Kwa sasa mna agenda ya ati kuongezeka kwa 'utekwaji watu', wakati mnajua ni uhalifu kama uhalifu mwingine! Mnataka hilo lipewe kipaumbele katika kujadiliwa badala ya bajeti kweli! Au kuna Wabunge wana agenda ya kisiasa dhidi ya maendeleo yetu!
Juzi tu mlilishikia bango kubwa suala la RC Makonda kuwaambia ukweli kwamba hamtimizi wajibu wenu. Baadhi yenu: husinzia wakati wa mijadala; hususia vikao; hawahudhurii vikao; hutumia lugha isiyo staha; nk.
Linapokuja suala linalogusa maslahi yenu mnaling'ang'ania kama ruba kulifanikisha.
Kuna matendo ya uhalifu mkubwa hakuna hata mmoja wenu anaguswa kupeleka hoja binafsi bungeni km kuongeezeka kwa wachungaji wanaopotosha jamii kwa mafundisho ya kitapeli na uchochezi; mauaji ya wananchi kimila sehemu kama Mkoa wa Mara; ugomvi wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji; biashara ya madawa ya kulevya; mmonyoko wa maadili nk. Masuala hayo, na mengine ya aina hiyo, mkiyapa kipaumbele kama maslahi yenu, hata kama ni wakati wa kipindi cha maswali na majibu, tungeukubali na kuheshimu uwakilishi wenu.
MTAFAKARI CHUKUENI HATUA, WAKATI NDIO HUU