Mr NdumbaroJl
Member
- Mar 23, 2023
- 69
- 75
MWELEKEO WA MCHAKATO WA USAILI WA WALIMU SEKRETARIATE YA AJIRA: JE, NINI KINAENDELEA?
Na Josephat H
Interview And Carrer Coach
+255656480968
Dar Es Salaaam, Tanzania
👉Leo ni tarehe 28.09.2024, na ni siku chache tu tangu usaili ulipositishwa rasmi kupitia barua iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Sekretariate ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Hadi sasa, hakuna taarifa mpya kuhusu hatua zitakazofuata ila nina imani taarifa mpya zitatolewa hivi karibuni.
MAZINGATIO KWA WAOMBAJI AJIRA,
👉Ni muhimu kuwa tayari kisaikolojia kwa hali yoyote itakayojitokeza ila usifanye makosa ya kufikia hitimisho usaili umefutwa kwa kusikiliza watu ambao wamesha chagua upande wa taarifa wanazotaka kuzisikia na wangependa kuzisikia (kutokuwepo kwa usaili).
Zingatia kwamba, Kuhairishwa kwa usaili, kusitishwa, au kubatilishwa sio mara ya kwanza kutokea pale sekretariate ila labda imekuwa ya kwanza kwa walimu hasa 2024 kwenye hihi mass Recruitment, lakini baada ya muda mfupi usaili unafanyika hivyo ndivyo walivyo Sekretariate.
Hivyo basi, msishangae kupokea barua mpya za kuitwa kwenye usaili, vituo vipya, na taratibu mpya hasa baada ya kumalizika kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura daftari la kudumu na mitihani ya kidato cha pili na cha nne. 👉Pia, siwezi kukufariji kwa uwezekano wa kuitwa kazini na Sekretariate ya Ajira bila kufanyiwa usaili hasa kwenye mazingira kama haya ambayo waombaji ni wengi na wote wanavigezo pia sipingi kwamba hilo haliwezekani lakini pia maswala ya kuajili kwa usaili hapo ndipo makao makuu yake na wanasheria zinazo waongoza kwa MICHAKATO IYO.
Historia imeonyesha kuwa ni kawaida kwa barua za kubatilisha tarehe ya usaili au kupanga tarehe nyingine au kusitishwa na kuleta tangazo jingine Bahada ya mda fulani .
👉Hivyo basi, kwa wale wenye nia ya kujiandaa, endeleeni na shughuli zenu kwa busara ila mkipata muda jiandaaeni tena jiandae kweli kweli.
Na kwa wale ambao wanaamini kuwa usaili umefutwa au utafutwa watachaguliwa moja kwa moja, unaweza kushikilia msimamo huo bila kuwasumbua wengine ambao wameamua kujiandaa ila epuka tu kulazimishia hisia binafsi kuwa taarifa rasmi nje ya utaratibu wa sekretariate wao wenyewe au taharifa rasmi kutokea selikali kuu kwa lengo la kutafuta validation au kupotosha Ni.
Kuna barua pepe zinazozunguka zikionesha Huduma kwa Wateja Sekretariate ya Ajira wakimjibu mtu kuwa “usaili umesitishwa kwa maelekezo kutoka TAMISEMI hivyo wasubilie utaratibu mpya wa kuwapangia kazi moja kwa moja,” na wameweka mawasiliano yao😁.
Mwalimu usiwr Mshamba Huo ni mkakati wa kuandaliwa kisaikolojia ili utapeliwe na utatapeliwa sana tu .
👉Simply and clearly, TAMISEMI haiwezi kutoa maelekezo kwa Sekretariate ya Ajira kwani ni wizara tofauti na kila moja ina mamlaka yake kisheria mbaya zaidi, zote zikiwa chini ya Ofisi ya Rais Wa JMT na hao UTUMISHI ndio kazi yao kutunga sera za maswala ta husuyo utumishi kitaifa, kutafuta wafanyakazi na kuendesha mchata huo sasa uliona wapi Nesi anampa maelekezo Doctar Bingwa ???.
Mwenye mamlaka juu ya Sekretariate ni Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (UTUMISHI) iliyopo chini wazili Boniface Simbacglhawene, Ofisi ya Rais yenyewe, na Rais mwenyewe. So, wao (Tamisemi) wanaweza kufanya kazi na sekretariate kwa kushirikiana tu, sio kutoleana maagizo Mfano: Tamisemi watafanya ubembuzi yakinifu kubaini mahitaji ya walimu ila Wafanyakazi watatafutwa na Sekretariate ya ajira wao ndio wenye hayo Mamlaka kisheria hasa kuendesha usaili .
LAKINI PIA KUITWA KWENYE USAILI SIO KUPATA KAZI
Tuendeleeni kufanya kazi kwa ushirikiano na taasisi zisizo za kiserikali ambazo tunejishikiza huko na kuwa wachapakazi na kuwatii wakubwa wetu kama tulivyokuwa mwazo kabla hata hatujaitwa usaili. Kuitwa kwenye usaili haipaswi kutufanya tuwe na kiburi au kubweteka na kuonesha tabia ya sasa sifanyi kitu soon nasepa. Ni muhimu kutambua kuwa wasomi ni wengi kuliko nafasi za ajira, hivyo hata usaili UFANYIKE au USIFANYIKE, UFUTWE AU USIFUTWE lazima kuna watu wengine bado watakosa kazi tu .
Nashangaa sana kuona mtu ana furaha na shauku ya kuona usaili utafutwa NA KUJIAMINISHA kwamba kwa kufanya hivyo ni rahisi kwake kupata kazi. Haipaswi tuamini kuwa tutapata kazi kwa urahisi katika hii dunia by any circumstances, umemaliza 2014 hukuwahi fanya usaili na bado kazi umekosa ndo ije kua raisi leo usaili ukifutwa sometime is better kujalibu njia nyingine kuliko kuamini njia za kibuniasi .
Kwa mujibu wa maoni ya wadau wengi, Sekretariate ya Ajira imeonesha kuwa vijana wengi wanaopata kazi ni kutokana na juhudi zao binafsi na kufaulu kwao wenyewe. Hii ni tofauti na TAMISEMI ambapo kumekuwa na malalamiko ya mianya mingi ya upendeleo na rushwa kwa wafanyakazi wasio waadilifu na wenye kutanguliza maslahi binafsi hasa zinapokosekana sheria, kanuni na utaratibu kama wanavyofanya Sekretariate na siwezi kuwalaumi kwasababu iyo kazi Sio ya kwao (Recruitment and Selection)
👉Ingawa usaili sio njia pekee ya kupata mfanyakazi mzuri kama wwengi tunavyo dai lakini pia hata kutofanya usaili sio njia pekee ya kupata wafanyakazi wazuri we should fix our educational system na kuacha tambia ta kuondoa tatizo kwa kutumia tatizo linalo leta tatizo zaidi, lengo la usaili mbali na kupata wagombea bora ni kuhakikisha kuwa watu wanapata kazi kwa ushindani wa haki kwenye KUNDI KUBWA LENYE WATU WENGI WENYE SIFA NA VIGEZO na sio ZANDAKALAWE.
Bila mchakato wenye kanuni na sheria, kuna uwezekano mkubwa wa upendeleo kwa kiasi kikubwa sana.
REALITY: Ajira haziwezi kuongezeka kwa kufuta au kubadili mchakato wa kutafuta wafanyakazi bali kwa kuongeza nafasi za ajira kwenye sekta binafsi na mashirika ya umma.
Hata hivyo, hakuna serikali inayoweza kuajiri wasomi wote duniani. Ni muhimu kuwekeza katika biashara binafsi na miradi mingine.
Hili litatusaidia kuzuia kusomesha watu kwa mkumbo, ambapo mwishowe mambo yanaweza kubadilika kama hali ilivyo sasa. Zamani, walimu walikuwa wachache na uhitaji mkubwa, lakini sasa walimu ni wengi na uhitaji umepungua.
Mwisho, tunapenda kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa ajira hizi. Ingawa zinaweza kuonekana chache kutokana na wingi wa wasomi, ni hatua kubwa. Tunamuomba Mh. Rais pia kuwapa nafasi na kuwawezesha vijana wenye nia ya kufungua viwanda, makampuni, na uwekezaji mkubwa ili kuweza kuajiri vijana wenzao kwa kuwapa wahitimu msamaha au punguzo la kodi kwa muda fulani mpaka viwanda na makampuni yao yatakapokuwa makubwa.
Kwa kumalizia, tunamuomba Mh. Rais kuangalia uwezekano wa:
1. Kuongeza nafasi za ajira kwa walimu na sekta nyingine muhimu.
2. Kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa mikopo nafuu ya kuanzisha biashara.
3. Kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje ili kuongeza fursa za ajira.
4. Kuboresha mazingira ya elimu na mafunzo ya ufundi ili vijana wapate ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.
5. Kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ajira ili kupunguza mianya ya rushwa na upendeleo.
Asanteni sana kwa muda wenu.
By Josephat +255656480968