Mwanaume kusaidiwa kulipa mahari na mkewe mtarajiwa ni sahihi?

Wanaume tumebaki wachache sana, nasikitika kuona kuna wanaume wanafurahi kulipiwa mahari na wachumba zao. Aibu sana
Na wanatetea kabisa. Sasa si bora usitoe hayo mahari umchukue bure.

Ila pia wanawake na wenyewe wameisha. Hakuna mwanamke atakubali kumlipia mwanaume mahari wote watakuwa wale wale tu.
 
Inategemea na wewe umejipangaje au nini chanzo cha kukosa mahari.Kama umejenga au umefanya mambo mengine,na hela huna,akikusaidia sawa(lakini labda kunahitajika ndoa ya haraka na pengine labda kamimba).Lakini kama huwezi kulipa mahali,nini utaweza? Kama kweli amedhamilia, bora muishi kimjini mjini,hiyo hela iwe mtaji mtayenda badae.
Vinginevyo,kutoa mahari,sherehe,mkirudi? Mtaanza kuchukua mikopo kila kona?
Kama kweli mmependana fanyeni yaliyo ndani ya uwezo wenu, ila kusaidiwa kulipiwa mahali sahau aise!
Hali mbaya zipo mpaka pale uwezo huo mtu anakosa,lakini kama we ni mchakalikaji,bora uichukue,ifanyie kazi(kama mtaji),lipa mahali mliyokubaliana,hera yake mrudishie aifanyie mambo mengine.Vinginevyo hapo ni sawa na umepata mke bure.Hutajua thamani yake
 
Habari wanaJf wenzangu na heri ya pasaka japo nimechelewa kuwatakia heri .. Kama kichwa cha habari kinavyosema ni mjadala ambao nimekuwa nikiusikia mara kadha na kiukweli kwangu mimi imeshindwa kuingia akilini nimeona nishare na nyie tuone mawazo yenu juu ya hili swala la kidume kusaidiwa kulipa mahari na mkewe mtarajiwa... Nini haswa kina mpelekea kulipiwa mahari?? Je kuna madhara yoyote kwa mwanaume kulipiwa mahari??
Mkuu hiyo ni weka mbali na watoto asee siwezi ata kwa mbali kijaribu
Ninyi nyote bado ni primitive minded, hakuna athari yeyote endapo lengo ni kuwa mke na mume ndani ya ndoa bora yenye upendo wa dhati, ila kama kuna anaye taka uchief na utemi ndani ya ndoa kweli kuna madhara.
 
Huwa inatokea. Home kwa binti wanataka mahari say 2.5M. Mwanaume anamwambia mchumba wake mimi sina hela hiyo hela, nona 1.5M tu kwa sasa...kama vipi tusogeze harusi mpaka mwakani. Binti kachoka kusubiri anaamua "kumchangia" mchumba wake ile deficit ili mambo yaende.

Nimeshaiona hii kitu kwa watu wawili.
 
Sina maana hiyo...

Labda tuambizane mahari kiutaratibu nani anatakiwa ailipe?
Mahari kiutaratibu Lazima ME ndio atoe, nisl sawa na kuoa, kuoa lazima aoe Mwanaume Na sio mwanamke ndio Aoe the same case na Mahari lazima Atoe mwanaume.

Sasa km ME hana uwezo inafaa mwanamke kumpa pesa Mchumba kwa Mlango wa Nyuma ili Akatoe mahari kwa Mlango wa Mbele.
 
Haha haha... Nwei haya maisha bwana kila mtu na mtizamo wake ilimradi unapeleka kitu kinywani na unaishi ni ok.
 
Desturi zetu waafrika ni mahari alipe mwanaume, muhimu ni kumuomba mchumba wako ndugu zake wapange mahari inayoendana na uwezo wako, kama umepungukiwa omba ndugu zako wausaidie ila sio huyo mchumba wako, hata hivyo mahari sio lazima utoe yote,

Tatizo kuna familia zinasifa za kijinga wanamfanya binti yao mtaji, wanataka makorokoro kibao na pesa juu, familia za hivyo unamueleza tu binti wazi mi hiyo siwezi, nilichonacho ni hiki, kama anakupenda kweli mtaoana tu hawezi kukukataa kisa mahari

Desturi za kiafrika kwenye suala la ndoa/kuoza huwa ni desturi za kipumbavu sana zinazoashiria umasikini uliotukuka uliopo katika bara hili, hivi huwa ni lazima kutoa mahari? Ni nini msingi wa kutoa mahari!? Mimi ukija kumuoa binti yangu hata kwa kilo moja ya unga wa udaga unamchukua

Familia zinazoendekeza pesa na kuwafanya mabinti zao mtaji huwa nazidharau sana, mimi nimewahi kimkosesha bro wangu mke kwa sababu ya huo ujinga, tumeenda kutoa mahari eti mashangazi wanatwambia binti yao wana muoza kwa milioni 17 kisa tu ana kadegree ka mambo ya Nutrition... Asee pale pale niliwatukana wote na hawatokaa wanisahau
 
Habari wanaJf wenzangu na heri ya pasaka japo nimechelewa kuwatakia heri .. Kama kichwa cha habari kinavyosema ni mjadala ambao nimekuwa nikiusikia mara kadha na kiukweli kwangu mimi imeshindwa kuingia akilini nimeona nishare na nyie tuone mawazo yenu juu ya hili swala la kidume kusaidiwa kulipa mahari na mkewe mtarajiwa... Nini haswa kina mpelekea kulipiwa mahari?? Je kuna madhara yoyote kwa mwanaume kulipiwa mahari??
Binafs sion kama kuna madhara but kwa wapendanao kusaidiana in vema
 
Habari wanaJf wenzangu na heri ya pasaka japo nimechelewa kuwatakia heri .. Kama kichwa cha habari kinavyosema ni mjadala ambao nimekuwa nikiusikia mara kadha na kiukweli kwangu mimi imeshindwa kuingia akilini nimeona nishare na nyie tuone mawazo yenu juu ya hili swala la kidume kusaidiwa kulipa mahari na mkewe mtarajiwa... Nini haswa kina mpelekea kulipiwa mahari?? Je kuna madhara yoyote kwa mwanaume kulipiwa mahari??
Kulipiwa mahari na wazazi si jambo geni katika jamii yetu,ila kulipiwa mahari na mke mtarajiwa ndilo jambo geni.Naomba kwa faida ya wasomaji wangu nidadavue ulipaji wa mahari kwa ujumla,halafu ndio nihitimishe na swala la kulipiwa mahari na mke mtarajiwa au mchumba.

Zamani wazazi ndio waliokuwa na jukumu la kuwalipia watoto wao mahari kwa kuwa wao ndio waliokuwa wamekamata njia kuu za uchumi kama mashamba na mifugo.Ajira ilikuwa ni kitu adimu sana wakati huo.Mpaka mtu aoe ndio agawiwe urithi wake na kuanza kujitegemea,kwa hiyo kulipiwa mahari na wazazi ilikuwa sahihi .

Kwa sasa mambo yamebadilika sana.Vijana wanaanza ajira mapema au kuanza kujitegemea kwa njia yeyote ile. Wazazi nao kwa upande mwingine uwezo ule uliokuwepo zamani wa mashamba na mifugo haupo tena kwa makabila mengi kwa kuwa mashamba yamekuwa madogo, productivity imeshuka mno na ufugaji maeneo mengi hakuna, simply because enough land isn't there anymore.Kwa sababu hiyo hawawezi kuwa na uwezo wa kulipia vijana wao mahari ambayo kwa sasa imefanywa kama biashara na ni kubwa mno! Worse still vijana wengi wazazi wao waliokuwa waajiriwa wamestaafu.Wastaafu hawa wengi uwezo wao ni mdogo mno,unless walipokuwa waajiriwa walikuwa mafisadi na wapiga dili. Most of them therefore have only enough for a days meal kwa hiyo huwezi kutegemea wawalipie vijana wao mahari!

Kulipia mahari vijana sasa sana sana imebaki kwa makabila ya kifugaji ambayo yana mifugo kama Wasukuma,Wamasai na Wabarbeig.Kwa mantiki hiyo kwa mazingira ya sasa,kijana anapaswa kujilipia mahari mwenyewe kwa kuwa wazazi hawana uwezo,unless mzazi voluntarily anaamua kulipa mahari. Hata hivyo,kijana mwenye busara atasema no father,ziweke hizo zitakusaidia baadae.

Nimetangulia kusema kwamba hili la kijana kulipiwa mahari na mchumba ni geni katika jamii yetu na si sahihi kwa kuwa inamdhalilisha binti.Naomba pia ieleweke kwamba kuweza kujilipia mahari ni test tosha kwamba hatimaye kijana ataweza kuihudumia familia yake. For if you can't even pay your dowry now, how for God's sake can you take care of your own family in future?

Kwa upande mwingine wasichana hii iwe your yard stick.Kijana asiyeweza kukulipia mahari from his own pocket hakufai,kwa kuwa most likely hataweza kukuhudumia hata baadaye.It turns out therefore that binti kumsaidia mchumba wake kulipa mahari is wrong.What she is infact doing ni kuchimba shimo ambalo litamkufukia yeye mwenyewe!How stupid.
 
Naunga mkonyo hoja(in makinda's voice)
Inategemea na wewe umejipangaje au nini chanzo cha kukosa mahari.Kama umejenga au umefanya mambo mengine,na hela huna,akikusaidia sawa(lakini labda kunahitajika ndoa ya haraka na pengine labda kamimba).Lakini kama huwezi kulipa mahali,nini utaweza? Kama kweli amedhamilia, bora muishi kimjini mjini,hiyo hela iwe mtaji mtayenda badae.
Vinginevyo,kutoa mahari,sherehe,mkirudi? Mtaanza kuchukua mikopo kila kona?
Kama kweli mmependana fanyeni yaliyo ndani ya uwezo wenu, ila kusaidiwa kulipiwa mahali sahau aise!
Hali mbaya zipo mpaka pale uwezo huo mtu anakosa,lakini kama we ni mchakalikaji,bora uichukue,ifanyie kazi(kama mtaji),lipa mahali mliyokubaliana,hera yake mrudishie aifanyie mambo mengine.Vinginevyo hapo ni sawa na umepata mke bure.Hutajua thamani yake
 
Mkuu popote ulipochukua ka balim nakuja kulipa
Jambo hili si ge katika jamii yetu.Zamani wazazi ndio waliokuwa na jukumu la kumlipia mtoto wao mahari kwa kuwa wao ndio waliokuwa wamekamata njia kuu za uchumi kama mashamba na mifugo.Ajira ilikuwa ni kitu adimu sana wakati huo.Mpaka mtu aoe ndio agawiwe sehemu yake na kuanza kujitegemea,kwa hiyo kulipiwa mahari ilikuwa sahihi .

Kwa sasa mambo yamebadilika sana.Vijana wanaanza ajira mapema au kuanza kujitegemea kwa njia yeyote ile. Wazazi nao kwa upande mwingine uwezo ule uliokuwepo zamani wa mashamba na mifugo haupo tena kwa makabila mengi kwa kuwa mashamba yamekuwa madogo, productivity imeshuka mno na ufugaji maeneo mengi hakuna, simply because enough land isn't there anymore.Kwa sababu hiyo hawawezi kuwa na uwezo wa kulipia vijana wao mahari ambayo kwa sasa imefanywa kama biashara na ni kubwa mno! Worse still vijana wengi wazazi wao walikuwa waajiriwa na wamestahafu.Hawa wengi uwezo wao ni mdogo mno,unless walipokuwa waajiriwa walikuwa mafisadi na wapiga dili. Most of them therefore have only enough for a days meal kwa hiyo huwezi kutegemea wawalipie vijana wao mahari!

Kulipia mahari vijana sasa sana sana imebaki kwa makabila ya kifugaji ambayo yana mifugo kama Wasukuma,Wamasai na Wabarbeig.Kwa mantiki hiyo kwa mazingira ya sasa,kijana anapaswa kujilipia mahari mwenyewe kwa kuwa wazazi hawana uwezo. Infact hii ni test tosha kama hatimaye kijana ataweza kuihudumia familia yake. For if you can't even pay your dowry, how can you take care of your own family in future?Kwa upande mwingine wasichana hii iwe their yard stick.Kijana asiyeweza kukulipia mahari hakufai,kwa kuwa hataweza kukuhudumia baadaye.It turns out therefore that binti kumsaidia mchumba wako kulipa mahari is wrong.
 
Back
Top Bottom