Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,674
- 23,536
View: https://www.youtube.com/watch?v=rm8wI2pHQ4s
Nimemsikiliza Boniphace Mwabukusi, nimegundua yafuatayo kutoka kwake na namna akivyo
1. Ni Clip ndefu kiasi.
2. Nimeisikiliza yote
3. Alianza kuongea vizuri sana
4. Alitulia na kutoa hoja zenye nguvu. Anaamini Muda unatosha kuwa na katiba mpya kabla ya Uchaguzi.
5. Baadae alibadilika kutoka alichokuwa anaongea.
6. Aliegemea mno CHADEMA na anaona kama ndio chama pekee cha Upinzani.
7. Akabadilika tena na kunanga CCM waliomtuma akawa anawasilisha anayoyataka yeye
9. Ana uwezo mkubwa wa kujenga Hoja, ila hajui kusimamia hoja.
10. Mwishoni hajatoa nafasi kabisa (room) kuwa kuna watu wanaweza kuwa na mtazamo tofauti.
11. Anaamini Katiba ya Warioba na ile pendekezwa ni njia pekee ya kutoka.
12. Nadhani ni vzr akajua NA SISI TUPO N.A TUNA MAWAZO TOFAUTI
13. Pia si vzr kutoa vitisho kuwa ataua mtu akiibiwa kura anaweza kufa yeye maana kifo ni haki ya Mungu pekee.
Mbinu mojawapo inayotumiwa na vyama vilivyo madarakani kushinda uchaguzi unaofuata ni kuandaa watu wao kwa kuwavisha joho la upinzani. Miaka kabla ya uchaguzi, watatiwa misukosuko mingi ili waonekane kweli ni wapinzani. Wataonekana kupingana na serikali na hata kushtakiwa. Wakishaingia kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi kupitia upinzani, basi lengo linakuwa limetimia.
Watavuruga mikutano na uchaguzi ndani kwa ndani . Hawa wapo kuanzia ngazi ya kata hadi ngazi za juu kabisa. Tumeyaona haya katika kila uchaguzi kuanzia kuhalalishwa sera ya vyama vingi.
Cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba upinzani haujataka kujifunza. Turejee tu historia ya vyama vyote vya upinzani, tutaona vurugu zinazotokana na wafuasi wa chama tawala kuingia upinzani na kurejea kwenye chama chao baada ya uchaguzi.
Jambo hili linajirudia rudia kama mzunguko wa dunia kwenye jua. Msaliti hapashwi kukubalika hata mara moja. Kwa bahati mbaya vyama vya upinzani vimejaza watu wanaobeba bendera zao lakini kimsingi wako upande mwingine. Wataingia wengi kwenye uchaguzi kuwakilisha upinzani, lakini lengo lao ni kuhakikisha chama tawala kinashinda. Kwa mwenendo huu, upinzani hautaweza kutoboa