Mwizi alienasa toka jana usiku duka la Simu na TV anasuliwa

Mkuu wewe uko sahihi usemacho nilikosea kum-quote mleta uzi nkakukoti wewe,ukweli ni yakuwa video na maelezo ya mtoa uzi ni mama mkwe na mkwe wake hawawezi kukaliana zero distance.
 
HUYO MWENYE DUKA ANAWEZA AKAWA TAJIRI FAAASTA
kutongana na msururu wa watu watakaoutaka ulinzi huo...
YETU MACHO TU...
 
Nimeona hiyo video, inaonekana kabisa kuwa jamaa alikwama kwenye nondo; Inaonekana alipitisha miguu vizuri, lakini kwenye kupitisha "kiuno/hips" zikakwama, na akawa anashindwa kutoka pia, so akaona auchune hapo hadi asubuhi kwa usalama wake, maana angepiga kelele usiku huo, wananchi wangemmalizia hapo hapo.
Ndio maana kwenye hiyo video inaonekana wanakata hiyo nondo, ndio jamaa akaweza kuvutiwa kwa chini na askari (na sio mwenye duka), na akachomoka kirahisi (baada ya nondo kukatwa).
Lakini jinsi habari hii ilivyoripotiwa 'kikuda', ama kwa hakika bila ya video, watu wote watakaoisoma bila kuangalia video watajua ni ushirikina.
Watanzania tunapenda sana mambo ya shirki; Ni maajabu kwamba habari hii imeripotiwa na mtu aliekuwa eneo la tukio, tena akachukua video kabisa, lakini namna anayoripoti anatuaminisha kabisa kuwa mwizi amenaswa na 'sumaku ya asili'. Na watu wote waliokusanyika pale inaonekana wanaamini kabisa kuwa jamaa kanaswa kwa "sumaku ya asili". Wabongo katika ubora wetu. Ashura9 stephot Jaim Nyaka-One STUNTER CleverKING Mlandula Jr Inno laka charminglady SALOK 0716
 
Uko sawa kabisa mkuu,haya matukioya kishirikina mengi huwa ni ya kupangwa tu ili kuwavutia wale wenye imani nyepesi na Mungu,

Na hujipigia Pesa kiulaini tu kwa watu kutaka eti wapewe nao huo ulinzi.
 
Uko sawa kabisa mkuu,haya matukioya kishirikina mengi huwa ni ya kupangwa tu ili kuwavutia wale wenye imani nyepesi na Mungu,

Na hujipigia Pesa kiulaini tu kwa watu kutaka eti wapewe nao huo ulinzi.

Inaonekana mmiliki wa duka kaamua kutafuta mtaji wa kupanua duka lake kwa kutumia usanii huu. Si unaona duka lenyewe bado changa?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…