Mwingine adakwa kwa kumkashifu Rais Magufuli kwenye mtandao wa "WhatsApp"

Kwani ukisema "Pombe" ndio umemaanisha mkaazi wa magogoni??

Ene wei, kuna wakati miaka ya zamani sana wanasayansi waliamini kuwa dunia iko kama meza na ilikuwa kosa la jinai kujinasibu na falsafa kinyume na hiyo.
Kuna scientist alinyongwa kwa kusema dunia ni umbo kama yai eti alipingana na mafundisho ya ukatoliki. Baadaye ikaonekana ni kweli mpaka leo dunia ni oval shaped
 
Hivi wakitaka kutudaka na sisi hapa jf wanaanzia kwa mods Kwanza ili wajue majina halisi, maana hapa Facebook twitter na whatsapp ndio wanadakwa sana ina maana humu watu wastaarabu sana?
JF full fake hakuna mwenye Jina Lake humu
We posti uone kama hawatakukamata fasta. Computer unayotumia au laptop itakuidentify tu, jina or nickname.
 
Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais kwenye mtandao wa WhatsApp.

Hapa cha muhimu ni kujuwa sheria hii inafanya kazi, inakamata, inahukumu na kufunga wananchi. Tutumie lugha ya staha, vijana hamko salama kwenye fb, twitter na WhatsApp...sheria ya mitandao ipo na inazunguka kama Simba aungurumae akitafuta mawindo.
Sheria zipo na zinafanya kazi usiku na mchana,
 

Mkuu unashanga nini ,ndivyo elimu inavyostahili. Mpaka sasa ni watuhumiwa na unaweza kuta bila kufahamu uhalisia au mantiki ya maneno maana mazingira ya maisha yako tofauti sana hivyo watu huyatumia maneno kwa mazoea ya mazingira yao.
 
Jaman kuandika jina au kutoandika haisaidii kujificha kama utaenda mrama na kwenye ujumbe wa kukashifu au kutukana tukifanya ufuatiliaji wa sms zetu tunaona kila kitu kuhusu usajili wa namba cha msingi tujitahidi kuandika kiungwana na kama una hasira tulia kwanza pamoja tuzingatie sheria hata kama zinatubana tumezipitisha na Zina fanya kazi
Hakuna mtu mwenye majina ya humu. Ila kwa vile sheria ipo basi pamoja na kuwa ni kandamizi we need to careful
 
Hivi wakitaka kutudaka na sisi hapa jf wanaanzia kwa mods Kwanza ili wajue majina halisi, maana hapa Facebook twitter na whatsapp ndio wanadakwa sana ina maana humu watu wastaarabu sana?
JF full fake hakuna mwenye Jina Lake humu
Wanaweza kukutrack ıngawa ınachukua mda zaıdı y whatssapp na fb
 
Hivi hiyo sheria ni kwa wanaomdhihaki JPM pekee? Mbona tunashuhudia wanasiasa na watu wakawaida wengi tuu wakitukanwa lakini hakuna hata zinachukuliwa? Nani hajaona matusi anayopewa Eddo mitandaoni na watu wanaofahamika? Mbowe, Slaa, Nape nk?
Kumbe ilitungwa kwa ajili ya mtu mmoja tuu
Waathirika waende kushitaki tu. Huenda hawa wasioshitaki hujifanya wanangozi ngumu na wanastahimili. Sheria ipo kwa wasiostahimili huu uchafu.
Hata wanawake wa kikurya huwa hawashitaki waume zao kwa kuendeleza mila. Hivyo hivyo chadema na watu wao huwa hawashitaki kwa sababu kutoa matusi ni mila yao.
 
kwa wale mnaozani kutumia term pombe utakwepa shitaka jifikirieni tena. huo ujumbe umetumwa watsup na watu walijadili so hapo lazima tafsiri ya nani linamhusu imeshajitokeza. Context inamfunga mtu. tuwe makini. kama atasema wamemuelewa vibaya then alitakiwa kuclarify kwa wanaochat nae. la sivyo, anakalia debe.
 
1466506495237.jpg
 
Haya makundi ya WhatsApp kuna "nyoka" kibao wamesambazwa....Cha muhimu ni kuwa makini sana sana
Unaweza dhani upo na Classamates mnakumbushana enzi za ShyBush na ShyCom au Enzi za Kazima na Uyui kwa Mzee Patel au Tabora Boys (Berlin) na Tabora Girls (Warsaw) au enzi za JKT Maramba na bogi la JKT Mafinga kumbe upo na "nyoka" wanatafuta "wateja" ili kazi yao ionekane imetendeka.

Kwa sasa hatuko salama,tunarudi enzi za Mwalimu,mpaka mke ndani ya nyumba unamuogopa,jirani yoyote "usalama wa Taifa".Tutaanza kuogopa mpaka wasafisha maofisi wa kampuni za usafi...Maana wengi wanawekwa kusikia mwenhe kaya anasemwaje humo maofisini

Mnapokuwa na Kiongozi ambaye si mwanasiasa,lazima mjiandae kwa yote..Hakuna kurembaremba
 
Hivi wakitaka kutudaka na sisi hapa jf wanaanzia kwa mods Kwanza ili wajue majina halisi, maana hapa Facebook twitter na whatsapp ndio wanadakwa sana ina maana humu watu wastaarabu sana?
JF full fake hakuna mwenye Jina Lake humu
Identity ya chombo unachokitumia inajulikana take care
 
Kuwa anonymus ni ghali kidogo, unaweza kufanya mambo haya na ukatukana kila tusi bila kukamatwa ila si kazi rahisi so kama unatukana na una maslahi na huko kutukana jitahidi kulipa gharama za kuwa anonymus ambazo ni kubwa kiasi flani!!
 
Back
Top Bottom