Mwenza wa ndoto yako

Mbona kama ulikurupuka kumvisha pete?
Au ulishinikizwa?
No ilipita miaka kama mitatu kabla ya ndoa nikijizungusha lakini jamaa aliendelea kukomaa na mimi nikaona isiwe taabu lakini matokeo ndo hayo mamito nimeshindwa kujifunza kupenda huenda nae anakata tamaa lakini hayuko tayari kuniacha niende zangu na visa navyo haachi yaani tafrani tu mkuu.
 
Mimi sio k'vile ila nafarijika napomuona maana nimebahatika kuoa mwanamke mzuri sana sema kinachosumbua hua ni kipato tu ukichanganya na hali ya Magufuli...

Ila pole sana kwa mkasa huo ila naungana na wenzangu hapo juu kua kinachowasumbua ni saikologia.

Pili mwanamke hata kama anakupenda ni wachache wanaoanza kukuonesha kua anakupenda mpaka uanze wewe.

Sasa na unavojifanya hujui kubembeleza ndio unaharibu kabisaaaaaaa....
 
Baada ya kuachana alibadilika mno na kuwa kicheche kwa vile wengi walitufahamu so nilikuwa napigiwa na kuniambia hadi sasa hajaweza kudumu na mke ni majanga mwendo wa kubadili wanawake. Wakimuuliza hao rafiki zake anadai mwanamke alikuwa ameweza kumfanya atulie ni mmoja tu yaani mimi wakiweza wampelekee ila mi sipo huko kabisa na wazazi wangu hawataki hata kusikia.
Sometime life style yako nzur nmeipend mno.
 
Mmh!, kweli nimeamini ndoa ni mpango wa Mungu. Inaonesha kabisa kulikua hakuna hata dalili ya upendo tangu mwanzo kabla ya ndoa ila nyie mkalazimisha.

Sijui niseme ni pigo au ni mapito mnayapita maana aieleweki.

Ila tu naona kilichobaki ni kumliloa Mungu aweze mpatanishi wenu.
 
Habarini za usiku wakuu.

Wakati wa Ujana kuna zile ndoto huwa tunakuwa nazo juu ya wenza tunaotaka kuwa nao maishani iwe kwa Msichana au Mvulana.

Lakini katika Safari hiyo ndefu ya kuelekea ukubwani tunapitia changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine huzima ndoto zetu na kujikuta tunaingia katika mahusiano na watu ambao siyo wa mioyo yetu kwa kurubuniwa na mazingira mbalimbali.

Binafsi nilitaraji kupata mwenza mchangamfu, rafiki, anayenifanya nitabasamu muda wote, anayejua nafasi yake katika familia, anayejua nimekula nini au nafanya nini yaani kifupi mtu anayajali na kutengeneza mahusiano rafiki, muwazi wa hisia na mjasiri. Kuhusu muonekano hapo naweka kapuni.

Wakati fulani katika maisha nilipata wa hivyo tunaefanana tabia tukafurahia mahusiano hadi ndugu na marafiki zetu walitupenda na tulikuwa na furaha tele kila mtu alipendwa kwa mwenzake coz hata muonekano wetu tulikuwa tunaendana sote majiyakunde yeye mrefu mi mfupi. Maisha yakabadilika kutokana na umbali akanisaliti kwa mtu wa jirani yetu sikuweza kusamehe nikajitenga nae ingawa aliniomba sana nimsamehe lakini moyo ulikataa na nikausikiliza. Akawa kama mwehu alitangatanga na wapenzi wa kila rika mi nilitulia kwa vile sipendi tabia ya kubadilisha wapenzi nilijipa muda isitoshe nilikuwa mbali nae.

Baada ya mwaka kupita nikaona nipate wangu cha ajabu macho yakakataa kuona wengi nikaona mmoja akajionesha kama ana utu ila alikuwa tofauti na vigezo vyangu nilimweka wazi kwamba hanivutii akanimbia naweza kujifunza kupenda sikumpa jibu akaniseduce vya kutosha ikabidi nifungue moyo. Cha ajabu tangu ndoa day one hadi leo zaidi ya miaka saba sijawahi kuwa na furaha nae.
Kila mtu kivyake tukutane kitandani furaha kwa nadra na wala sichepuki akisafiri anaweza wapigia simu wengine ila mi hata akae miezi mitatu hapigi simu na wala simpigii au kumlaumu kwani hata akinipigia sauti yake hainisisimui hivyo nachukia , kukiwa na lolote namtumia text mesage akijisikia atajibu. Hata akiwa online WhatsApp hatuwezi kuchati nae hata nikimtumia sms hajibu hadi siku akirudi ndo tuonane. Imekuwa ndiyo mfumo wa maisha yetu na Kuzima ndoto ya Maisha ya furaha niliyokuwa nayo na niliyolelewa.

Mara nyingi napenda kukaa peke yangu sipendi kelele na hata sipendi kupiga simu ndugu na marafiki wananilaumu, sipendi kwenda kwenye starehe na nikienda nailazimisha tu furaha. Ingawa kila kitu changu kinaenda sawa.

Hivyo leo nikapenda nipate kujua kama nyie wenzangu mlifanikiwa kupata Wenza wa ndoto zenu au wa Mioyo yenu? Kama ndiyo hongera na Kama siyo umewezaje kuishi na huyo ulonaye kwa Sasa? Karibu tupeane uzoefu.
Ndoa nyingi za sasa karibia ziko hivohivi.
Bora ya wewe ulijitia kitanzi huku ukifahamu fika kuwa huyo bwana humpendi nawe humpendi manana ulujiandaa kisaikolojia kukabiliana na hayo unayoishi nayo sema tu wewe unaonekana kigeugeu kwa sasa.

