huku nikimtazama usoni.
" Hahahaha! Umeogopa eeenhe!"
" Muone! Umenitisha ujue"
" I'm sorry! Lakini nimeigiza vizuri"
" Sio Siri kama ni kuigiza unajua. Embu tukae Ile. Nataka niende nyumbani mara Moja Binti yangu Kuluthumu atakuwa na hamu kuniona"

Tukaa tukala na kunywa kifungua kinywa,
Wakati tunakula Bihawa alikuwa wakwanza kuzungumza;
" D ninaweza kukuuliza swali?"
Kichomi kwenye kifua kilipita shaaa! Mawazo yangu yaliniambia huenda Bihawa ameiona Ile video hivyo anataka kuuliza kuhusu video hiyo. Kwa kweli sikutaka mtu yeyote aione video Ile. Nilihisi mtu yeyote akiiona haina tofauti na wale majambazi nao watakuwa wameiona. Nakumbuka Baba yangu kabla hajafa aliwahi kuniambia Dunia haina Siri. Kama hiyo haitoshi hakuna Siri ya watu wawili.
Baba yangu alinisisitizaga kuwa kamwe nisifanye Siri na Mwanamke, kwani mwanamke hana kifua.
Sasa ikiwa Bihawa ameiona Ile video itakuwaje? Siri hii ataweza kubaki nayo kifuani?

Hayo maswali yalikuwa yakipita katika Akili yangu huku nikiwa nimeangalia kwenye sahani yenye maandazi nikiwa natafuna mdomoni.
" Dimoso!"
" Naam B" nikainua kichwa kumtazama Bihawa.
" Nimesema nikuulize swali?"
" Uliza tuu. Swali gani?"
" Hivi unampango gani na Mimi? Maana naona siku zinaenda naona kimya" akasema huku tukitazamana. Kimya kikapita Mimi nikiwa nafikiri nijibu nini huku nikishukuru hajauliza swali kuhusu Ile video.
" Unajua tuna miezi mitatu Mpaka sasa tangu tuwe pamoja?"
" Hivi eenh" miezi mitatu?"
" Tena wiki lijalo tunaingiza miezi minne. Lakini mwenzangu naona kimya. Ni kama Umeridhia tuishi hivi"
" Unamaanisha nini Mpenzi"
" Hunielewi au unanizuga?
" Najaribu kukuelewa Bihawa lakini bado sikupati"
" Hahah! Wana..ume! Haya tutaishi hivi Mpaka Lini?"
" Oooh! Hapo nimekuelewa! Unazungumzia kufunga Ndoa?"
" Eeenhe! Unajua sio adabu kuishi hivi kihuni. Wazazi wako hawanijui, siwajui. Wewe kwetu huna unayemjua na hakuna anayekujua. Wewe unaona ni Sawa kweli?"

"Uuh!" Nikashusha pumzi. Kwa kweli Maneno ya Bihawa yaliongeza uzuri kwenye Akili yangu. Mimi nioe wakati Kula yangu ya shida. Kwa kweli nisingeweza kuruhusu Jambo hilo litokee. Alafu kingine bado Bihawa hakuwa amenivutia kumfanya awe Mke wangu.
Sio kwamba Bihawa alikuwa mbaya hapana. Niseme ukweli Bihawa alikuwa mwanamke Mzuri Sana, mwenye sifa zote ambazo wanaume wengi huzitafuta kwa Wanawake lakini kama ujuavyo moyo ndio huamua linapokuja swala la mapenzi. Moyo wangu bado ulikuwa Mgumu kama moyo wa Farao. Haukutaka kumruhusu Bihawa aingie ndani.

" D! Mbona Kimya!"
"Haaa! Umenishtukiza Bihawa"
" Mmmh! Nimekushtukiza. Kwa hiyo kumbe hujawahi kulifikiria Jambo kama Hilo Kabisa"
" Hamna sio hivyo!"
" Sio hivyo vipi? Au Basi usijeona Mimi ndio na kulazimisha. Kwa kheri"
" Subiri Basi, kwa hiyo umekasirika?"
" Tutawasiliana kwenye simu"
Bihawa akaniambia huku akichukua Mkoba wake akaondoka na kuniacha nikiwa Mlango na Bukta nikiwa kifua wazi.

**********

Habari kubwa mtaani iliyokuwa inaendelea ni mwanamke Mmoja wa Kiwangwa kuzaa Panya aliyekufa.
Panya! Ndio Panya huyuhuyu tena Panya Buku. Alikuwa Panya Mkubwa Sana. Ilikuwa habari ya ajabu Sana ambayo sio tuu ilivuma pale Kiwangwa bali ilipenyeza Mpaka kwenye anga la kwenye mitandao ya kijamii na kuvuma na nchi nzima.

Vyombo vya habari kama luninga na radio ndio ilikuwa habari kuu.
" Mwanamke Mmoja ajifungue Panya Buku" hiyo habari kwa mara ya Kwanza niliipata nikiwa natoka kununua Digadi jingine nikiwa tayari nimelipachika kwenye tairi la Mbele.
Kilichonishtua na kunifanya niachie ukelele "haaaa! Ni kusikia tukio hilo limetokea katika kituo cha afya cha Kiwangwa.

Nilihisi akili yangu ikijawa na upepo, ikawa inapoteza mhimili wake na kunifanya nikose utulivu. Nilijikuta nikilihusisha tukio Hilo la mwanamke kuzaa Panya na lile la usiku wa Jana kile PF55.
" Uongo! Uongo huo! Huo ni Uongo msidanganye watu!" Nilisema nikiwa ndio naingia Kiwangwa nikitokea Makurunge.

Kituo cha afya nilikuta watu wengi wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio hilo. Ni kama mji mzima wa Kiwangwa ulikuwa umehamia pale. Watu walikuwa wengi Sana.
Nikatafuta sehemu nikaiweka pikipiki yangu kisha niasogea kwenye ule umati Kupata habari Kamili ambayo kiini chake nilikuwa nakijua.

Polisi walikuwa wameshafika, nikamwona mwanamke Mmoja akilia kwa uchungu. Nikagundua ndiye ambaye watu wanafikiri amejifungua Yule Panya Buku. Alikuwa akilia sana. Alikuwa kajifunga kanga huku akilia.
Mara kwa mara Polisi walikuwa wakituliza watu,
Nilijikuta machozi yakinilenga lenga kwa hisia za huruma. Niliposikia Maneno Maneno kuwa kumbe Yule dada ametafuta mtoto kwa Muda mrefu. Ndoa yake inamiaka zaidi ya kumi na tano bila ya mtoto. Hatimaye akajaliwa Kupata ujauzito lakini matokeo yake ndio haya ya kujifungua Panya Buku.

Watu wengi pale walilihusisha tukio Hilo na mambo ya kishirikina. Kila nilipopita watu walisema Yule mwanamke alitupiwa Uchawi Mkubwa Sana. Wengine niliwasikia wakisema ule ni Uchawi wa jinni anayeishi kwenye Mikuyu Dume.

Mama Mmoja nilimkuta akiwa amezungukwa na Makumi ya watu akawa anasimulia;
"Huu ndio Uchawi hatari zaidi. Huyu mwanamke itakuwa alichukua Mume wa Mtu au Mchumba WA mtu. Kule kwetu kuna Uchawi wa Jinni la kwenye mkuyu Dume. Asalala! Hakuna Uchawi hatari kama huo. Mtu akikuibia Mchumba au Mume unaenda kwa huyo Mzee Sabaro, Mzee Hatari huyo. Atakuchukua kisha mtaenda kwenye Moja ya Mikuyu Mikubwa sharti iwe dume. Alafu atafanya uganga wake kumtoa jinni kwenye ule mkuyu. Kisha atakupa masharti kulingana na Nyota yako. Ukiyatimiza hayo masharti huyo aliyekuibia huyo Mchumba au Mume lazima atazaa Kiumbe cha ajabu. Wengine wanazaa Panya Buku kama huyu mwanamke..."

" Wewe mama Acha Uongo" nikamkatisha, umati mzima ukanigeukia na kunitazama. Kisha ukaanza kunisakama huku ukinizomea,
Wengine nikawasikia wakisema "hawa ndio Wachawi wenyewe"

Mimi nilijua Yule mwanamke hakuwa amezaa Panya isipokuwa mtoto wake ameibiwa. Na waliomuiba nilikuwa nawakumbuka kwa sura wale wanaume wawili. Yule mwanamke pekee ndiye nilikuwa simjamuona.

Nikaamua kuondoka kwenye ule umati uliokuwa unamsikiliza Yule Mama. Nikaona nihame upande nisije nikapigwa.

Ghafla watu wakaanza kusukumana na kupigana vikumbo huku wakikazana kuangalia upande mwingine. Sikutaka kupitwa. Nilipotazama nilishtuka kuona Polisi Mmoja Akiwa amebeba mfuko wenye Panya Buku aliyelowa damudamu.
"Waliokuwa wanabisha! Panya si Yule pale! Yule pale" kijana Mmoja aliropoka.
" Jamani Yule pale!" Sauti ya mwanamke ilisikika. Lakini sikumwona aliyekuwa amesema.
" Haa! Panya! Panya Buku!"
Makelele mtindo Mmoja. Vurugu na kelele zilitawala eneo lile.

Mara ghafla nilishtuka kumwona Yule Kijana ambaye Jana yake alikuwa na yule mwanaume wa Makamo wakiwa wanakula Kule kwenye Mgahawa wa Bihawa.
Macho yangu yalijikuta hayana nguvu yakavutwa kwake. Muda wote nilikuwa nikimtazama. Yule Kijana naye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakishangaa tukio lile. Lakini Mimi nilijua anaigiza tuu.

Ghafla nikamwona akiangalia kwa mbele Kabisa upande mwingine. Nami nikatazama Kule alipokuwa ametazama, nikamwona Cathy Akiwa anatembea kwenye korido za wodi sikujua ni wodi gani. Nafikiri umbo la Cathy lilimvuruga Yule Kijana muuza mtoto.

Kwa upesi niliwapangua watu waliokuwa pale nikijaribu kumuwahi Cathy. Hatimaye nilifanikiwa kumfikia.

Cathy alishtuka kuniona pale;
" Dimoso! Upo!"
" Huu! Huu! Huu!" Nilikuwa napumua harakaharaka kutokana na kumkimbilia Cathy!
" Ni Muda sasa!"
" Nipo Cathy! umeshtuka Sana! "
" Eenh! Kukuona lazima nishtuke. Miezi miwili sasa"
" We Acha tuu! Tangu unifungie vioo"
" Uliniudhi Sana D."
" I'm sorry Cathy! Haikuwa vile"
" Stop! Kimya! Mtu mnapika pakua useme haikuwa vile"
" But.."
" Nini? Sikia kwa sasa nipo busy, naenda kupiga round wodini kuwapa wagonjwa Dawa"
" Daaah! Kwa hiyo mikazo inaendelea"
" Uliitaka mwenyewe!" Akasema, hapo nikabaki nimemtazama naye ananiangalia kwa macho ya kiburi. Kisha akawa anaondoka. Nikawa nimuangalia akitikisa makalio yake polepole kwa madaha.
" Jioni uje nyumbani" nilishtuka aliposema hivyo.
Nikamfuata nikiwa nyuma yake " D sitaki kufuatwa nyumanyuma. Nitaghairi usije hiyo jioni"
Niliposikia hivyo nikasimama kama afande aliyeambiwa attention. Kisha nikamwambia nimemuelewa.
Nikamsindikiza Mpaka alipofika kwenye Mlango Mmoja akaufungua na kutokomea ndani.

Nikageuka Kule kwenye umati. Nikagongana macho na Yule Kijana muiba watoto, kumbe alikuwa akitutazama Mimi na Cathy tukiwa tunaongea.Nikampuuza.

NIkaamua niondoke zangu niende nikapumzike Nyumbani. Ilikuwa tayari saa sita hivi inaenda saa Saba mchana. Nikiwa napanda kwenye pikipiki ghafla nasikia Sauti ya Mtu ikinisemesha. Nikageuka, nilishtuka kumwona Yule Kijana Akiwa nyuma yangu amesimama. Yule Kijana muiba mtoto.

Itaendelea

Nini kinafuata?
Je mapenzi baina ya Cathy na Dimoso yatarejea?
Muuza mtoto anataka nini kwa Dimoso?
Je ameshamshtukia Dimoso kuwa ndiye aliyewaona Kule PF55?

Usikose sehemu ya 4

Robert Heriel
CEO Taikon Publishers
CEO Taikon Cleaning Services
+255693322300
 
MY LAST RIDE; SAFARI YANGU YA MWISHO.
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Episode 04.
Ilipoishia....
NIkaamua niondoke zangu niende nikapumzike Nyumbani. Ilikuwa tayari saa sita hivi inaenda saa Saba mchana. Nikiwa napanda kwenye pikipiki ghafla nasikia Sauti ya Mtu ikinisemesha. Nikageuka, nilishtuka kumwona Yule Kijana Akiwa nyuma yangu amesimama. Yule Kijana muiba mtoto.

ENDELEA..

Yule Kijana muiba watoto akanisogelea. Kisha akanisalimu. Nilimuitia kwa kichwa bila kutoa Sauti huku macho yangu yakiwa yapo mbele ya macho yake.
" Wewe ni bodaboda" aliniuliza. Akiwa bado ananitazama machoni nami nikiwa nayatazama macho yake.
" Unataka nini?" Nikamuuliza.
" Ungenijibu! Wewe ni bodaboda au sio. Kuniuliza nataka nini sio jibu" akasema huku pumzi zake zikiwa zinaanza kuchanganya.
" Wewe unaona Niko na chombo alafu unauliza"
" Kwamba kila mwenye pikipiki ni bodaboda?"
" Kwa hapa kiwangwa Hilo ni jibu" nikamjibu wakati huu nikiwa nimechomw fungua kwenye pikipiki ili niiwashe. Kisha nikamuuliza, " unaenda wapi?"
" Nipeleke Msata"
" Msata?"
" Ndio! Shilingi ngapi?"
" Aaah! Bei ya Msata ni elfu thelasini "
" Mmh! Mbona unabei Sana"
" Hapana Boss, ndio bei yake. Tafuta dereva yeyote umuulize"
" Nakupa ishirini na tano"
" Hailipi Boss" nikasema nikiwa ninamtazama pikipiki ikiwa inanguruma. Kisha nikaendelea kumwambia " Mafuta yapo juu Sana. Hapo faida napata elfu kumi tuu. Hela nyingine yote inapotelea kwenye Mafuta"

" Sawa! Sio Kesi! Tutaends Kwanza Kiwangwa Lodge kuna begi langu naenda kulichukua. Kisha safari itaanzia huko"
" Haina shida Boss. Panda tuondoke"
Akapanda kisha Moja kwa Moja nikampeleka Mpaka Kiwangwa Lodge. Hapo akashuka akaingia ndani ya Kiwangwa Lodge. Akaa kama dakika tano hivi alafu akatoka akiwa amebeba begi la mgongoni lakini mara hii alikuwa amevaa kwa juu koti la ngozi huku kichwani Akiwa amevaa kapero.
" Twenzetu Mkali" akasema Akiwa anapanda juu ya pikipiki.

Safari ya kutokea Kiwangwa kuelekea Msata ikaanza. Siku hiyo haikuwa na manyunyu ingawaje anga lilikuwa limetawaliwa na mawinga ya Mvua. Hali ya hewa ilikuwa ya mashaka kwamba Muda wowote Mvua ingeweza kushuka.
Kimoyomoyo nilikuwa naombea Mvua isije ikanyesha Mpaka nitakapokuwa nimerudi.

Hakuna aliyekuwa anamsemesha Mwenzake. Mngurumo wa pikipiki na upepo ndivyo vilikuwa vikirindima.
Mawazo yangu yaliniambia kuwa lile begi ambalo Yule Kijana alikuwa amelibeba mgongoni ndilo lililokuwa na pesa. Sijui kwa nini nilihisi hivyo lakini niliziamini hisia zangu.
"Milioni kumi na tano kwenye begi" niliwaza. Kuna Muda tamaa ya Kutaka kumuibia Yule Kijana zilikuwa zinakonyeza. Lakini nilikuwa na Hofu.
Kama ningeziiba zile Milioni kumi na tano zingenifikisha sehemu kimaendeleo.
Sasa nilifikiri nitakapoziiba zile milioni kumi na tano za Yule Kijana ningefanyie Jambo gani. Akili yangu ikawa inawaza, kuna nyumba, kuna gari.
Nitajenga nyumba. Nawaza bado. Lakini Akili nyingine ikawa inanicheka. Nyumba ya Milioni kumi na tano. Mbona hiyo pesa ndogo.
Milioni kumi tano haiwezi kujenga nyumba labda nijenge kajumba kadogo kwenye vyumba viwili hivi.

Bora ninunue gari. Nikawaza. Wazo hilo likawa bora kwangu.
Sasa Mawazo yangu yakaonyesha picha kama mkanda wa video jinsi nilivyonunua gari.
Safari yangu ya Kwanza nitaenda Morogoro kwa Mama. Atafurahi Sana. Nikamwona Mama akinipokea kwa furaha huku akipiga shangwe na vigelegele. Mara afungue Mlango wa gari mara afungue. Mara aende mbele ya gari kisha alale juu yake Basi ilimradi furaha yake itakavyokuwa inamtuma.
Nilijikuta natabasamu huku bado nikiwa naendesha pikipiki nikikata upepo kuitafuta Msata.
Tamaa ilikuja kwa nguvu Sana. Lakini nikakumbuka nitalichukuaje lile Begi. Nitamuibiaje Yule Kijana zile pesa.

Mji wa Kiwangwa ni Mji mdogo. Vituo vya bodaboda ni vichache. Kiasi kwamba msako wa kunitafuta na kujua aliyefanya tukio ni Mimi ungechukua masaa machache tuu.
Kutoroka isingewezekana kwa Sababu tayari Nina Mkataba na Yule Mzee Abeid ambaye jina langu lipo kwenye mkataba pamoja na vitambulisho vyangu. Kama hiyo haitoshi najua rafiki yangu ambaye ameenda Kiteto huko Manyara angetafutwa na angewapeleka nyumbani kwetu Morogoro kwa Sababu anapajua niliwahi kumpeleka mara Moja Kipindi tupo Chuo mwaka wa Kwanza.

Kufikia hapo Mpango ulikuwa umekufa.
Lakini Wazo jingine likaja. Vipi Ukimuua?
Nilishtuka wapi Wazo Hilo limetokea. Kwa kweli sikuwahi kufikiri kumbe kwenye Akili yangu kuna Kona ya mawazo Mabaya yaliyojificha.

"Niue Mimi"
" Ndio wewe uue upate hizo pesa"
" Siwezi! Haiwezekani Mimi kuua!"
" Haujaamua tuu. Maisha yanahitaji moyo Mgumu na maamuzi magumu. Unafikiri kwa namna hii ya kufukuza upepo utatoboa kweli?"
" Sasa nitafanyaje. Kuua mtu ni Kazi".
" Sikia Dimoso, wewe sio muoga Kiasi hichi Wala wewe sio mwema Sana Kiasi cha kujifanya malaika. Ukiamua unaweza Kabisa kuua huyu Kijana"
Mawazo yangu yalikuwa yakibishana. Bado nilikuwa naendesha pikipiki nyumba yake nikiwa nimempakiza Yule Kijana muiba mtoto.
" Kwanza huyu Kijana hizi pesa kazipata kimazabe. Ukimuua hutakuwa na hatia yoyote"

Wakati nawaza hayo mara, nikaikatisha pikipiki nikaiingiza upande wa mapori. Yule Kijana akawa ananiambia unanipeleka wapi. Nikawa simjibu chochote zaidi nikawa naongeza mwendo kulikabili pori. Yule Kijana akawa anapiga makelele " huko wapi! Huko wapi!"
Nikapunguza mwendo na kusimami pikipiki! Kisha nikashuka nakumuacha kwenye pikipiki.
" Subiri naenda kukata Gogo" nikamwambia.
Yule Kijana akawa ananitazama kwa macho ya mashaka huku akinidadisi usoni.
" Sasa si ungesema tuu!"
" Sorry! Acha niwahi nahisi tumbo la kuhara. Hujabeba Maji hapo" nikawa naongea huku najikunjakunja kama Mtu anayejizuia asijinyee.
Yule Kijana akaniambia hajabeba Maji. Huku akiniambia niharakishe nisije kudondosha vitu. Niliacha funguo ya pikipiki makusudi ili kujenga Imani.

Nikapotelea kwenye vichaka nikawa nazuga kama ninaendesha. Baada ya dakika kadhaa nikainuka kwa kujificha nikawa namchungulia Yule Kijana. Nikamwona Akiwa anabonyeza bonyeza simu yake akiwa Hana hili Wala lile.
Nikaona ndio Muda sahihi wa kumuua. Kwa bahati pembeni yangu nikaona Gongo la mti. Nikalichukua kisha nikamnyatia polepole kwa nyuma Mpaka nilipomkaribia, alipohisi nyuma kuna mtu akaangalia kwenye kioo cha pikipiki, maskini alikuwa amechelewa aliambulia kuona sehemi ya gongo likiwa linakuja kupiga kichwa chake. Sekunde alizobakiwa nazo hazikumruhusu kukwepa. Hatimaye akadondoka chini huku damu zikimtoka piani na mdomoni.

Nilikuwa nimeduwaa nikiwa nimelishikilia lile Gongo la mti nikiwa tayari kumpiga pigo jingine ikiwa angetaka kufurukuta. Alikuwa amekufa. Nikamtoa begi alilokuwa amelivaa mgongoni. Mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakipiga mno. Nikafungua lile begi. Hamadi! Nilijikuta natabasamu kuona mabulungutu ya pesa. Kama nilivyokuwa nimebeti.
Natabasamu lakini ghafla tabasamu linayeyuka baada ya kusikia Sauti za watu zikisema ameua. Hapo nikageuka upande ambapo Sauti hizo zinatokea. Nikawaona wa Masai wawili. Nimekwisha!

Hayo yalikuwa mawazo tuu ambapo yalikatishwa na swali la Yule Kijana muiba watoto niliyekuwa nimembeba tukielekea Msata.
" Yule Muuguzi mnafahamiana?"
Nikamtazama Yule Kijana muiba mtoto kupitia kwenye Kioo pasipo kumjibu. Akaendelea kuongea;
" Yule mwanamke ni mzuri Sana. Sema Wakubwa wengi wanafukuzia pale. Kuna Mkurugenzi wa kile kiwanda cha bari na Nondo na kuna Mkubwa Mmoja ambaye Yule Serikalini"
" Mkubwa gani?"
" Kwamba humjui au unanichora? Kwani wewe Muda ule ulikuwa unazungumza naye Jambo gani"
"Siwezi fuatilia mambo ya wanawake bro! Kwamba nijue wanaume wake wote ama!"
" Kufuatilia ni muhimu kijana. Unaweza kujikuta kwenye mdomo wa Anaconda. Wanawake wengine ni lango la kuzimu "
" Unamaana gani?" Nikamuuliza mara hii nikiwa nimevutiwa na mazungumzo yak. Huku upepo ukiwa kikwazo cha mawasiliano yetu kutokana na upepo uliokuwa unapiga masikioni.
" Maana yangu ni kuwa, hata Wanyama porini wanapowinda huangalia mnyama anayemuwinda nani na nani wanamkodolea macho. Fikiria wewe ni mbwa mwitu unawinda digidigi alafu kumbe huyohuyo digidigi kuna Chui na Simba wanamvizia. Unafikiri Usalama wako utakuwaje?"
" Utakuwa mashakani!"
" Ndio hivyo kuwa Makini"
" Huyo Mkubwa serikalini ni Nani?"
" Mimi sitakutajia, ila mji mzima pale unamjua. Sasa ni ajabu wewe kusema humjui. Ukirudi fuatilia haitachukua Muda mrefu utamjua"
Akasema, kisha akakaa Kimya. Kitambo kidogo kukawa Kimya nikijaribu kutafakari uzito wa habari Ile.
" Kwa hiyo ni kweli unamfukuzia Yule mwanamke muuguzi"
" Hapana!" Nikamjibu kwa kifupi.
" Vizuri! Mwenyewe ningekushauri Ukae naye Mbali Sana Yule Demu. Ni Hatari kwako"

Ukimya kidogo ukapita. Sikutaka kuendelea na hiyo Mada. Baada ya dakika Mbili hivi ambapo kwa Mbali kama kilometa tano mji wa Msata tulianza kuuona nikamuuliza;
" Unaamini Yule mwanamke alizaa Panya?" Hapo nikawa namtazama usoni kupitia kwenye Kioo cha pikipiki. Nikamwona akiingiwa na kihoro, bado hakujua namtazama kupitia kwenye Kioo. Akashtuka macho yake yalipogongana na macho yangu kwenye Kioo na kugundua nilikuwa nikimtazama.
Nikamwambia,
" Binadamu hawezi kuzaa Panya bhana! Hizo ni fix tuu"
" Mimi katika Hilo Sina chakuchangia. Sio Mtaalamu wa mambo hayo" akasema.
" lakini wewe kwa akili yako unaamini mtu anaweza kuzaa Panya?" Nikamuuliza.
" Nimesema sijui! Wewe unaamini Uchawi upo au haupo?" Akanitupia swali. Hapo nikarudisha macho yangu kwenye Kioo tena kumtazama, nikamwona akiniangalia, alafu akaniuliza Akiwa anatabasamu " Uchawi upo au haupo?"
" Mimi sijui" nikamjibu.
" Ndio hivyo. Mambo mengine ni magumu Sana kuyaeleza hasa ukiwa huyaelewi" akasema.
Tayari tulikuwa tumefika Msata. Akanishukuru na kunipa Kiasi cha shilingi elfu thelasini.
**************

Ulikuwa usiku wenye furaha Sana kwangu. Siku hiyo nilikuwa nimeenda kwa Cathy kama alivyonitaka niende kwake nilifanya hivyo.
Cathy alinisamehe lakini alinipa sharti Moja kuwa hataki niwe na mwanamke mwingine. Zaidi akanipiga Marufuku kukutana na Bihawa.

