Aniko
JF-Expert Member
- Jan 3, 2016
- 1,766
- 960
Mkuu wewe uko sahihi usemacho nilikosea kum-quote mleta uzi nkakukoti wewe,ukweli ni yakuwa video na maelezo ya mtoa uzi ni mama mkwe na mkwe wake hawawezi kukaliana zero distance.Kwani mkuu ukiangalia kwenye video huoni kwa juu kuna mtu anakata grille kwa msumeno? Na anaemvuta chini mtuhumiwa siyo polisi? Kwa maana nyingine sijaona mtu mwingine tofauti ambaye anamshusha chini zaidi ya huyo askari. Na ndiyo sababu nikasema labda askari ndiye mmiliki wa duka au kama kweli mmiliki wa duka alimvuta hii haionekani kwenye video. Kulingana na maelezo ya awali iliandikwa mmiliki wa duka ndiye aliyemvuta. Lakini kwenye video haionyeshi hivyo.
Na usishangae katika tukio hili kunaweza kuwa na collusion inayowahusisha mwenye duka, mwizi na mganga ili kuwapata wafanyabiashara au watu wengine wanaohitaji ulinzi wa aina hiyo kwa kulipa fedha nyingi.