Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,167
- 14,467
Hapana shaka kabisa Zanzibar imejibebea sifa nyingi hapa ndani katika jamhuri ya Muungano na nje ya nchi pia.
Na imebeba historia kubwa ya mambo ambayo inawafanya wageni kutoka mataifa mbali mbali kwende kutembea huko na kujionea utajiri wa historia wa mambo ya Kale.
Bila kusahau ukarimu wa Wazanzibar ambao kwa miaka mingi sana wamekuwa wakiishi kwa upendo na mapenzi kwa jamii nyingine.
Inasemwa huko zamani kabla ya watanzania bara hawajaanza kwenda huko kwa wingi, ilikuwa si jambo la ajabu kuacha au kusahau mali yako Sehemu na ukaikuta salama salimini, kwani hakika wanzazibar ni watu wenye imani kubwa na hofu ya Mungu ambayo imewajenga kuwa na imani pamoja na huruma.
Lakini baada ya ujio wa sisi wabara nasikia mambo yakabadilika, ustaarabu kwa kiasi kikubwa ukatoweka, uaminifu ukaisha na janja janja nyingi ikaingia huko, na ikawa sio zanzibar ile tena tunayoijua.
Pamoja na yote hayo bado zanzibar ina miiko yake na tamaduni zake ambazo bado wakazi wa huko wanajivunia nazo,na hiyo ndio asili yao.
Nakumbuka hivi karibuni kulizuka maneno mengi kuhusiana na wamasai kutotakiwa kutembea na silaha za jadi, watu walisema mengi sana juu ya Zanzibar. Swali linakuja je wazanzibar waache kufuata sheria zao kisa tu jamii fulani inaendeleza tamaduni zake?
Jibu hapana kila sehemu kuna sheria na taratibu zake, kinachopaswa kufanywa ni jamii hiyo inapoingia mazingira mapya inatakiwa ifuate taratibu za huko na huo ndio uungwana, kisha baadae wakirudi wanapotoka basi waendeleze tamaduni zao.
Nakumbuka hata wazungu wakienda sehemu yoyote kutalii kwanza hujifunza tamaduni na desturi za eneo husika ili wasije kuwakwaza wenyeji wa huko. Na ndio wazungu wanaoenda zanzibar huwezi kuwakuta wanatembea na vikaptula vifupi kwakuwa wanajua huo usio utamaduni wa wazanzibar.
Wakazi wengi wa Zanzibar ni waislamu ambao miongoni mwa ibada zao kubwa ni kufunga mwezi wa Ramadhani, hii ni ibada kubwa si kwa wazanzibar tu bali kwa waislamu duniani kote.
Zanzibar imejiwekea utaratibu wa kutokula hovyo hadharani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na lengo ni jamii ipate kuheshimu ibada hii adhimu na muhimu sana katika dini ya kiislamu.
Lakini bahati mbaya sana kuna watu ambao kwa mitazamo yao hasi wanaona jamii nyingine isiyo ya kiislamu inatengwa na kubaguliwa huko zanzibar, kitu ambacho si kweli.
Watu hawa huanzisha choko choko ili mradi tu taswira ya zanzibar ipate kuchafuka huko duniani,,, Watanzania huu sio utamaduni wetu hata kidogo, tunajulikana kama kisiwa cha amani basi ebu tusianze kuharibu taswira yetu kama Taifa.
Siku zote mitafuruku yote iwe ya kisiasa au ya kidini huanza kidogo kidogo kama hivi na mwisho wa siku linakuwa bomu ambalo halitamchagua mzanzibar wala mtanganyika,sisi sote tutakuwa katika balaa kubwa.
Ombi langu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muainishe maeneo maalumu ambayo wale ambao sio waislamu wapate kwenda kula milo yao huko na wawe huru kwa hilo, na hata kama ipo kwa sasa basi iongezwe ili ikidhi mahitaji halisi, kwani inahuzunisha sana kila Ramadhani inapoingia kunawepo na kashfa kama hizi.
Natumaini kwa uwezo wa Allah subhanahu wataala atawawezesha kuliendea jambo hili kwa hekima na busara kubwa.
Asante
Ni hayo tu!