" D nimekusamehe. Nataka uwe Mume wangu tena wa Peke yangu. Unajua vile ninavyojisikia kuwa na wewe. Nakupenda Sana. Nahisi kama nitaua mtu hivi. D sio utani. Mimi nina Wivu mbaya nakuambia"
Cathy alikuwa akiongea huku macho yake yakiwa machoni mwangu.
" Yule Mama Ntilie achana naye. Alafu nawe mwanaume mzuri unatokaje na mwanamke mama Ntilie kama Yule? Mbona unajidhalilisha hivyo D.
Tena nasikia mwanamke mwenye anamtoto. Hivi D kweli wewe ni wakuwa na mwanamke mwenye mtoto?"
Cathy alisema huku akinitazama.
" Tatizo sio mtoto Cathy"
" Tatizo ni nini sasa Mpaka uwe na mwanamke mwenye mtoto. Kwani wengine wameisha?"
" Kwani Cathy kuwa na mtoto ni kosa? Mimi naona kwa vile tu...." Kabla sijamaliza akanikatisha.
" Oooh! Sio Kosa kumbe ndio maana upo naye. Unamtetea si ndivyo?"
"" Hapana Mpenzi. Sio kwamba namtetea. Hata hivyo Mimi nakupenda wewe mwenyewe. Ndio maana nipo hapa. Unajua vile ambavyo mioyo yetu ilivyoshikana. Hakuna wa kuitenganisha kipenzi"

" Unajua D ni watu wangapi wanakuja kutaka kunichumbia. Wengine wanapesa haswa wengine ni watu Wakubwa"
" Mimi sijui! Nachojua nakupenda Basi. Kama kuna wanaokufuata waambie mwenye Mali nipo"

Siku Ile tulifurahia Sana na ilikuwa ndio siku ya Kwanza kumjua Cathy. Alinipa yote. Cathy alikuwa mwanamke Mzuri Sana. Mbali na uzuri wake pia nilikuwa nampenda Sana.

Baada ya kufanya mapenzi. Tukaenda kuoga. Kisha tukarudi chumbani.
" D unajua wewe ni Mume wangu Mtarajiwa. Nataka uache Kazi ya ubodaboda"
" Niache ubodaboda? Alafu nifanye Kazi gani?"
" Unajua ubodaboda sio Kazi ya kujivunia. Alafu rafiki zangu watakuwa wakinitania na hawataniheshimu"
" Cathy! Unajua Kabisa siwezi kuacha Kazi ya ubodaboda kwani hata nikiacha Sina Kazi nyingine ambayo ninaweza kuifanya itakayoniingizia kipato. Alafu mimi sijaoa hao rafiki zako. Nimekuoa wewe. Kama watanidharau au kukudharau hiyo ni juu Yao. Mimi ilimradi Mkono uende kinywani"

" Hapana D. Bodaboda sio Kazi ya kujivunia. Kazi ya kukimbiza upepo hapana bhana! Alafu Mimi kukaa Roho juu kila siku siwezi. Pale hospital haziwezi kupita siku mbili lazima boss aletwe amepata ajali. Sitaki Mume wangu uwe kilema. Sitaki ufe ungali kijana kipenzi changu"
" Mmmh! Cathy .. unachoongea ninakielewa Kabisa lakini fahamu ajali hutokea mahali popote. Hata wewe unaweza Kupata ajali ingawaje hatuombei"

" D pale hospitalini asilimia kubwa ya wanaoletwa wamepata ajali ni bodaboda. Inaweza pita mwezi mzima mtu hata Mmoja ambaye sio bodaboda akaletwa pale lakini haijawahi kutokea zikapita siku mbili asiletwe bodaboda aliyevunjika mguu au maiti yake"

" So unataka nikiacha bodaboda nikae nyumbani! Unataka niwe Baba wa nyumbani. Hapana Cathy siwezi kuwa golikipa"
" Sijasema uwe golikipa au uwe Baba wa nyumbani. Ndio tutajadili hapa ufanye Kazi gani nyingine"
Nikakaa Kimya huku Cathy Akiwa anaendelea kuongeaongea. Cathy alikuwa mwanamke Mzuri lakini mwenye kupenda kuongeaongea yaani mwenye kisirani. Akiongea hivi hajatulia anaongea hiki. Hakuwa Yule mwanamke anayeweza kukaa Kimya.

" Mkataba wako umebaki Muda gani?" Akauliza.
" Mwezi Mmoja"
" Kheee! Mwezi Mmoja. Ama kweli siku zinakimbia. Unataka kuniambia miezi kumi na Moja imekatika..."
" Yeah! Hata hivyo naona kama siku haziendi. Natamani hata hizo siku zilizobaki ningekuwa na pesa ningempa Mzee Abeid pesa yake kisha nimiliki chombo" nikasema.

" Sasa naelewa kwa nini unang'ang'ania ubodaboda. Kumbe ni Kwa sababu umemaliza Mkataba"
"Wala sio hivyo. Ni kwa sababu ndio Kazi ninayoweza kuifanya kwa sasa"
" Kwani ukiwa na hiyo bodaboda huwezi kumpa kijana mwingine akawa anakuletea marejesho kila siku kama unavyompelekea Mzee Abeid. Alafu wewe ufanye Kazi nyingine?"

" Kazi nyingine ipi?"
" D kwamba hapa kiwangwa Kazi ni hiyohiyo bodaboda? Kuna biashara, Kuna Kilimo cha nanasi, unaweza fungua Duka la spea za vifaa vya pikipiki na Magari. Mbona Kazi zipo nyingi "
" Eeenhe! KAZI zipo nyingi kumbe! Cathy Kazi zipo nyingi lakini ishu ni Mtaji. Hivi unafikiri wale vijana pale wangekuwa na Mitaji wangefanya Ile Kazi?"
" Oooh! Now you talking! Kumbe hata wewe Kazi ya kufukuza upepo huipendi lakini tatizo ni Mtaji. Sasa si ungesema "
" Ningesema?"
" Ndio!"
" Kwa Nani? ili iweje?"
" Hahaha! Nataka nikupe mtaji. Unajua Mimi ni mtumishi wa serikali. Hapa nachukua Mkopo chapu nakupa pesa unaenda kupiga Kazi"

"': ngoja nimalizane Kwanza na kuchukua hiki chombo. Nikimaliza ndio nitawaza mambo mengine. Unajua nimeisotea Sana hii pikipiki. Miezi kumi na Moja sio lelemama"

" Kwani nikikupa Kiasi gani inatosha kumpa Yule Mzee Abeid kisha uchukue chombo?"
"' Laki tatu na nusu hivi Laki nne"
Nikasema huku nikimtazama Cathy usoni.
" Nipe Leo na Kesho nitakupa hiyo Pesa"
" KWELI!"
":Ndio hivyo tuombe Mungu."
Cathy akasema.

Usiku ule nililala kwa Cathy.
******
Kesho yake asubuhi nilienda kwa Mzee Abeid.
Nilimkuta nyumbani kwake akiwa Anasafisha Banda la Kuku.
" Shikamoo Mzee Abeid"
" Marhaba kijana hujambo!"
" Niko Salama Mzee wangu. Naona unaweka Sawa mazingira ya mifugo"
" Usafi muhimu kijana. Unajua Kuku ni kama watu. Bila Usafi watapata Magonjwa"
" Ni kweli Kabisa"
" Haya niambie Kijana kuna shida?"
" Hapana! Wala hakuna tatizo. Ila kuna Jambo nataka tuzungumze"
Mzee Abeid kusikia hivyo akaacha kufanya Usafi akawa ananitazama kwa umakini
" Jambo gani?"
" Aaah" nikaguguma, kisha nikakaa Kimya.
" Nakusikiliza kijana "
" Samahani Mzee wangu. Nilikuwa nauliza, hivi haiwezekani hizi siku zilizobakia tukapiga hesabu kisha nikakupa pesa yote?"

" Kwani zimebaki siku ngapi kijana?" Mzee Abeid aliuliza swali huku Uso wake ukijawa na hisia za hasira. Niliweza kuona hasira zake kupitia Toni ya Sauti yake.
" Zimebaki kama siku ishirini na Tisa hivi!"
" Siku ngapi?"
" Ishirini na Tisa Mzee wangu"
" Haiwezekani!"
" Nakuambia! Nilianza Kazi mwaka Jana mwezi wa kumi na Moja mwisho tarehe 29 Mpaka sasa ni miezi kumi na Moja na siku mbili"
" Heee! Siku zimekimbia Sana"
Mzee Abeid akaongea alafu uso wake akaupeleka chini akawa anapigapiga chini na fagio alilokuwa amelishika mkononi.
" Sawa kwa hiyo hizo siku ishirini na Tisa unataka unipe shilingi ngapi?"
" Ndio nimekuja Mzee wangu tupige hesabu"
" Dimoso unataka kuniambia umetoka nyumbani Mpaka hujapiga hizo hesabu? Embu Acha kunitania"
" Hahaha! Kama ni Kila siku ni elfu kumi kumi hiyo itamaanisha siku ishirini na Tisa itakuwa Laki mbili na tisini"
" Anhaa! Unazo hapo sasa hivi?"
Akaniuliza nikawa nababaika.
" Aah! Eee. Ndio zipo Nyumbani"
" Ooh! Kumbe! Inaonekana pikipiki yangu imekupa pesa nyingi Sana"
" Hapana Mzee Abeid. Ni juhudi tuu"
" Juhudi bila pikipiki yangu ingekufikisha wapi kijana. Kubali pikipiki yangu imekusaidia"
" Ni kweli Mzee wangu. Ila na juhudi zangu pia"
" Sawa! Sasa... Sasa. Aaah!" Mzee Abeid akasema huku akitafakari kipi aseme. Kisha akakohoa kusafisha Koo, kisha akasema;
" Nafikiri uendele kuleta hizohizo elfu kumi kwa hizo siku zilizobakia kama mkataba unavyosema, hiyo Laki mbili na tisini unaweza fanyia mambo mengine"
Maneno hayo yalinikata Moto. Nikabaki namtazama bila kusema kitu.
" Kwani unaharaka gani Dimoso? Umeweza kufanya Kazi miezi kumi na Moja huwezi shindwa kumaliza hizo siku ishirini na Tisa"
Akasema. Nikamwambia Sawa huku nikiwa nawasha pikipiki yangu nakuondoka.

