Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,900
- 31,972
MWENGE WA UHURU NA KITABU CHA WATOTO CHA MWENGE WA UHURU ("THE TORCH ON KILIMANJARO")
Mwaka wa 2007 Oxford University Press (OUP), Nairobi walianzisha mradi wa kusomesha Kiingereza na historia pamoja kwa shule za msingi Afrika ya Mashariki.
Nia yao ikiwa wanafunzi wa shule za msingi katika nchi za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania wanafunzi wajifunze historia ya nchi zao wakati wakisomeshwa Kiingereza kupitia vitabu vitakavyochapwa.
Mradi huu mpaka walipowasiliana na mimi walikuwa tayari OUP washachapa vitabu 15 kutoka waandishi Kenya na Uganda na viko katika shule zao vinasomeshwa.
Hapakuwa na kitabu hata kimoja kilichoandikwa kutoka Tanzania.
Jambo hili liliwasikitisha OUP na ndiyo ikawa sababu ya wao kuniomba niandike kitabu katika mradi huo wa kusomesha Kiingereza pamoja na historia.
Nikaandika kitabu, "The Torch on Kilimanjaro."
Kitabu hiki kilizinduliwa Kilimanjaro Kempisky mwaka wa 2007 na nilipewa jukwaa kukieleza mbele ya wageni waalikwa maofisa kutoka Wizara ya Elimu, wauza vitabu na waandishi wa habari.
Kitabu hiki kimechapwa mara mbili kama picha zinavyoonyesha hapo chini na kinasomwa shule za msingi Kenya na Uganda sasa kwa miaka 17.
Hapa nyumbani Tanzania inaelekea kama vile Wizara ya Elimu wanakikwepa kukiingiza katika mtaala kisomwe katika shule zetu za msingi.
Kitabu hiki hakisomeshwi Tanzania.
OUP wanasema hili linawashangaza sana.

MohamedFacebook
www.facebook.com