Mwanza: Rais Magufuli aruhusu Machinga kupanga bidhaa zao hata kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya au mkurugenzi sababu ndio waliompa kura

Ubungo wachina wanapata tabu sana kwenye eneo la mradi wa barabara,watembea kwa miguu ndio tabu zaidi kila mahali kuna biashara.
Wewe endelea kushangilia.
Rais wa wetu sisi wanyonge uonevu sasa basi..na tutapanga bidhaa zetu bila bugudha.
 
Nadhani kauli hiyo iwe somo kwa hao viongozi kua wakiona machinga wanakera basi waandae maeneo rasmi kwa ajili ya Machinga. Mathalani sio kila kauli ya raisi huwa direct kama inavyotolea na viongozi mbali mbali akiwemo rais.

Sent using Jamii Forums mobile app

Basi tupange nje ya ikulu pia. Na wafugaji wakikosa malisho wakavamie bustani za ikulu ili iwe fundisho akiona tumkera atutafutie maeneo
 
Jana tumemsikia Rais Magufuli akiwa Sengerema akiagiza kwa mkuu Wa mkoa Mwanza kuwa wafanya biashara wadogo wasibughuziwe na kwamba hata hao wauza mananasi wakiona wakipanga hayo mananasi mbele ya ofisi ya DC au DED inalipa wasibughuziwe.
Tamko LA Rais ni kama sheria, hivi kweli biashara ikiwa holela namna hiyo hata usafi unaweza kudhibitiwa? Au yeye furaha yake ni KUSHANGILIWA tuu?
Kwa kweli anatukwaza sisi watendaji Wa serikali watoa maamuzi.
Ukitaka kujua kuna tatizo kwa huyo mtu ngoja nikukumbushe kauli zake 3 tu
1. Fyatueni watoto wengi kwa sababu elimu ni bure-kauli hii ilitenguliwa na ummy
2. Machinga kariakoo dar fanyeni biashara zenu na mtu yeyote asiwabughuzi-kauli hii ilitenguliwa na makonda
3. Mwanza hawa ni wapiga kura wangu waacheni wafanye biashara mitaani - hii nayo ilitenguliwa na mongela

My take
Huyu mtu ana tatizo kubwa sana kuliko tunavyodhani
 
Jana tumemsikia Rais Magufuli akiwa Sengerema akiagiza kwa mkuu Wa mkoa Mwanza kuwa wafanya biashara wadogo wasibughuziwe na kwamba hata hao wauza mananasi wakiona wakipanga hayo mananasi mbele ya ofisi ya DC au DED inalipa wasibughuziwe.
Tamko LA Rais ni kama sheria, hivi kweli biashara ikiwa holela namna hiyo hata usafi unaweza kudhibitiwa? Au yeye furaha yake ni KUSHANGILIWA tuu?
Kwa kweli anatukwaza sisi watendaji Wa serikali watoa maamuzi.
Wewe sio Mtendaji wa serikali acha mdomo mrefu. Ile kauli haina utata wowote. Kama hujui siasa nyamaza kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubungo wachina wanapata tabu sana kwenye eneo la mradi wa barabara,watembea kwa miguu ndio tabu zaidi kila mahali kuna biashara
Kwa hiyo kwa sababu wewe una kibarua unataka wenzako wakale wapi?!

Tokea raisi aingie Madarakani mgambo wa jiji wamenywea kama piriton
 
Hivi umepita Ubungo umeona kinacho endelea,au unaandika tu hapa kujifurahisha.
Kwa hiyo kwa sababu wewe una kibarua unataka wenzako wakale wapu?!

Tokea raisi aingie Madarakani mgambo wa jiji wamenywea kama piriton
 
sm-IMG_5575.jpg

downloadfile-10.jpg

Machinga kila sehemu hapa duniani wapo.
 
Ukitaka kujua kuna tatizo kwa huyo mtu ngoja nikukumbushe kauli zake 3 tu
1. Fyatueni watoto wengi kwa sababu elimu ni bure-kauli hii ilitenguliwa na ummy
2. Machinga kariakoo dar fanyeni biashara zenu na mtu yeyote asiwabughuzi-kauli hii ilitenguliwa na makonda
3. Mwanza hapa ni wapiga kura wangu waacheni wafanye biashara mitaani - hii nayo ilitenguliwa na mongela

My take
Huyu mtu ana tatizo kubwa sana kuliko tunavyodhani
Usemalo ni kweli, maana hata Sera za chama Tawala anachokiongoza sio hizo.
Kuna mipango miji na taratibu za kufanya biashara kwa sheria sasa kama Rais anasema biashara ya mananasi hata ikipangwa kwenye korido LA DC ndio inauzika wasibughuziwe inatia Mashaka uwezo wake Wa kiuongozi
 
Niwe nisiwe sio juu yako. Na kusema haina utata wowote ndipo unapoonyesha una uwezo kiasi gani katika kufikiri.
Kuruhusu mananasi yakapangwe hata ofisi ya DC kwako ni sawa!
Wewe ni papai. Hivi unajui kiswahili vizuri. Pia unajua maadili ya watumiahi wa umma, ndivyo ulivyoelekezwa kwamba watendaji wa serikali mahala pao pa kutolea kero ni humu JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom