Mwenzenu nimegundua siri kubwa ya mafanikio ni ubahili

Kufanikiwa kuna masharti yake moja ya sharti kubwa ni KAFARA.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia mia, mwenyewe nlijifanya bahili mpaka jana nimeenda kudipositi vilaki vitatu nlipochungulia kibubu nkakuta kina milioni nne na laki moja....akiba muhimu kuwekwa
 
Maisha hayampangii mtu namna ya kujiendesha bali mtu anayapanga maisha yaendeje baada ya kukaa mda mrefu nimegundua nilikuwa mjinga sana nimechelewa mno kwa kutokuweza kuyatawala maisha lakini sasa nimejifunza nahisi sitorudia kosa.

Nilichogundua ili kufanikiwa lazima uwe bahili sana, unatakiwa ujinyime sana, kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, kufanya mambo ya lazima na muhimu kutotumia pesa kufanyia kitu kisicho cha lazima.

Pili ili pesa zikae jaribu kutokutafuta sifa za kijinga kama kufanya kitu kwa kutumia pesa ili uonekane unazo hapo utakuwa umepotea kabisa, ni vyema uonekane huna pesa kumbe unazo utajikuta mambo yako yanaenda vizuri.

Ogopa sana kukopa pesa zisizo na ulazima, pale unapobanwa jaribu kuvumilia changamoto unazokumbanazo

Ili kushinda yote hayo jiwekee malengo katika pesa unazopata kila mwezi au kila siku jipangie kiasi cha kuweka akiba hata kama akiba ndogo we weka na hakikisha kila mwezi unafikisha kiasi ulichojiwekea. Kama mwezi mwingine utapata na matatizo usipofikisha kile kiasi hakikisha unaongeza kiasi kwa miez ijayo ili kufidia kiasi kilichopotea.

Mafanikio yanakuja kwa kuweka akiba na kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, hayo yote yatawezekana ukiwa bahili wa kutupwa.

Kitu kikubwa kinachochangia umasikini ni kujihusisha na michango hata kwa wale wasio karibu na wewe!

Michango ya harusi, misiba, kipaimara, komunyo ya kwanza, mahafali, ...mwisho wa siku unashindwa kujiwekea akiba hata ya kufanya mambo ya kimaendeleo.
 
Kuwa bahili halaf hakuna uwekezaji sana na bure bora uendelee kuzitumbua tu
 
Tumia PESA ikuzoee... Haya maneno yana maan kubwa watu hawajui tu yule Mzee aliyechimba shimo ndani ya nyumba kumbe eneo ni la barabara yaliyompata ndio ya kujifunza sasa. Ubahili wa kikuda hauna tija.!
 
Saving pekee haitengenezi utajiri bali ivestment ndo inayo tengeneza pesa. Ku hifadhi pesa benki ni uoga. pesa inatakiwa ifanye kazi.
unaweza bana matumizi sawa ila kama hizo pesa hazielekezwi kwenye uwekezaji basi hakuna kitu hapo
 
Maisha hayampangii mtu namna ya kujiendesha bali mtu anayapanga maisha yaendeje baada ya kukaa mda mrefu nimegundua nilikuwa mjinga sana nimechelewa mno kwa kutokuweza kuyatawala maisha lakini sasa nimejifunza nahisi sitorudia kosa.

Nilichogundua ili kufanikiwa lazima uwe bahili sana, unatakiwa ujinyime sana, kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, kufanya mambo ya lazima na muhimu kutotumia pesa kufanyia kitu kisicho cha lazima.

Pili ili pesa zikae jaribu kutokutafuta sifa za kijinga kama kufanya kitu kwa kutumia pesa ili uonekane unazo hapo utakuwa umepotea kabisa, ni vyema uonekane huna pesa kumbe unazo utajikuta mambo yako yanaenda vizuri.

Ogopa sana kukopa pesa zisizo na ulazima, pale unapobanwa jaribu kuvumilia changamoto unazokumbanazo

Ili kushinda yote hayo jiwekee malengo katika pesa unazopata kila mwezi au kila siku jipangie kiasi cha kuweka akiba hata kama akiba ndogo we weka na hakikisha kila mwezi unafikisha kiasi ulichojiwekea. Kama mwezi mwingine utapata na matatizo usipofikisha kile kiasi hakikisha unaongeza kiasi kwa miez ijayo ili kufidia kiasi kilichopotea.

Mafanikio yanakuja kwa kuweka akiba na kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, hayo yote yatawezekana ukiwa bahili wa kutupwa.
You are collect
 
Back
Top Bottom