Mwinjilisti: Barua kwa Rais Magufuli, kwanini umejiandaa kumwaga damu za watanzania wasio na hatia?

Francis12 Leo kwenye uzinduzi wa ukuta kwenye machimbo ya Tanzanite, huko Mererani mkoa wa Manyara Rais Magufuli amemtambua rasmi mgunduzi wa madini hayo mzee Jumanne Ngoma na kutangaza serikali yake itampa millioni 100 !

Kwa mara ya kwanza mzee Jumanne Ngoma alitumiwa barua ya kutambuliwa na baba wa Taifa mwl Julius Nyerere mwaka 1967.

Awamu zilizofuata hazikuumiza kichwa kumtambua mzee huyu pamoja na kulalamika sana kuwa anaumwa na amepooza mguu hivyo kusitahili heshima yake kama mgunduzi namba moja wa madini ya Tanzanite.

Kwa hali hii mamillioni ya watanzania wanaendelea kutojutia kura zao kwa kumchagua Magufuli ambaye ni mcha Mungu na anapiga kazi kwelikweli kutatua kero za wananchi.

Kwa kasi hii kujifanya hauoni kasi ya Magufuli katika kutatua kero za wananchi na kujifanya wakala wa shetani ni kujitafutia vidonda vya tumbo bure na utashindwa na kulegea .
 
Francis12 Gazeti la Mchungaji Kasupa sikulisoma lote kwa kuwa ujumbe uliomo ni wa yale yale ya viongozi wa vyama vya upinzani:

1) Kudai demokrasia wakati ndani ya vyama vyao haishi kidemokrasia.

2) Kudai haki na uhuru wa kutoa mawazo wakati kila kukicha wanatumia vyombo vya habari kumkosoa na kumtukana Rais, na vyombo hivyo vinaendelea kuwasikia na kuandika pasipo kubughuziwa na Serikali.

Inashangaza wanaoikosoa Serikali kwa lugha chafu hawakemiwi na hao Watumishi wa Mungu!

Francis12, umeandika mengi tu dhidi ya Rais Magufuli, na wakati mwingine kwa lugha chafu, tarehe 26/4/2018 ingia barabarani uandamane, uoneshe ujasiri na uzalendo wako kwa nchi yako ambayo inaharibiwa na huyo mnayemwita dikteta.
 
Kule Kagera alipayuka-"huwezi kunijibu hivyo mimi!!"

Ninaamini atasoma halafu na kumalizia "huwezi niandikia hivyo mimi"

Anajiita jiwe-sjiwe - bila shaka alificha tu kusema yeye ni Jabari kuu na hajaribiwi!!

Utawala uliofitinika,HAKI HUINUA TAIFA ,Wao wtamechagua kuinua vibaraka na marafiki zao huku wakiangamiza Taifa.!!
Usinung'unike tu mitandaoni, fanya uamuzi wa kushiriki maandamano na siku hiyo upande jukwaani kusema yaliyo moyoni mwako.
 
Watu wanakufa wewe unasema dini na siasa tena!
Watu wangapi wanakufa kwa ajali barabarani hao watumishi wa Mungu hawasemi, au ni wamiliki wa hivyo vyombo vya usafiri?

Akina mama wazazi na watoto wanakufa wakati wa kutimiza wajibu wao wa kibindamu, Watumishi wa Mungu hawakemei, au wanahusika na kuwapa mimba!

Watoto wa shule wanapewa mimba na kuharibu mategemeo ya maisha ya, Watumishi wa Mungu kimya!

Kuna nini nyuma ya matamko na nyaraka zao hizo! AIBU TUPU
 
Mwaka huu ni mwaka wa nyaraka tu, jamani wasomaji tutasoma sana,
Maaskofu tayari, TEF tayari, Mwinjilisti tayari, .....

Ushauri wangu:

Mliobaki ombeni mkaonane na Rais Ikulu muongee naye ana kwa ana. Nadhani itasaidia zaidi.

Mbona wenzenu wanaomba appointment na wanaenda kumuona? Mf. Lowasa, wafanya biashara, wazungu wa ACACIA nk.
Hawa watu wa nyaraka wana lao jambo sio bure, kila mbinu watatumia na kudandia kila hoja, yaani mifano yooote aliyotoa ni kumuunga mkono mange kimambi! Nimemtoa maanani kabisa
 
Hawa watu wa nyaraka wana lao jambo sio bure, kila mbinu watatumia na kudandia kila hoja, yaani mifano yooote aliyotoa ni kumuunga mkono mange kimambi! Nimemtoa maanani kabisa

Hivi huko aliko Mange kuna amani? Au anadhani hatujui jinsi watu wanavyouliwa hovyo huko Marekani.

Watu wanamiliki silaha ovyo, wanauana na kuua watu wasio na hatia kama vile wanafunzi mashuleni.

Manyanyaso ya watu weusi hayajakomeshwa bado yanaendelea. Trump Rais wao mwenyewe kuwapiga marufuku waislam kukimbilia nchini mwake, je hizo ndio haki za binadamu?

Au tunafumba macho yetu makusudi ili kushabikia ujanja wake wa kuhamasisha maandamano huku yeye akiwa mbali?

Kwa nini asije ili awe mstari wa mbele siku hiyo?
 
Kwani hayo maandamano yataanzia wapi na kuelekea wapi? Halafu coordinator wa maandamano hayuko Tanzania Mwinjilisiti anafananisha hayo maandamano na yale ya 1966. Hapo hajataka kutumia akili yake vizuri kutofautisha. Sasa hivi ni kujenga nchi maendeleo kwanza hayo mengine badae.
 
Back
Top Bottom