MWANZA: Jeshi la Polisi lamkamata mfanyabiashara akiwa na madawa ya kulevya

Hongera Makonda juhudi zako zimezaa matunda askari wa Mwanza wamefanya vizuri ....njia ya Makonda imewafikia wengi Mungu akulinde na usikate tamaa
 
Hawa polisi wamenifurahisha kweli na hii ndio ufanyaji kazi wa kipolisi sio wengine wanafanya kazi kama sungu sungu
 
Njia ya Makonda ni bora zaidi.....vijiwe vingi vya wauza ngada Dar vimepotea
Uko sahihi kabisa hasa ukizingatia na taarifa ya habari ya juzi channel ten walipowatembelea mateja, wengi walikuwa wanalalamika arosto! kwamba wanalalalala ovyo ovyo, kujiny**ea n. k

Kweli unga umetoweka, but is't forever!? I hope ni kwa muda tu hasa kwa technique inayotumika! Mateja huenda wakafa kwa arosto, lakini wauzaji wakubwa na baadhi ya wasambazaji wakabaki

Unamuita TID na Chid Benzi kwenye media, wanakili kwamba kweli wanatumia, halafu unatangaza tena kwenye media kwa kukiri kwao!? Hivi watakutajia wanaowauzia kweli!? Hawataingiwa na hofu ya usalama wao kweli!? Nadhani media ni nzuri, lakini sio pa kusemea kila kitu jamani tuweni watu wazima sasa!!
 
Naamini Jeshi la polisi mkoa wa dar wakiachwa kufanya kazi zao bila ya kuingiliwa na mtu yoyote yule, (kama ilivyo sasa) ambaye hana mafunzo wala mbinu zozote zile za kijeshi naamini watafanikiwa vizuri tu , even hata zaidi ya hawa wenzetu wa mwanza katika vita hii ya ngada.
 
Hapa mbinu za utaalam kijeshi zimetumika na kuleta mafanikikio,kule Dar askari waliamua kwa manufaa yao kuingiliwa kazi na mwanasiasa anayesaka umaarufu hivyo kutofanikiwa mpaka sasa kukamata hata kete moja zaidi ya msokoto wa bangi kwa wema ambapo tuliosoma saikolojia ya polisi tunajua walichomtendea Wema
 
Nawapongeza Mwanza.HUku Dar ni sheeda!Full kuabishana na manyanyaso.
 
Hii ndo inatakiwa sasa,

natumaini mangu akistaafu msangi anafaa sana kuwa IGP maana hakurupuki
Mkuu wamekosea kidoooogo!
Swala la kuvamia nyumba ya mtuhumiwa usiku inahitaji ithibati.

Kinyume chake wameenda na hayo madawa kwa nia ovu.

Ni mambo ya sheria ya ushahidi tu mkuu.
Full mikurupuko.
 
huyo kamanda wa mwanza c mtu wa mchezo mchezo namuonaga sana kwe media akituripotia vitu vnavyoeleweka...jamaa hana maneno sana yeye ni kazi tu
 
Back
Top Bottom