Mvua na radi ya kutisha inanyesha sasa hivi!

Kwa karibu zaidi ya nusu saa sasa hivi, mvua kubwa sana inanyesha.
Radi na upepo unavuma hadi naogopa.
Umeme umekatika na sijui watu wa mabondeni itakuwaje?
Niko mitaa ya Kinondoni kaskazini, asubuhi itakuwa bonge ya foleni!
Huku Tukuyu ni mvua masaa 20 yote wiki ya 3 sasa
Kuna wale walijenga vibanda vya mabati pale Kinondoni mkwajuni usiku huu sijui inakuwaje.
Wanapigana nyama kama kawa tu.
 
Tuwaombee wa mabondeni wasifikwe na maafa. Hii mvua ni kubwa sana na itanyesha muda mrefu ujao leo.
 
Du kweli TANESCO wameionja Hapa Kazi Tu, umeme umerudi saa hizi.
Zamani ndo ingekuwa hadi mtondogoo!
Mvua inanyesha kistaarabu, lakini hii ndo inaelekea mpaka mchana au vipi!
Haahaaa we jamaa una vituko.hiyo imejiunga na kifuruushi cha masaa 24 hivyo itanyesha mchana kutwa mpk usiku muda ilipoanza kunyesha ndio itaisha
 
Watu walidhani mamlaka ya hali ya hewa inatania au inahujumu wakazi wa mabondeni kuhusu mvua za El-nino...Sasa hii mvua ndio inathibitisha kuwa mamlaka ya hali ya hewa haikuwa inafanya mzaha.

Na pia serikali ilivyokuwa ikiondoa wakazi wa mabondeni kwa haraka vile ilikuwa inajua what's best for them...Lakini ujuaji mwingi umefanya hadi leo hii wakazi wa mabondeni waendelee kubaki huko.

Yule mbunge wa CUF wa hapo Kinondoni ataweka wapi uso wake!?
Huyo mbunge , The Boss na Salary Slip, hope watakuwa tayari kupiga mbizi kwenda kuokoa wakazi wa mabondeni.
 
Kwa karibu zaidi ya nusu saa sasa hivi, mvua kubwa sana inanyesha.
Radi na upepo unavuma hadi naogopa.
Umeme umekatika na sijui watu wa mabondeni itakuwaje?
Niko mitaa ya Kinondoni kaskazini, asubuhi itakuwa bonge ya foleni!
Poleni ndio mambo ya mungu.
 
serekali yetu inawapenda sana sana watu WA mabondeni na chamno zaidi ni Juu ya uzima wao! au uhai wao!/uhai haununuliwi Bali chochote kile kinajengeka / taratibu.
THANKS TO NEMC.
 
hali ya hewa ni nzuri leo, haka kamvua kaendelee siku 5 hivi mfululizo....
 
Back
Top Bottom