Kabla sijafika Mbali nikasikia akiniita. Nikasimama;
" Ukinipa Laki tatu na nusu nakukabidhi chombo hata Leoleo" Mzee Abeid akasema,
" KWELI?"
" Niamini!" Akanijibu.
" Sawa Kesho asubuhi nakuletea hiyo pesa" nikaondoka nikiwa nimemuacha Mzee Abeid akinisindikiza na macho. Nilimuona kupitia kioo cha pikipiki.

Jioni ilifika, akaja kijana Mmoja pale kijiweni, Moja Kwa Moja alinifuata Mimi, akaniambia nimpeleke Bagamoyo, ilikuwa jioni Sana. Siku hiyo nilitaka niwahi nyumbani nipumzike kutokana na kuchoka kwa mishemishe za mchana. Kwenda Bagamoyo ni Mbali lakini pia hela yake ni nzuri. Kwema na kurudi ingenichukua masaa matatu Mpaka manne kwa mwendo wa kawaida.
Sikutaka Kumchukua Yule mwanaume hivyo nilijikuta namtajia pesa kubwa ili akatae lakini cha ajabu akakubali.
Aliniambia kuna kazi ameitiwa Bagamoyo, kuna Wazungu wametoka Austria wamekuja Bongo kwa project Fulani ambayo hakutaka kunitajia.

Pesa niliyomtajia ilikuwa maratatu ya pesa ya nauli ya kawaida. Sikuwa na chaguo.
Nikampakiza kisha safari ikaanza.
Tayari Giza lilikuwa limeshaingia Muda ulikuwa ni saa moja kuelekea saa mbili usiku nilikuwa nimeshapita mji wa Makurunge.
Wakati tupo njiani Yule mwanaume akaniomba tusimame ili avute sigara kidogo kwani alihisi kiu ya kuvuta.
Nikamwambia Muda unaenda akaniambia ataongeza pesa kidogo. Aliponiona nikamshika akatoa elfu sabini na kunikabidhi.
Kisha akatoa sigara yake akaanza kuvuta.

Muda huo nimesimamisha pikipiki pembeni ya barabara. Na tulikuwa katikati ya pori dogo ambapo hakukuwa na makazi ya watu karibu.

Yule mtu alikuwa akinisemesha kama Mtu anayehitaji kupiga Stori lakini Mimi sikuhitaji mazoea Sana. Nilikuwa nimechoka. Nilichokuwa nataka Muda huo ilikuwa niwahi kurudi nyumbani.

Ghafla Yule mtu akanitolea Kisu;
Wakati huo nilikuwa juu ya pikipiki yeye alikuwa amenikaribia Sana hivyo sikuwa na ujanja wa kufanya lolote.
" Unataka nini Bro?" Nilijikuta namuuliza swali nikiwa nimejawa na Hofu.
" Hahaha! " Akacheka!
Akili yangu ilinikumbusha kuhusu lile tukio la wizi wa mtoto Kule shamba la nanasi la PF55. Nilifikiri huenda watu wale walifuatilia na kujua aliyekuwa amekimbia siku Ile wakagundua ni Mimi.

" Bro tafadhali usiniue"
" Nataka nikuue"
" Kwa nini?" Nikamuuliza swali ili kumpotezea Muda.
Hakunijibu, akavuta sigara pafu Mbili. Nikaona hiyo ndio Nafasi ya kukabiliana naye.
Nimrukia kwa nguvu kisha wote tukadondoka chini lakini yeye bado alikuwa ameshikilia kisu mkononi. Pikipiki nayo ilikuwa imedondoka.
Kukurukakara zikaendelea, nijitahidi kwa uwezo wangu wote kupigana na Yule mwanaume ambaye sikujua alikuwa anataka kuniua kwa Sababu gani.

Akanichoma Kisu cha bega. Nilihisi maumivu makali Sana lakini nikajikaza, nikampiga kichwa kwa nguvu akapagawa. Yeye alikuwa juu yangu Mimi chini yake. Akaking'ofoa kile Kisu kwenye bega langu nikapiga kelele lakini nikamsukuma kwa nguvu akaangukia upande wa Pili. Nikaamka nikiwa nataka kukimbia akanipiga ngwala nikaangukia Uso. Nikagugumia. Akawa ananivuta mguu nami nikawa najilazimisha kujikokota kumkimbia. Akanichoma Kisu kingine cha mguu nikapiga yote la maumivu. Kwa bahati nilikuwa karibu na Jiwe nikamtupia likampiga kichwani akaanguka chini. Nikakitoa kile Kisu kwenye mguu wangu. Damu zilikuwa zinatoka nyingi.

Yule mwanaume akanyanyuka, wakati huu alikuwa ameshika Kisu kingine hiki kilikuwa kifupi ambacho kilikuwa cha kukunja na vijikisu vingine vidogovidogo, akanisogelea kisha alipokuwa akiinama kunifuata pale chini nikampiga Teke la kidevu, akapiga yowe kama beberu lakini lile teke halikumtosha. Akanifuata pale chini kisha akanikaba shingoni Akiwa ananiletea Kisu shingoni kunichoma. Chwaaa! Kisu kikaingia.

Sauti ya kelele inasikika!

Itaendelea;

• Je Dimoso atachomoa au ndio safari yake ya mwisho ndio imefika?
• Kwa nini huyu mwanaume anataka kumuua Dimoso?

Usikose sehemu ya tano

Mwandishi

Upo kimya sana Mkuu!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom