Mwenyekiti wangu, Mfukuze Nape Uanachama Mara Moja

Ewe Mwenyekiti wangu wa chama Chetu pendwa CCM Dk John Magufuli tunaomba kwa kulinda heshima yetu ya serikali na chama tunaomba umfukuze Uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Mnauye.

Tunashuhudia kijana huyu akikukosea heshima wewe, serikali na chama chetu.
Nape sio mtu wa kwanza kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri.
Walisha ondolewa Mawaziri wengi ambao mimi nimeshuhudia nikiijua siasa kipindi cha JK lakini sijawahi shuhudia Waziri aliye enguliwa kuendelea kuiandama serikali.

Juzi Kitwanga ulimtumbua lakini kwa heshima ya serikali na Chama Kitwanga alikaa kimya, na hakuzungumza chochote.

Tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiondolewa lkn hakuna hata mmoja aliye lalamika na kupiga makelele.

Kwa sasa Nidhamu yaa Nape ktk serikali yako na hata Chama imepungua, ni wazi kwamba huyu ni Mwanachama asiye mtiifu, asiye weza tunza siri za Chama na hata serikali.

Kwa heshima ya chama Chetu na hasa sisi wanachama ambao hatupendezwi na mambo anayofanya Nape tunaomba umvue uanachama.

Nakuomba Mwenyekiti wangu uwe jasiri katika hili, usiogope!!
Kukaa na nyoka ndani ipo siku atakuuma!!

Asante!!

General Mangi
Kukaa kimya nako ni utumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inaonekana we general mangi unawashwa washwa, usimnyime uhuru wake wa kikatiba
 
Nape ni mwana-CCM wa ukweli ila hawa wakina bashite na mjomba wake wanataka kutengeneza CCM yao ya kikundi kidogo
 
Hapa watakuja wengi hasa mashabiki (Sio wanachama)wa upande ule wa chama kingine. Mana huko Tz mwapambana CCM ana CDM. So watajaa wa CDM mana hao ndo wapokeaji wa wote wanaotoka CCM. Ingawa wanasema CCM imetwala Muda mrefu ila ata wakipewa leo atawaongoza mwanaccm. Sijui wanaumwa nini. Nakumbuka 2015. na 2010. Silaa alikuwa na nguvu sana. Yani na hoja. Watu walimpenda na bila kushawishiwa wala kutukanana na kutafuta kiki. Mitandaoni kama sasa. Tz hmfanyi kazi. Kila wakati mnatafuta jambo La kuwatia uvivu na kuwaondoa kwenye Target. Wauza mambo na mhhh watawagombanisha hasa na wajinga mpka nifike 2025 hakuna dira ya maendeleo bali magomvi. Na wkimpata wao ndo mtaabiwa. Mtalishwa unga mpka muelewe. It will be too late.
 
Vya chadema nani anavitamka hadharani. Kila kundi lina miiko. Hata sisi wa weruweru girls tulikuwa na miiko. Kuna siri za Jeshi. Ahhhhh. Kama hujawahi kuwa katika kikubdi utaendelea kumsifia huyo jamaaa wewe. Lakini kama unajua vita. Huwezi toa siri. Utatoka kwanza. Au kukaa kimya. Kwenda kuongelea ndani. Kama wazee wetu. Huwezi juu kama wamedundana mpka unaona Kesho mama kavaa miwani. Baba naye anachechemea. Ila hawatakwambia. Watacheka nk. Ila ukimvuzia mama jikoni. Utaskia misonyo ya mwendo kasi. Peke yake
 
Ndani ya ccm kuna demokrasia ya kweli na kila mwanachama anao uhuru wa kusema ya moyoni, tofauti na kule ukitofautiana na miunguwatu wa chama unaitwa msaliti na kufukuzwa chamani kama sio kupotezwa kabisa.
 
mtoa mada bado unaishi lalaland,nenda kasome katiba ya ccm vipengele vya mwanachama kufutwa uanachama,then uje hapa na hoja inayoeleweka,kwako our no 1 ni kama Mungu haambiwi chochote hata kama yupo uchi,JMP amekuja na ataondoka bali ccm itabaki keep this in mind comrade.
 
Ewe Mwenyekiti wangu wa chama Chetu pendwa CCM Dk John Magufuli tunaomba kwa kulinda heshima yetu ya serikali na chama tunaomba umfukuze Uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mbunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Mnauye.

Tunashuhudia kijana huyu akikukosea heshima wewe, serikali na chama chetu.
Nape sio mtu wa kwanza kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri.
Walisha ondolewa Mawaziri wengi ambao mimi nimeshuhudia nikiijua siasa kipindi cha JK lakini sijawahi shuhudia Waziri aliye enguliwa kuendelea kuiandama serikali.

Juzi Kitwanga ulimtumbua lakini kwa heshima ya serikali na Chama Kitwanga alikaa kimya, na hakuzungumza chochote.

Tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiondolewa lkn hakuna hata mmoja aliye lalamika na kupiga makelele.

Kwa sasa Nidhamu yaa Nape ktk serikali yako na hata Chama imepungua, ni wazi kwamba huyu ni Mwanachama asiye mtiifu, asiye weza tunza siri za Chama na hata serikali.

Kwa heshima ya chama Chetu na hasa sisi wanachama ambao hatupendezwi na mambo anayofanya Nape tunaomba umvue uanachama.

Nakuomba Mwenyekiti wangu uwe jasiri katika hili, usiogope!!
Kukaa na nyoka ndani ipo siku atakuuma!!

Asante!!

General Mangi

Amefanya nini?

Ametoa siri gani za chama toka sirini? Mbona huzisemi na badala yake unalalama tu... mfukuze... mfukuzee... mfukuzee, anatoa siri za chama, anatoa siri za chama...

Hivi ile kusema na yeye amewahi kufuatiliwa na gari la wale mahayawani Toyota Premio Reg. No. T...... waliopiga risasi Tundu Lissu ktk jaribio lao la kutaka kumuua, nayo ni "siri ya chama" kumbe?

Kumbe Nnape Nnauye kutaka kupigwa risasi na kufa nazo ni siri za Chama Cha Makinikia - CCM??

Aisee.....
 
Back
Top Bottom