George Michael
George Michael mmoja wa wanamuziki maarufu duniani amefariki dunia leo nyumbani kwake.
Familia ya George imeomba kuheshimiwa kwa faragha yao.
George Michael alizaliwa akiitwa Georgios Kyriacos Panayiotou katika kitongoji kijulikanacho kwa jina la Finchley, kaskazini mwa jiji la London, nchini Uingereza.
George alishiriki kuimba katika kundi la Band Aid kwenye kibao kiitwacho 'Do They Know It's Christmas' (1984), na baadae kushuka na vibao vingine vikali vya 'Careless Whisper' na kingine cha 'A Different Corner'.
Mwaka 2002 alitunga muziki uloitwa Shoot the Dog ambao katika video yake alikuwa akiwakebehi Tony Blair Cherie Blair na George Bush.
George ameuza Zaidi za santuri milioni 100 katika maisha yake yote ya muziki katika uahi wake ulosambaa ndani ya miongo mine.
Katika miaka ya hivi karibuni George alikuwa akikabiliwa na matatizo ya ulevi wa madawa ya kulevya na pombe.
lakin chanzo halisi cha kifo chake hakijawekwa wazi na mtoa habari wake.