Mwanamke ambaye hajijali na hajali hawezi kukujali wala kujali Watoto wako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
23,815
56,817
MWANAMKE AMBAYE HAJIJALI NA HAJALI HAWEZI KUKUJALI WALA KUJALI WATOTO WAKO

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Unaweza ukawa kijana smart na mwenye bidii ya kutafuta maendeleo.

Lakini ukajikuta jitihada zako zinaishia ukingoni baada ya kukutana na Mwanamke kisha ukamuoa(ukaamua kuishi naye).

Ogopa Mwanamke asiyejali wala kujali.
Huyu ni kansa kubwa ambayo ukiipata umekwisha.

Mwanamke asiyejijali ni yule asiyejali utu wake.
Utu ni heshima ya ndani ya binadamu.

Utajuaje Mwanamke huyu ni garasha, cherema au HAJIJALI.
1. Hufanya mambo mabaya kwa visingizio kwamba angefanyaje.
Mfano, Mwanamke yeyote, narudia yeyote bila kujali nafasi yake, cheo, umri au vyovyote vile ambaye anafanya ukahaba au umalaya kwa kisingizio kuwa ati angefanyaje elewa mwanamke huyo hafai hata kidogo kuwa mkeo.

Kuna wale wanawake wanajiuza ati kwa kisingizio wasomeshe au wajishe watoto. Ukikutana na Mwanamke wa hivyo kaa naye mbali. Hapo hamna kitu.

Ni akheri hao watoto wafe au wewe ufe au familia ife kuliko kujishushia heshima.
Kazi zipo nyingi fanya hizo. Hata kama unapata miambili mia mbili ni akheri kuliko ujivue utu wako na mnyama awe na thamani kuliko wewe.

2. Hutumia mwili wake kama chanzo cha mapato
Ukipata mwanamke anayeweza kuhudumiwa tuu ukimuuliza sababu anaanza kupiga blah blah! Mwingine anakuambia kisa anakupa papuchi. Jua hapo hamna kitu.

Ukiwa unachumbia ukakuta binti anakataa pesa zako na mapenzi yenu yanaendelea tuu. Au wote mnapeana vitu na zawadi jua hapo umepata Mke na mama bora wa familia.

Mwanamke anayetumia mwili wake kama silaha ya mapato huyo mkimbie. Hamtafika popote.
Soon utajikuta kwenye ile Mass kwaya ya kuimba Kataa Ndoa.

3. Anatumia uanamke wake kama udhaifu wa kufanya makosa ya makusudi.
Mwanamke hana udhaifu katika Makosa ila hutumia kwa makusudi neno udhaifu kufanya makosa kama makosa ya kiuchumi.
Unampa mtaji lakini kwa makusudi anatumia kwa mambo yake mengine kama urembo alafu ukimuuliza analeta uanamke wake wa kijinga.
Mwanamke bora hufanya jitihada kuonyesha kuwa hata mwanamke anaweza kufanya vitu vikatokea.

4. Huwa tegemezi.
Mwanamke yeyote ambaye ni tegemezi na anauendekeza utegemezi huyo hafai kuwa mkeo wala hawezi kutunzia watoto wakawa watoto wa kueleweka.
Mwanamke yeyote ambaye anafanya kazi za uzalishaji huyo ana moja ya sifa ya kuwa Mke na kuanzisha naye familia.

Mwanamke ambaye atakubali kuambiwa akae nyumbani bila kufanya kazi huku asipewe utaratibu wa vipi ikitokea mume amekufa au vipi ikitokea ukaniacha asiwaze hayo na kuyasema kwako jua hapo hakuna kitu hilo ni kopo. Hawezi na hafai kuwa mke. HAJIJALI wala hatakujali wewe na watoto wako.

5. Haoni umuhimu wa mambo ya Msingi Kama Elimu.
Mwanamke yeyote ambaye haoni umuhimu wa elimu huyo mkimbie.
Huyo atakuharibia watoto wako.

Mtoto aende shule asiende kwake ni sawa. Mtoto afaulu asifaulu kwake ni sawa. Mtoto amevaa vizuri nguo za shule au kavaa kihuni kwake ni sawa.
Hapo hamna kitu.

Usiendekeze ndoa za kijinga.
Ndoa sio kuvumilia ujinga wa makusudi.
Ndoa sio sèhemu ya kuvumilia uhujumu wa hatma ya familia. Hiyo sio ndoa. Fukuza haraka.

6. Mwanamke anatumia kipato chake Rafu. Hajali jasho lake.
Huyo mkimbie.
Lazima uwe na Mwanamke mwenye akili yaani mfano wa mwanaume.

Elewa Mwanamke aliumbwa kwa mfano wa mwanaume ili àwe msaidizi wa mwanaume.
Mwanamke ambaye sio mfano wa mwanaume hawezi kuwa msaidizi wako.

Usijesema hao wanawake mfano wa wanaume hawapo. Wapo kibao.
Sema wengi mnakimbilia wanawake mfano wa wanawake na sio wanawake mfano wa wanaume.

Kama hajali jasho lake ndio atajali jasho lako?

Ni lazima Mwanamke mwenye Akili ukimpa pesa ajue inatoka wapi.
Lakini ogopa Mwanamke ambaye hakuulizi unapàta wapi pesa. Na hataki kujua yaani hajali anachojali ni yeye apewe pesa basi.
Huyo hakutakii mema na anatamaa.

Elewa, Mwanamke atakayekuwa mkeo anaenda kuchukua nafasi ya Mamaako na wewe unaenda kuchukua nafasi ya Babaake.
Kila mmoja ni mzazi kwa mwenzake.

Mzazi lazima ajali usalama wa mtoto wake. Mke lazima ajali usalama wa mume.
Na mume lazima ajali usalama wa mke.

Kwa kufanya hivyo usalama wa familia na kizazi cha familia hiyo unakuwa salama.
Kipato huwa chanzo cha baraka au laana ndani ya familia au kizazi ndio maana Mwanamke makini lazima aulize chanzo cha pesa zinazoletwa na mumewe kama ni halali au haramu.

Hakuna mwanamke au mwanaume anayetaka abaki mjane au mjane na watoto kubaki Yatima. Hakuna mwenza anayetaka mwenza wake aishiye Jela alafu familia ibaki na simanzi na mateso.

Kwa Watibeli, binti ,a Tibeli ni lazima vipato viwe bayana na kila pesa itolewe maelezo.
Na kama hilo haliwezekani ndoa hiyo au familia hiyo itavunjwa mapema sana.

Hivyo ndivyo Watibeli tunavyofanya mambo yetu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam to
 
Sikutaka kucoment ,kwanza nataka niwe mtu wa mwanzo kuichungilia mada ya mtibeli mtaalam wa fasikh,,
 
kitu ujui ni kwamba WOMEN ARE SELFISH.

lastly hizo ni description ni za women raised by SINGLE PARENTS.
 
Mkuu unawaza kumuweka huyu mwanamke kundi gani? Ipo hivi nina mwanamke nimepata nae mtoto mmoja, yule mwanamke wakati napata nae huyo mtoto alikua chini ya wazazi wake hata baada ya kujifungua aliendelea kuwa chini ya wazazi wake process za kujitamburisha zilifanyika ikatolewa posa, lakini siku zinakwenda ikabidi nimwambie kuwa tufanye utaratibu wa kuanza kuishi pamoja akakubali lakini akasema bila mahari ya 2.m hawezi kutoka kwao na katika kikao wakati wa kutoa posa familia yao ilitaja 5.m cash wala hawakuhitaji kitu kingine zaidi ya cash, na mpaka sasa binti anasema hawezi kwenda against na familia yake, kwa uelewa wako uyu mwanamke unamuweka kundi gani?
 
Mkuu unawaza kumuweka huyu mwanamke kundi gani? Ipo hivi nina mwanamke nimepata nae mtoto mmoja, yule mwanamke wakati napata nae huyo mtoto alikua chini ya wazazi wake hata baada ya kujifungua aliendelea kuwa chini ya wazazi wake process za kujitamburisha zilifanyika ikatolewa posa, lakini siku zinakwenda ikabidi nimwambie kuwa tufanye utaratibu wa kuanza kuishi pamoja akakubali lakini akasema bila mahari ya 2.m hawezi kutoka kwao na katika kikao wakati wa kutoa posa familia yao ilitaja 5.m cash wala hawakuhitaji kitu kingine zaidi ya cash, na mpaka sasa binti anasema hawezi kwenda against na familia yake, kwa uelewa wako uyu mwanamke unamuweka kundi gani?

Mwambie kwa Karne hii kutoa mahari ni kinyume na haki za binadamu.
Mwambie hutotoa na hutaenda kinyume na msimamo wako.

Sisi watibeli ni mwiko kutoa mahari wala Binti zetu kutolewa mahari

Hata ingekuwa elfu hamsini mwambie hutotoa
 
apa unazungumzia wanawake 7 tofauti. ni ngumu kupata mwanamke mmoja wa sifa zote izo na akawa mtu mwema kwako na bahati mbaya wenye hizi sifa nzurinzuri ulizotaja apo ni hawa much knows yy kila kitu anajua.

mtapata utajiri lakini mwisho wa siku anakugeuka akumalize ili abakie yy mwenyewe aitwe bosledi

wkt mwingine mm nazan mwanamke anayefaa ni hawa tunawaona wajingawajinga/ wasiojielewa la msingi we mpe muongozo mzuri tu. km ni msikivu mtafika kaanani vizuri tu mbona.
 
Mwambie kwa Karne hii kutoa mahari ni kinyume na haki za binadamu.
Mwambie hutotoa na hutaenda kinyume na msimamo wako.

Sisi watibeli ni mwiko kutoa mahari wala Binti zetu kutolewa mahari

Hata ingekuwa elfu hamsini mwambie hutotoa
Mkuu hivi ni haki kweli kununua matatizo kwa kulipa mahari aisee hata iweje siwezi kutoa mahari mi nimemuacha tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom