Nyambala badala ya wewe kupindishia pia ungeendelea kutujuza ni nani aliyesema kuwa kuna vitu wameficha? Ni nani ambaye aliomba mjadala wa Richmond urudi upya ili watoboe siri?
Mimi sijasema kwamba Mwakyembe ni mchafu, ninachoquestion ni hicho kitu wanachokisema ni ushujaa wa kusema. Kwanza hataki kutoka CCM, pili kuna vitu alivificha. Soma hii article kama nilivyoitoa kwenye mwananchi.
Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu Richmond/Dowans Send to a friend Tuesday, 25 January 2011 19:51 0diggsdigg
George Maziku
NAANDIKA makala haya kwa lengo la kusimamia ukweli na kuweka kumbukumbu sawa, nataka kurekebisha tabia tuliyojijengea Watanzania ya kuwalaumu na kuwashutumu watu kwa kutumia taarifa nusu-nusu, taarifa zisizo na ukweli kamili, taarifa za kuungaunga tu, na wakati mwingine tunawaacha wahusika halisi bila kuwabebesha msalaba wao.
Wakati wote wa sakata hili la Richmond na Dowans, Watanzania tumekuwa tukiwashambulia watu wawili tu, Lowassa na Rostam, tukiwatuhumu na kuwahukumu kuwa wao ndio vinara wa sakata hili, kwamba wao ndio wahusika wakuu wa kashfa hii ya kihistoria katika nchi yetu, kwamba wao ndio wamiliki wa makampuni haya ambayo sasa yanayoligharimu mabilioni taifa letu.
Waliosababisha tuamini hivyo ni wanasiasa na wanahabari ambao wakati wote wamekuwa wakitushawishi Watanzania tuamini kuwa Lowassa na Rostam ndio "wezi" wetu, kwamba hawa ndio waliosuka njama za kukwapua mabilioni yetu kupitia mradi wa dharura wa kufua umeme.
Kwa mfano, iliyokuwa Kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba kati ya serikali na Richmond iliyoongozwa na mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, maarufu kama kamati ya Mwakyembe, iliyotoa ripoti ikiwatuhumu wanasiasa hawa wawili kuwa nyuma ya kashifa hii.
Kwa upande wetu wanahabari kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika taarifa kwa kuzirudia rudia tukiwahukumu moja kwa moja Lowassa na Rostam kama wamiliki wa Richmond na Dowans, na kwa maana hiyo wamekula njama za kutuibia.
Binafsi msimamo wangu umekuwa wazi kabisa tangu mwanzo, kwamba Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu suala hili, tumefichwa habari muhimu na nzito kuliko hizi tunazozisikia, tumelishwa taarifa zitokanazo na chuki binafsi za kisiasa na pengine kibiashara.
Kwa mfano, Kamati ya Mwakyembe ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa mbunge huyo wa Kyela ambaye sasa ni Naibu waziri wa ujenzi, haikusema ukweli wote, ilituficha ukweli halisi wa sakata hilo, kwa ufupi kamati ile iliamua kwa makusudi kumlinda mtu aliyestahili kubeba lawama zote, mtu aliyestahili kusulubiwa.
Kamati ya Mwakyembe haikusema ukweli kuhusu nafasi ya rais Jakaya Kikwete katika mchakato mzima wa kuipatia mkataba wa kufua umeme wa dharura kampuni ya kitapeli ya Richmond, na hata katika uamuzi wa baadaye wa kuhamisha kinyemela mkataba huo kwenda kwa Dowans.
Yapo maelezo na nyaraka zinazothibitisha kuwa rais Kikwete alikuwa msimamizi mkuu wa mchakato ulioipatia Richmond zabuni ile, alikuwa akitoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa aliyekuwa waziri mkuu wake, Lowassa na alikuwa mwamuzi wa mwisho wa uamuzi wowote uliofikiwa wakati huo.
Kwa msingi huo, kuwatwisha zigo la lawama aliyekuwa waziri mkuu Lowassa, mawaziri wa zamani wa nishati na madini Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi bila maelezo ya kina na yenye mashiko na ushahidi madhubuti, ni uonevu na upotoshaji wa ukweli halisi wa sakata hilo.
Ni kweli Lowassa, Karamagi na Dk Msabaha walihusika kutokana na nyadhifa zao serikalini, lakini hawakuwa waamuzi wa mwisho wa suala hili, walikuwa wakitekeleza maagizo ya juu, kulikuwa na mtu mzito kuliko wao aliyekuwa na maamuzi ya mwisho, huyu ndiye anayestahili kulaumiwa na kuhukumiwa kwa yote yaliyotokea baadaye.
Lakini kwa sababu ambazo haziko wazi, Kamati ya Mwakyembe haikuhoji kabisa nafasi ya rais Kikwete katika sakata hili, waliamua kumlinda Rais, hata aliyekuwa Spika wa Bunge wakati ule, Samuel Sitta hakujihangaisha kuutafuta ukweli uliofichwa na Kamati ya Mwakyembe, hata kambi ya upinzani bungeni haikuhoji suala hilo, na hata wananchi hatujahoji hilo.
Kwa upande wa Rostam, yeye amekiri kuileta nchini kampuni ya Dowans iliyonunua mkataba wa Richmond, lakini yeye amesema alifanya hivyo baada ya kuombwa "kuwaokoa" wakubwa waliokuwa "wamebanwa mbavu" baada ya kubumbuluka kwa "dili" lao la Richmond.
Sasa kwa nini yeye abebeshwe lawama zote? Kwanini ahukumiwe kwa kosa lisilo lake? Rostam hakuiba, yeye kosa lake ni kuwasaidia wezi kuficha mali ya wizi, tumhukumu kwa hilo, lakini si kwa kosa la wizi, tuwatafute wezi wetu na tuwahukumu kwa madhambi yao. Source: Mwananchi
Kwa mantiki hii viongozi wote waliohusika na kuileta Richmonds na dada yake Dowans ni lazima wawajibike bila upendeleo.Haingii akilini tukawawajibisha wachache na kuwaacha wengine.Haki ni lazima itendwe kwa wote waliohusika na ufisadi huu.