Huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu. Kwa sababu tumeshajifunza chaguzi tatu mfululizo yaani 2019, 2020 na 2024 hatuhitaji tena kubembelezana. Nadhani kama ni busara au hekima vimetumika na sasa iwe mwisho. Mimi nadhani harakati zianze sasa kabla kabisa ya mchakato wa uchaguzi haujaanza rasmi. Taasisi mbalimbali ziwajibike kuleta vuguvugu la kudai uchaguzi ulio huru na wa haki. Zaidi sana Taasisi za Dini ziwe kinara katika hili.
Nawashukuru sana viongozi wa Dini kwa jinsi walivyokuwa mstari wa mbele kupinga uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, 2024.Lakini kwa sasa nadhani viongozi wetu wa Dini wabadili style kidogo. Imefika muda wenye Mamlaka hawasikilizi hata kidogo kelele za watu wanaopinga udhalimu wao.
Yaani hata upige kelele namna gani wao kwa sababu tu ya Mamlaka yao wataendelea tu na lile jambo hata kama ni la ovyo kiasi gani. Niliwahi kusema na narudia tena. Naomba viongozi wetu wa Dini watuongoze kupiga kelele ambazo watawala wetu watazisikia. Niliwahi kusema na narudia tena.
1. Kila siku ya ibada angalau pale mwishoni kila anayeongoza ibada hiyo atumie angalau dakika 5 hivi kutoa Elimu ya Uraia na kukemea vikali Mambo ya ovyo wakati wa uchaguzi.
2. Angalau kila mwezi siku moja baada ya ibada itumike kufanya maandamano ya amani ya kudai uchaguzi ulio huru na wa haki. Maandamano yafanyike ndani ya viwanja vya nyumba za Ibada. Bila shaka hili tunaliweza tena sana. Hili lifanyike na Dini zote na madhehebu yake yote.
Ikumbukwe kuwa, uchaguzi huru na wa haki huleta viongozi waadilifu, wenye uwezo na wenye nia njema ya kuwatumikia Watanzania. Kwa hiyo, Dini haiwezi kujitenga na siasa wakati viongozi wetu wa Nchi ni wanasiasa. Lakini pia, viongozi wetu wa Dini hawawezi kuendelea kutuongoza kupambana na SHETANI tusiyemuona lakini wanaacha kutuongoza kupambana na watu waovu tunaowaona kwa macho yetu, tunaishi nao na tunasali hata kuswali nao.
Kwa wakristo itakumbukwa kuwa hata Yesu siku moja alichukua hatua ya kumwaga biashara za watu alipokuta wanafanya biashara hekaluni. Kwa hiyo, alipambana na waovu wazi wazi kwa sababu alikuwa anawaona. Kwa mfano, walioandaa na waliosimamia chaguzi hizo tatu mfululizo si hawa hawa tunaosali na kuswali nao? Tumewachulia hatua gani katika nyanja zetu za Dini?
Wanaodhulumiwa katika chaguzi zetu ni waumini wetu kwa hiyo ni lazima tuchukue hatua za pekee ili kukomesha dhuluma katika Nchi.
Nitoe ombi kwa viongozi wetu wa Dini kuepuka kupewa michango ya mamilioni ya kujengea nyumba za Ibada hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu.
Nawasilisha.