Wapo watu wa kuonewa huruma ila sio wewe. Hawa ni wale ambao walirubuniwa na wapenz wao ama mazingira ya wakati huo ya wapenzi wao na wakajikuta wanaingia choo cha jinsia tofauti na wao.

Tamaa ya mali na pesa za huyo mumeo wa sasa ndivyo vilikuponza.

Hukumpena ila ulipenda pesa zake ndio maana ukajitoa muhanga ukidhami maisha ni pesa na pesa ndo maisha.

Kwa inavo inekana kadiri ya maelezo yako umesha amua liwalo na liwe na kujishusha hutaki tena maana kiburi kimeifunga roho yako.

Sina shaka umeamua kuchepuka ama unajiandaa kuchepuka ili kusuuza roho yako.

Nakushauri anza kufanya ibada kwa dhamira ya hali ya juu kwa kutafuta ukaribu sana wa Mungu ktk imani yako huenda .
 
Ndoa nyingi za sasa karibia ziko hivohivi.
Bora ya wewe ulijitia kitanzi huku ukifahamu fika kuwa huyo bwana humpendi nawe humpendi manana ulujiandaa kisaikolojia kukabiliana na hayo unayoishi nayo sema tu wewe unaonekana kigeugeu kwa sasa.

Wapo watu wa kuonewa huruma ila sio wewe. Hawa ni wale ambao walirubuniwa na wapenz wao ama mazingira ya wakati huo ya wapenzi wao na wakajikuta wanaingia choo cha jinsia tofauti na wao.

Tamaa ya mali na pesa za huyo mumeo wa sasa ndivyo vilikuponza.

Hukumpena ila ulipenda pesa zake ndio maana ukajitoa muhanga ukidhami maisha ni pesa na pesa ndo maisha.

Kwa inavo inekana kadiri ya maelezo yako umesha amua liwalo na liwe na kujishusha hutaki tena maana kiburi kimeifunga roho yako.

Sina shaka umeamua kuchepuka ama unajiandaa kuchepuka ili kusuuza roho yako.

Nakushauri anza kufanya ibada kwa dhamira ya hali ya juu kwa kutafuta ukaribu sana wa Mungu ktk imani yako huenda .
Hahaaaa mkuu kipato hatutofautiani bhana kila mtu ana mudu kuendesha maisha tena mi nikitaka chochote nyumbani naongezewa hadi leo.
Huyu bwana mwanzo alikuwa wa kwanza kujua huzuni yangu tulikuwa tunakutana katika utafutaji kwa vile alikuwa mchunguzi aligundua kama vile kuna kitu kinanitatiza ingawa sikutaka mtu yeyote ajue hali niliyokuwa napitia baada ya kuachana na yule mchumba wa mwanzo zaidi ya ndugu zangu nao niliwaonesha furaha nilipokuwa nao kwani sikutaka waumie na wakose amani sababu najua mara zote hawapendi kuniona sina Amani . Hivyo akatake advantage na akajiphttp://thechoicetz.com/sakata-la-ndege-uchambuzi-na-maswali-ya-zitto-juu-ya-ripoti-maalumu-ya-gazeti-la-jamuhuri/a kazi ya kunishauri baadae akanigeuzia kibao cha kunitaka kwa vile aliweza kucheza na saikolojia yangu ndo nikajikuta ndani ya shela. Isitoshe nilichukulia simple sana kuwa ningeweza kujifunza.
Ila sikulazimishi kunionea huruma na wala siombi huruma ni jinsi ya kufanya moyo utoe makandokando kwa kusikia sauti za wengi mkuu. Pole kama nimekukwaza kwa hii thread nisamehe bure uwe na furaha haaaaa.
 
Pole mkuu naelewa unachopitia.usifeel guilty kwa kutafuta furaha yako.vitisho vyake vya kujiua na mengineyo visikufanye ukagive up furaha yako. Hiyo ndoa inawaumiza nyote wawili bora muivunje tu.
Many people exist but don't live nanyie unaweza kuwa mna exist tu.
Yaani namuonea raha sana Flora Mbasha alivyomuvu on na maisha yake. Changamoto ni zile kejeli na matusi ya watu anayopitia mmmm.
Na hawa wazazi wangu ni wazee wa kanisa sijui wataficha wapi sura zao naona kama nitawatafutia presha za moyo au kifo kwani wananiamini mno na hawategemei kusikia kitu cha ajabu toka kwangu mkuu.
 
Ahsante mkuu hadi misa ya asubuhi sikosi ila sijawahi mwambia hata Padre yanayonisibu na siwezi mwambia kwani kwa kadiri atujuavyo hatoamini atajua namtega. Hata Mwenyekiti wa kigagwe nitaanzaje kumwambia si ataniona mzizi huenda.
mahali ambapo huwa tunakosea wanadamu ni kumtegemea mwanadamu badala ya Mungu yeye kasema tumtwike yeye fadhaa zetu wewe achana na mwanadamu hayo unayoyaona ni mazito na magumu mweleze Mungu anazo njia atayatatua mimi ninachojua ni kuwa hakuna jambo asiloliweza hata kama unaliona liko kama mlima yy analiweza embu jifunze kumtegemea Mungu kwa kila kitu utaona jinsi itakavyokuwa kwa maisha
 
Back
Top Bottom