Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,624
- 47,256
Mwaka unaelekea mwisho, ila kama ndugu/Jamii moja basi tunastahili kushauriana baadhi ya vitu, ili walau mwaka ujao tuuanze tukiwa na mentality mpya kwenye baadhi ya mambo.
Maisha ni magumu, na tunalalamika kuwa ni magumu, lakini approach zetu kwenye baadhi ya mambo ndio huwa zinaongeza ugumu. Tusipokubali kubadilika, basi tusitegemee mabadiliko yoyote, sana sana tutazidi kuwa depressed. Ujumbe wangu umewalenga sana wale job seekers, hustlers, fighters, educated and non educated. Ila yeyote atakayeona unamfaa,pia anaweza take note on anything.
Nitaongelea mambo kadhaa kwa kiasi fulani, mengine tutayajadili kupitia comment box.
1. Uaminifu ndio msingi wako
Wasomi wengi huwa mnadhani elimu ndio ngao yenu kubwa, yawezekana mkawa sahihi, lakini sio kitu pekee kinachoweza kukuweka mahali. Hakuna ubishi kuwa ukiwa na elimu, ni rahisi mtu kukubeba, lakini in some cases elimu pekee haitoshi, lazima uwe na vitu vya ziada, mfano uaminifu. Nitawapa mfano kutokea humu humu JF. Kuna member mmoja 2 or 3 years back alinifata pm kwamba life limempiga sana, kila siku ni afadhali ya jana. Akaomba nimsaidie kwa namna yoyote nitakayoweza. Kwanza nikajiuliza why kanifata Mimi na sio wengine? Ntawezaje kumsaidia mtu mwingine ilhali Mimi pia life langu gumu? Sikuijibu ile msg yake. One week later, kwenye ofisi inayonifanya nipate vihela vya kujistiri, nikasikia tetesi za kuwepo kwa nafasi ambazo zinahitaji kuwa covered, na uzuri ili hitaji mtu mwenye degree bila kujali ni kada gani. Nikarudi PM, nikamchek yule mdau na kumuuliza elimu yake. Nilivyoona anafit, kimoyo moyo nikajisemea labda Mimi ndio natakiwa kuwa daraja ili huyu mwamba aweze kuvuka.
Nikamuelekeza vitu vyote anavyotakiwa kuwa navyo. Alivyo vikamilisha, nikamuambia sehemu ya kwenda, na akifika amuulizie mtu fulani ( tumuite D), akimpata huyo D, then amwambie amekuwa recommended na R, from there kila kitu kitakuwa sawa. Jamaa alifanya kila nilichomwambia, tena siku hiyo alikuwa na full confidence (siunajua ukienda sehemu kwa recommendation sio randomly).
Alivyofika alipokelewa vizuri. Bahati mbaya/nzuri kwake siku hiyo palikuwa na ugeni wa ghafla, wenye ofisi yao wazungu walikuja tu for random visit ya hiyo branch yao maana ilikuwa mpya. Nadhan mnajua pakiwa na ugeni kama huo pilika pilika zake. Sasa jamaa baada ya documents zake kupokelewa, akaambiwa aungane na staffs wengine na wale wazungu kwenye orientation ya ile ofisi. Akaambiwa awe makini katika kunote down vitu, maana interview yake ndio inaanzia hapo. Jamaa hakuwa na pen, badala ya kuazima kwa staff yoyote, akaenda kuchukua ile pen ya reception ambayo kila anayeingia ofisini lazima aitumie kusaini.
Sasa kuna muda yule boss mzungu akataka kujua staffs waliokwisha fika ofisini, kwenye list ikaonesha watu 20, badala ya 25, wawili walikuwa na udhuru, watatu hawakusaini. Hao ambao hawakusaini, ikashindwa kuonesha muda walioingia kazini (maana lazima uandike reporting time). Hao ambao hawakusaini, walikuwa ni wageni, hawana hata week. Baada ya issue kuwa resolved, msala ukarudi kwa receptionist why anashindwa kulinda vitu alivyokabidhiwa (peni ya 200 😅😅😅). Baada ya hapo wakataka kujua pen imeenda wapi (wazungu walikuwa wanoko nao). Sasa sijui ni uoga au Nini, jamaa yetu akashindwa kujisema kuwa pen amechukua yeye, mpaka walipoangalia kwenye cctv camera. Wazungu wanamuliza MD, huyu nae ni staff wa hapa? Akasema hapana, ndio amefika leo for interview. Wazungu wanamuliza jamaa, why hukujitokeza tulipoulizia, mpaka tumeangalia camera? Jamaa kimya. Akaulizwa unadhan unastahili ajira hapa? Jamaa akasema sorry. Mzungu akamuuliza, are you ethical? Jamaa mdomo haufunguki kabisa. Yule MD akamwambia hii ndio interview yako sasa, kwa ulichokifanya, unadhani unastahili kufanya kazi hapa? Jamaa Kingereza chote kilipotea. Pen ya shilling 200 ikamkosesha kazi. Hakunichek tena pm, na tokea siku hiyo simuoni akichangia au kuanzisha threads humu, sasa sijui alibadili account au aliniweka kwenye ignored list.
2. Aibu ni adui yako mkubwa
Kinacho watofautisha wasomi na wasiosoma ni aibu. Wasomi wengi mnakuwaga na aibu ambazo hazina msingi. Wasiosoma au walioshia let say la saba, au waliosogea sekondari kidogo alaf wakashindwa kuendelea for any reason, hawa watu akili yao inakuwaga imeshakubaliana na mazingira, na huwa ni wepesi kujichanganya kwenye deals tofauti tofauti ambazo ni halali. Ndio maana ukijaribu kuangalia waliofeli primary, sasa hivi wamepiga hatua, au wako vizuri kiasi. Ukija kwa wasomi, pamoja elimu ambayo mtu anayo, ila fikira zake zinakuwa limited kwa kiasi fulani.
Wasomi wanabagua sana kazi. Mtu hana source yoyote ya kuingiza hela, ila Bado anakwambia kazi fulani siwezi fanya nitaonekaje. Sawa, u can be selective, lakini usiwe too selective wakati unajijua huna hela,huna connection na mahitaji yako ni makubwa. Weka elimu pembeni, jichanganye na wale unaowaona sio level zako, wale ndio wanaconnection za kutosha, wanajua vichochoro vingi na Wana uzoefu mwingi pia kwenye biashara maana ilo ndio tumaini lao. Kuna sehemu wao hawawezi kufika,sababu hawana elimu ya kutosha, ila asilimia kubwa sio wachoyo wa deals, na huwa ni wepesi kukuunganisha sehemu ambayo wanaona unaweza fit.
Watu wengi Wana kawaida ya kuwakimbia rafiki zao ambao wamefanikiwa. Unatembea zako kwa mguu ukimuona mshikaji wako yupo kwenye gari Kali , unajificha asikuone, eti kisa kipindi mnasoma wewe ndio ulikuwa unaongoza darasa, so unahisi atakucheka life limekupiga. Kuna tendency ya wale waliopigika kutafutana, ila wanajitenga na waliotusua.
Zamani wazee walikuwa wanasema damu nzito kuliko maji, au mchuma janga hula na wa kwao, ila kwa zama za sasa, mchuma janga hula peke yake, mara ngapi unaingia kwenye misala au msoto ila kila ndugu unayehisi atakusaidia ukimfata anakukataa? Damu sio nzito tena kama zamani, marafiki Wana mchango mkubwa pia. Ni heri ukachekwa, lakini komaa na unachohitaji. Maji huwa yanatoboa mwamba, sio kwavile yako strong, bali ni persistence.
3. Usipende kuomba hela, omba michongo
Ili la kuomba hela lipo sana tu. Sijajua kwa wengine, ila upande wangu huwa nakutana sana na pm za mtu anaomba umpush na 5k, 10k n.k. Sio mbaya sana, maana siku hazifanani. Wapo wanaojituma sana ila kuna siku mambo yanabuma. Hii JF kuna watu wako very connected, ila huwezi jua nani ni nani, maana hatufahamiani. Instead of kuingia inbox ya mtu kuomba hela, atleast omba connection, kama itakuwa ndani ya uwezo wa mtu atakusaidia. Kama ambavyo mtu anavyo andaa CV zake then anasambaza maofisini, just ingia pm ya mtu, jielezee. Japo humu wengine sound nyingi, ila maisha yao nao magumu tu, so kuwa makini. Cha msingi ni kwamba mwenye Nia ya kusaidia huwa hakuzungushi wala aanzi habari za kuomba hela, ukiona Kona Kona nyingi, achana nae. Ila hutakiwi kuacha kujaribu.
4. Ukiamua kuanzisha biashara, kuwa serious.
Kuna tofauti kati ya kuanzisha biashara au kujishikiza/kuzuga. Wasomi wengi huwa wanaanzisha biashara ili kubuy time, huku wakisubiria ajira. Na hii inasababisha wasiwe committed kwenye hizo biashara. Kila kitu inabidi kiwe na mipangilio, kama ushasema naanzisha biashara, basi komaa na hiyo biashara kwa nguvu zako zote mpaka walau isimame. Sio unaanzisha biashara leo, after 3 weeks hata wateja Bado hawajakuzoea, unachota hela, unaifanya nauli, huyo Dodoma kwenye usaili wa utumishi. Biashara yoyote mwanzoni inahitaji commitment ya muhusika. Kama unataka ku chase 2 birds at one time, basi tafuta mtu ambae mna interest sawa, share nae idea, akielewa, shirikianeni kwa kila kitu, ili hata ikitokea unahitajika sehemu nyingine, yeye anaweza kusimamia. Ila ukiwa peke yako, alaf ukapata dharura kama hiyo ya kwenda kwenye interview, ukisema umchukue tu mtu yeyote kwavile mna undugu, basi asimamie biashara yako wakati haupo, basi jiandae kula hasara.
Biashara hazihitaji kujaribu, maana setbacks ni nyingi mno. Ukiingia kwa kujaribu, alaf ukakutana na changamoto mbili tatu, niamini Mimi,utafunga hiyo biashara. Ila ukiwa serious,utavumilia. Kwenye biashara hasara na faida ni 50/50
Usifanye biashara kwa kujaribu au kujishikiza. Kuna msemo mmoja unasema "When you lose hope, you are dead", ila tunahitaji kujifunza kuwa flexible. Imagine tokea umemaliza chuo ni almost 5 years, umezungusha sana bahasha, umeapply sana kazi ila still upo high high.
5. Kuwa makini na unachopost humu JF, hiyo ndio CV yako kwa tusiokujua.
Kuna baadhi ya watu kwavile tunatumia ID fake, basi hawajali wanacho andika humu. Ikitokea umepatwa na shida au unahitaji msaada, post zako za nyuma ndio zitakuhukumu. Imagine mtu anaanzisha Uzi wa kuhitaji msaada let say anauhitaji wa kifedha, alaf unapitia posts zake za nyuma unakuta anaelezea namna ambavyo kuhonga kwake sio issue, cha msingi apate mbususu. Au anasema kuweka akiba hakuna tija, we only live once, ponda raha kifo ni anytime. So, sisi tuweke akiba ili tuje kukusaidia wewe unayeishi mara moja?
Tunatumia ID fake, ila tunavyopost somehow vinareflect maisha yetu. Sisi humu hatukujui, ila CV yako tuliyonayo, ni posts zako. Kuna ambao wakiwa na shida, wanaanza kufuta/kuedit posts zao za nyuma au wanafungua ID mpya. Uzuri huwezi futa vyote, na wale wanaokujaga na ID mpya kuomba misaada nadhani mnaonaga majibu ya members humu.
Binafsi nikionaga mtu ameanzisha thread ya kuomba msaada au amekuja PM lazima ni review posts zake za kitambo, na nadhani sipo peke yangu anayefanyaga hivi. Zamani ilikuwa mtu akiomba msaada namchukulia tapeli tu, nilijifunza kwa mdada mmoja hivi ambae aliombaga nimsaidie chochote aboost mtaji wake, ila sikumtilia uzito, japokuwa alifafanua vizuri sana wazo lake la biashara. Ila baada ya miezi mingi kupita, nilireview post zake ndio nikaona ni kweli alikuwa muhitaji, bahati mbaya account yake haipo tena active.
6. Acheni kuamini ushirikina.
Sio kila tunachofanya basi kitaenda kwa 100%, kuna muda mambo yanaweza kukuendea kombo mfululizo mpaka uhisi Dunia yote ipo against you. Unachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi katika upambanaji. Imekuwa kawaida, mambo yakienda vizuri tunajisifu kuwa tunabahati, ila yakienda kombo, either tunamlaumu Mungu kwa kututenga, au tunahisi kuna mkono wa mtu.
Kila mtu Yuko busy na maisha yake, nani akuroge wewe? Una nini cha tofauti? Jifunze kushukuru kwa kila jambo. Yakienda vizuri, mshukuru Mungu wako, yakienda ovyo, mshukuru pia. Unachotakiwa, jifunze kuwa msiri kwa baadhi ya mambo yako, ikitokea umekutana na mtu akakuunganisha sehemu, basi usimpe kero ya kumtaka amuunganishie kila rafiki yako. Jijenge wewe, ili uweze kuwabeba na wenzako.
7. Usianzishe mahusiano serious ikiwa bado unapambana.
Wanasema mapenzi yanarun Dunia, ila kiukweli mapenzi yana ruin Dunia. Mapenzi yanarudisha sana nyuma. Mapenzi na hustling haviendi pamoja hata ufosi vipi, lazima kimoja kipotee, na usipokuwa makini hata vyote vinaweza kupotea ubaki na kilio. Mkuu utastack sana. Utapata mchongo somewhere mbali na ulipo, ila badala ya kwenda, utaanza kujadiliana na mtu ambae hata hamjaoana. Utajikuta katika situation ya either ufate mchongo au upiganie penzi. Ukifata mchongo, huku nyuma huna chako, na ukisema umsikilize usiende, fast forward miezi kadhaa mbele, anakuacha, then utakuja humu kuomba ushauri.
Sisemi usiwe na mahusiano, ila kuwa na mtu kwa ajili ya kusogeza siku tu, but ukitaka kusettle, utasota. Love is a serious mental disease, ila ni vile huu ugonjwa upo underrated, ndoto na michongo mingi imekufa sababu ya mapenzi. Are you looking for love at the age of hustling?
8. Maboss wanaringa, ila jobless ni viburi.
Hii ipo wazi, wenye hela wengi wanaringa sana. Ila siwezi walaumu maana sijui walizipataje hela zao. Ila ukishajiona unashida, jifunze kujishusha, cha ajabu jobless wengi tunavimba. Hatukubali kuendeshwa. Broh, huna hela, huna connection, unapata wapi kiburi aisee? Nje ya topic, kuna lishangazi moja nilikuwaga nalo kipindi cha nyuma anaitwa Mwahija, kuna siku night kali nilishtuka usingizini kwenda msalani, nilivyorudi, jinsi alivyonona, ile shape na lile pozi alivyokuwa kalala, nikajikuta naomba shoo round ya pili, yule Maza alipatwa na mshangao, tena ule genuine sio wa kuigiza. Akaniuliza "Hivi we mtoto, unapata wapi nguvu za kuomba shoo usiku wote huu?" Umeshindwa hata kutoa mchango wa umeme leo (10k), hivi utaweza kumudu gharama za ghafla zikitokea?, huna hela, huna kazi ya maana mjini, hivi unawezaje hata kusimamisha?". Zile kauli zilinikwaza sana, kwa siku ile sikuweza kumuelewa, ila zilimake sense na zilisaidia kufungua akili yangu. So, back to the topic, kijana huna hela, huna kazi ya maana, huna connection, unatoa wapi kiburi??. Sehemu pekee ambayo kijana anaweza kujishusha to the maximum, ni pale anapotongoza demu mpya, ila sehemu zingine ni mwendo wa kuvimba. Tunasafari ndefu sana ya kutengeneza kesho yetu/ya watoto wetu, so tujifunze kujishusha.
Hii tabu na msoto tunaopitia leo, ni kwavile wazazi wetu hawakuwa na connection. Tunatakiwa kuikata hii chain ya msoto, tuifanye iishie kwetu. Tukishindwa kutoboa, basi atleast tuweke mazingira mazuri kwa kizazi chetu kijacho. Tukileta kiburi, msoto hautaishia kwetu. Elimu imekuwa rahisi sana now days, few years to come, majority watakuwa wamesoma, kutoboa maishani haitojalisha unajua nini, bali unamjua nani?
***** ****** ******* *******
Nina vingi sana ambavyo naona vinafaa kuviongea, ila naomba niishie hapa. Mengine kama nilivyosema tutaambiana kwenye comments box. Na Mwaka ujao, yafaa uwe ni mwaka mzuri kwa kila mmoja wetu
Wasalaam,