My Dear Ex Girlfriend

Pole sana Mkuu,nipe namba yake nikusaidie kufikisha ujumbe ili umfikie haraka
Salaam wakuu.

Mpenzi wangu najua mimi ndiye nilitaka tuachane na hii ilitokana na kupata binti mwingine.

Leo siku ya pasaka, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu nikuache, nazidi kukukumbuka kwa mengi. Hii imepelekea kujifunza mambo mengi ambayo kwa wakati unanifanyia nilikua nayaona kama mambo ya kawaida.

Ulikua na huruma na mimi, na hii ilijidhihirisha pale ambapo kwa kidogo nilichopata, ulisisitiza nikitumie vizuri. Nilikua nikikupa pesa iliyotokana na boom, ulikataa kiasi nilichokupa ijapokua haukua na mkopo.

Nilikukuta bikra na umri wa miaka yako 22 mwaka wa kwanza chuo, nakiri katika hili pia, ilionesha jinsi gani ulijiheshimu ilihali ulikua binti mrembo.

Upole wako, ulifanya hata nikikukosea unalia, unasali, unamwambia dada yangu, ananikaripia, nami nakuja kwako nakubembeleza, unatabasamu, nakubusu mashavuni tunafurahi uliwahi nikamata mara kadhaa na wasichana wengine, ukaniambia unanipenda sana, ukanisamehe.

Hata baada ya break up, ulinipigia simu nilivopata msiba wa baba yangu mlezi ukanitumia hela Tsh 5000, sitakaa nisahau, najua ulijinyima sana maana uchumi wako naujua. Ulifanya haya yote ingawa nilikutenda vibaya.

Suala ya kuachana na mimi haukuliafiki, hivo ulipata msongo mawazo uliopita kiasi hadi ukapata ajali ya moto.

Leo naamini usemi wa kiebrania na kigalatia usemao, "What goes around comes around" Leo hii sina amani katika mahusiano, naburuzika kama punda, huyu niliyenae tunaishi ila sio siri naburuzwa vilivyo. Nisamehe kwa yote.

Najua hatuwezi kurudiana tena, ila nimejifunza.

Ukipendwa pendeka.

Mgalatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom