Mwanasheria:Wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji wa madini kadri wanavyoona inafaa

Come on, one of the responsibilities of the Minister is to advise the President on matters pertaining to law of the country, among others , while the AG is responsible , among , to advise the President on legal technicalities.........
But the attornery general being the principal architecture of all legal draft is in better position to work on those matters. And also his office being the custodians of all legal documents of the government he can study them and provide the needed advice more than the minister whose main responsibilities are to drive the policy of the ministry
 
Unajuwa watu kuingiza siasa katika mambo kama haya tutaenda kubaya, Rais lazima aambiwe ukweli maana mkataba wa mpangaji tu na mwenye nyumba una terms and conditions sasa mikataba mikubwa kama hii, Mimi wasiwasi wangu tu isiwe kuwa CCM wanajuwa matokeo sasa ili wanataka wapate huruma kwa wengi bila kujua madhara ya kuiuchumi wawachague tu ni kama ya Mugabe hata kama alikuwa sawa lakini hali ilikuwa hairuhusu ila yeye alikuwa na target moja tu ku win election ndio kuja kuwapokonya mashamba sio wawekezaji ila wazimbabwe wachache matokeo akapata umaarufu sana lakini matokeo tuliona pesa yao tu wakawa wanaikimbia. kitu kimoja usimuamini mwana siasa anaweza kufanya lolote ili abaki kutawala hiyo ndio primary target. haya makampuni ya nje yako stock market lazima yaweke kila kitu wazi ukidanganya tu penalty yake sio mchezo ni kama yale ya kampuni ya Siemen kutoa hongo balaa lake fine 5 Billion$ ndio maana sitaki kuamini ACCACIA wafiche mapato maana ni pesa za watu hizo stock exchange. TZ wakacheck income ya jamaa halafu wacheck walilipa ngapi suala la 4% hilo ni ujinga wetu sio wao.
kama hayo makampuni yako kwenye stock exchannge kwa sheria na kanuni za huko kwenye nchi zao ni kwa nini serikali kupitia taasisi zake kama Stamico hawajawai kwenda kununua share ili wawe watch dogs wetu.

Je kama tulilazimiswa kusaini MIGA na BITs ni kwanini tulilidhia bila ya kuweka condition kuwa selikali yetu italazimika kununua share za mwekezaji kupitia stock exchange ili kulinda maslahi ya nchi.

hebu wanasheria tusaidieni hapa
 
Kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhui na mada ikiwa ni Uzalendo kwa Maslahi ya Taifa, mwanasheria wa kujitegemea,Gaspar Mwanalyela amerejea taarifa ya Policy Forum kuhusu mikataba/sheria zetu za madini na kunukuu clause mbili mojawapo ikitamka wazi kuwa, "wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji kadri wanavyoona inafaa."

Akasoma na kifungu kingine kinachosema kuwa hatuwezi kutaifisha mali za wawekezaji hawa.

Chanzo:Star tv

Hata pale mjengoni huwa tunaona kiti kinavyoweza kufanya maamuzi kadri ya aliekikalia anavyoona inafaa na madhara yake tunayajua na hata yule wa magogoni nae anaweza kuamua kari anavyoona inafaa na tumeyaona matokeo yake.

Naungana na mwanasheria huyu pale anaposema mikataba hii ni mikataba ya "kimangungu".
Sasa huyo mwanasheria anajua nini kuhusu sheria na mikataba ya madini? Huyo kijana Alikuwa anaisaidia chadema kwenye kesi dhidi ya Dr. Kafumu kwa mategemeo ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Ilemela kupitia chadema mwaka 2015. Kilichomtokea hawezi kukisahau maana uhuni aliofanyiwa na chadema hana hamu
 
Mw
Kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhui na mada ikiwa ni Uzalendo kwa Maslahi ya Taifa, mwanasheria wa kujitegemea,Gaspar Mwanalyela amerejea taarifa ya Policy Forum kuhusu mikataba/sheria zetu za madini na kunukuu clause mbili mojawapo ikitamka wazi kuwa, "wawekezaji wanaruhusiwa kufanya uchimbaji kadri wanavyoona inafaa."

Akasoma na kifungu kingine kinachosema kuwa hatuwezi kutaifisha mali za wawekezaji hawa.

Chanzo:Star tv

Hata pale mjengoni huwa tunaona kiti kinavyoweza kufanya maamuzi kadri ya aliekikalia anavyoona inafaa na madhara yake tunayajua na hata yule wa magogoni nae anaweza kuamua kari anavyoona inafaa na tumeyaona matokeo yake.

Naungana na mwanasheria huyu pale anaposema mikataba hii ni mikataba ya "kimangungu".
Mwaka huu mtapagawa enyi bavicha. Jpm kasha washika hamuoni pa kutokea. Kila mtu mnahisi anaweza kuwa msaada kwenu. Hata ikitokea kesho jpm akaruhusu mchanga uondoke nje mtapumua kidogo. Sasa hivi kila sikio LA mwanachadema limeelelezwa kwa kila mwanasheria anayetamka kuishtaki au kusaidiana na mafisadi dhidi ya serikali. Maskini chadema mnatapatapa na imewachanganya sana hili la mchanga mana hamkuamini kama ccm au jpm angechukua hatua. Sasa sijui mkiibua madudu huwa lengo lenu serikkali iyafanyie kazi au iache ili muendelee kuwepo hewani!!!!
 
Sijasema Anavunja mikataba, Katika kesi kutakuwa na madai au remedies for non performance,hao Acacia walisema wanapoteza sijui dola zaidi ya million kwa siku .. sasa calculate tutakacho walipa...hakukuwa na haja ya kuyazuia makontena 277, angezuia tu 3-5 hivi ili ku- prove point ...na wakati hao jamaa wanaendelea na shughuli yao, kamati YA JPM nayo ingeendelea na mambo yao.. baada ya hapo, tumawadai backdated loss na wasipolipa inakuwa ni chanzo cha kusimamisha mikataba kiulaini...
 
kama hayo makampuni yako kwenye stock exchannge kwa sheria na kanuni za huko kwenye nchi zao ni kwa nini serikali kupitia taasisi zake kama Stamico hawajawai kwenda kununua share ili wawe watch dogs wetu.

Je kama tulilazimiswa kusaini MIGA na BITs ni kwanini tulilidhia bila ya kuweka condition kuwa selikali yetu italazimika kununua share za mwekezaji kupitia stock exchange ili kulinda maslahi ya nchi.

hebu wanasheria tusaidieni hapa
Unayo point nzuri tu, unajuwa ni ukweli wote tunaujuwa ukiwa registered stock exchange mahesabu yote lazima yawekwe wazi sababu kubwa ni pesa za watu, sasa nchi zingine wanakuwa na kampuni owned wao kazi yao kununua shares kuinvest kama kampuni lakini ni Goverment wanaimiliki inakuwa inajiendesha kifaida. Mimi na uhakika 100% kama unataka upuuzi basi usiwe katika stock exchange vinginevyo huko kila kitu wazi hata wakati wakufunga mahesabu ya robo mwaka au mwaka shares zinakuwa wanasimamisha kuuza mpaka mahesabu yatoke kama kuna faida au hasara na inside trading ni marufuku wewe uwe Manager halafu ujue kuwa kampuni haikufanya vizuri umpe tip ndugu akauze shares au kinyume akanunue yaani unafungwa jela. inside trading marufuku kabisa. ACCACIA nasikia wako S.Exchange kwa hilo hawawezi kufanya magumashi ni hatari ukitoa dola mia lazima iwe ina maelezo huo ndio ukweli.
 
Courtesy group la telegram
===
Tumsome maftaa Mbunge kanena kisheria zaidi.


MBUNGE MAKINI WA MTWARA MJINI MAFTAH NACHUMA (Cuf) .

Imeandikwa na Maftah Nachuma (MB)
Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(im
plied obligation).
Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.
Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.
Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).
2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).
3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fra
ud).
Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.
Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;
1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).
2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).
Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.
Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.
Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.
Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.
Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.
Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.
Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.
Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.
Ni wakati sasa watanzania wote bila kujali Itikadi za vyama au Dini kuungana pamoja kupigania haki yetu.
Prof Ibrahimu Lipumba alionya jambo hili miaka kumi wakati wa utawala wa awamu ya tatu lakini serikali haikuchukua hatua za msingi.
Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.
MAFTAH NACHUMA Mbunge Mtwara mjini.
Dah!! Kweli jamaa kaeleza vitu vya maana sana naunga mkono 100%
 
Back
Top Bottom