Mwigulu amewaagiza Wataalamu wa Wizara yake kukaa na Wajumbe wa IMF wajadili Athari za Upungufu wa US Dollar kwenye Uchumi!

Waziri wa Fedha Dr Mwigullu Nchemba PhD amewaagiza Wataalamu wa Wizara yake kukaa na Ujumbe wa IMF wajadili Athari za Upungufu wa US Dollar kwenye Uchumi wa nchi

Dr Mwigullu amewataka Wataalamu hao kujadili namna ya kushughulikia Upungufu wa mzunguko wa Dollar ya Marekani Ili kunusuru Uchumi

Source: Ayo tv
Mods unganisha huu uzi
 
Mtumie rubo na yuan Sasa si kila siku mnatamba kuipoteza us dollar mnaitafuta ya nn?

Wenye akili wanatest mitambo kwanza kupima upepo wa sarafu nyingine ikiwa dollar kweli ita disappear
 
Dawa ni kujiunga na BRICS ili kuendeleza mpambano wa Dedollarisation. Inawezekana sasa hivi tunafanya biashara kubwa zaidi na nchi za Brics kuliko timu mkoloni, kwa nini tuendelee kulialia kuhusu dollar?
Achana na dollar, tulipane kwa local currency kama tunavyofanya na India.
Hakuna tofauti yoyote hapo yote ni mabeberu tu hayo, labda ungesema mfanye biashara wenyewe wa Africa
 
Yaani Serikali inakopa hadi aibu.

Spika Dugai alikuwa sahihi sana.
Iko siku hii nchi itauzwa.

Kipande kimoja cha Ardhi Kishauzwa kwa Nchi ya Zanzibari.
 
Chifu,

Kama DEMAND can't meet Supply ndo SHORTAGE yenyewe hiyo!! Nchi nyingi za Afrika mara zote tumekuwa ni wa kununua zaidi kuliko kuuza na kwahiyo kama issue ingekuwa ni trade imbalance basi US Dollar zingekuwepo kwenye mzunguko lakini exchange rate ingekuwa kubwa!!

Of course, zipo sababu kadhaa zinazoweza kupelekea hiyo situation including hilo suala la trade imbalance lakini kinachoendelea sasa ni zaidi ya trade imbalance!!

Btw, Hiyo ni Egypt, na vp kuhusu hizo nchi zingine nilizokuwekea?! Au all of sudden nchi kadhaa za Afrika zimekuwa na more demand for USD?

Kila nchi inaweza kuwa na sababu yake iliyopelekea hiyo shortage lakini kwa upande mwingine Mahasimu wa USA wanapambana wakijaribu kufanya De-Dollarization... kwamba, wanajaribu kuipoteza US Dollar especially kwenye cross-border trade settlement.

Mchina anatumia kaulimbiu nyepesi tu kueleweka "getting rid of weaponized US Dollar"!! Sasa hapo unaachaje kumvuta Urusi, Iran, Venezuela, na wengineo?

Kwa mfano, ili kufikia de-dollarization, taarifa zinasema China's Central Bank imefanya currency swap agreement na zaidi ya nchi 40 duniani, yenye thamani ya YUAN 4 TRILLION, ambayo ni more than USD 580 BILLION! Sio hivyo tu, Mchina kafungua hadi Yuan based Clearing Banks kwenye nchi 29.

Kwa asiyefahamu, hizi clearing bank zina-act kama bridge kati benki mbalimbali duniani!

Aidha China amefanya similar agreement na nchi za BRICS ambazo ni Brazil, Russia, India, China na South Afrika! Sasa hivi block kama hiyo inafanya biashara ya Dollar bilioni ngapi miongoni mwao?

Hapo kabla, kufanya trade settlement miongoni mwao wangelazimika kutumia US Dollar lakini kwa makubaliano hayo, hawatakuwa tena na sababu ya kutumia dollar!!

Habari zinasema hata Saudi Arabia, Kuwait, UAE, Oman ni suala la muda tu kabla hawajaingia mkataba na Uchina uitakaowezesha cross-border trade kati yao amaifanyike kwa Yuan au kwa local currencies!

Mchina mjanja sana, anafahamu nchi nyingi zitakuwa comfortable kuingia makubaliano ya kutumia local currency lakini kwa ukubwa wa biashara za China, ni Yuan ndie ataibuka kidedea!!

Sasa kwa mazingira kama hayo unatarajia nini?! Mosi, demand for USD itapungua. Na USA wakiona demand ya USD ipo kwenye hatihati lazima watadhibiti supply yake kwa hofu isije kuporomoka thamani! Sio hivyo tu, nchi kadhaa hatimae zitaweka udhbiti kwenye foreign reserves ambayo inakuwa in USD na hivyo kuendelea ku-create dollar shortage!
Well I can’t argue with that, nonetheless from that viewpoint somewhat you agree; crucial to shortage is internal economics fuelled by trade deficit.

Hela ipo sokoni sema mabank wanaogopa current libor, na hizo nchi pia zimejikita kulinda thamani ya sarafu zao kushinda kuitafuta dollar.

Hao wengine najua ukienda kupekua utakutana na same stories, internal economics for the most lakini US aijazuia dollar kupatikana; ipo ila not cheap kwa sababu ya higher interest rate.
 
Biggest sources za usd ni tourists na gold sales

Je kuna upungufu wa watalii? Hapana
Je kuna upungufu wa gold? Hapana

What’s happening then!
Wakenya wamekuja kununua?
Tunalipa mikopo!
Tunalipia ndege na miradi!
Au tunatengeneza crisis ili tuje na solution ya upigaji

Tuendelee Kula Mtori Nyama zipo tu
 
Jamani Mwigulu sio Mtaalamu wa fedha ?, Mbona Analia Lia ?,mbona anataka wataalum wakae ? Au PhD yake ni ya mchongo ?
 
Pendelea zaidi kusikiliza kuliko kusikilizwa.View attachment 2643969
Mzee, uchumi wa hizo G7 ni sinusoidal na benchmark yao ni UTAJIRI sio!

Nani kati ya hao G7 au G20 wenye bajeti ya kutegemea wahisani?

Sasa wewe uwe kwenye dimbwi la umasikini halafu uzungumzie uchumi kuyumba? Uchumi upi?

60 good yrs ya kuwa huru, fananisha na 60yrs ya nchi yeyote kwenye hizo G7/G20 kimaendeleo ya uchumi, tupime huo ukuaji wa uchumi ili tuone kama DEFINITION ya uchumi ndio hiyo hiyo!
 
Umeambiwa duniani uchumi umeporomoka au umeambiwa duniani Dola imeadimika?! Yaani unashindwa kuelewa sentensi yenye maneno yasiyofika hata 10 halafu bado unaona wenzako vilaza!!
Pitia heading kisha jaribu kusoma soma comment za watu humu, kama hawazungumzii kuadimika kwa dollar au yafananayo, kataa kuwa KILAZA!
 
Back
Top Bottom