kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,569
- 14,033
Ndoto ya Mwl. Nyerere kukubali vyama vingi vya siasa nchini ni kupata vyama viwili vikubwa vinavyokosoana, kuonyana na kuogopesha kisera katika kuitawala nchi. Hakupenda utitili wa vyama vidogovidogo visivyoweza kuikosoa na kuitikisa CCM katika kuzuia ukabila, umaskini, udini na rushwa.
Vyama vya upinzani na CCM lazima vizingatie maono haya ya Mwalimu kwa mustakabali wetu, watoto na wajukuu wetu; maana leo una madaraka lakini kesho huna, leo uko CCM lakini kesho uko upinzani au huna chama au leo uko upinzani lakini kesho uko CCM.
Ni upuuzi kufanya lisilo na faida au kukataa kufanya jambo lenye faida kwa taifa kwakuwa tu wewe leo uko na madaraka.