WADAU WA TPSF 'WAICHARUKIA' TRA / WADAI KUKADIRIWA KODI ZA 'UWONGO'/ RUSHWA YATAJWA
View: https://m.youtube.com/watch?v=j869hATU_8U
Biashara ya usafirishaji kwa asilimia 75 tunafanya na nchi za kusini za SADC, asilimia 25 iliyobaki tunafanya na Bururundi, Rwanda hilo serikali iliangalie
Sheria za kodi za EAC kutumika SADC ni kikwazo
Makampuni ya usafirishaji yamesajiliwa nje ya Tanzania kutokana na sheria za kodi za Tanzania kutokuwa rafiki
Tunajivunia $260 za bandarini lakini $6,000 zinakwenda kwa wasafirishaji wa malori ambayo makampuni yake yamesajiliwa nje ya Tanzania, yaani faida $6,000 kwa kila Lori inakwenda nje haibaki Tanzania. Tunapoteza pakubwa.
Madereva wa malori ya makampuni ya kitanzania wanasimamishwa njia nzima kila kituo cha ukaguzi katika barabara za Tanzania kuulizwa nyaraka hivyo hubeba rundo la makabrasha , lakini yale malori ya makampuni ya nje hayasimamishwi.
Tunasema tunataka Kariakoo iwe kitovu cha biashara eneo hili la Afrika ya Mashariki lakini bidhaa zinazouzwa Tanzania ni ghali kuliko bidhaa hiyo hiyo inayouzwa nchi jirani iliyopita bandari ya Dar es Salaam kutokana na kodi
Wafanyabiashara wa Tanzania na nchi jirani wanaona bora kwenda kununua bidhaa nchi jirani kuja kuuza Tanzania kutokana na bei kuwa ndogo nchi jirani wakati ilipita hapa bandarini Dar es Salaam
Hakuna nchi unaweza kununua bidhaa dukani halafu ukitoka unaanza kuulizwa risiti na task force ya idara ya kodi, ni Tanzania tu huwezi kuulizwa risiti Dubai, Zambia n.k Wafanyabiashara wameacha kuja Kariakoo kwa kuogopa kuulizwa risiti kwa kuviziwa.
Idara ya Research ya TRA ijifunze kuweka kodi zinazoipa Tanzania unafuu ili kuvutia wafanyabiashara wa SADC na EAC waje wanunue bidhaa zilizoagizwa nje Kariakoo
TRA watafute mfumo mpya utakaoondoa usumbufu wa kuviziwa kuombwa risiti na kufanyiwa ukaguzi, maana mfumo wa EDF umepitwa na wakati hausomani na mifumo mingine ....
View: https://m.youtube.com/watch?v=nV4eqpD9PE0