1gb
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 2,169
- 2,820
MUNGU HACHELEWI WALA HAWAHI ni Tafsri ya vifungu hivi vya maandiko.mkui huu mstari wa kwenye biblia wa HACHELEWI WALA HAWAI.
unatoka kifungu gani ,msaada tafadhali
“Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.”
— Habakuki 2:3
“Maana mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU.”
— Ezekieli 12:25.
“Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.”
— Zaburi 27:14 .
Jambo lolote alilokusudia Mungu kwny Maisha yako litatimia tu,kwa majira yaliyokusudiwa.
“Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?”
— Hesabu 23:19
“Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.”
— Zaburi 33:11.
KARIBU.