MUWASA Yaendelea Kusambaza Maji ya Bomba Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189

MUWASA YAENDELEA KUSAMBAZA MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI

Mitambo iliyofungwa Bukanga, Musoma Mjini, kwa ajili ya kuzalisha maji kutoka Ziwa Victoria ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 36 za maji kwa siku - haya ni maji mengi mno ukilinganisha na mahitaji ya maji ya kila siku ya Mji wa Musoma!

Tenki kubwa lenye ujazo wa lita milioni tatu (lita 3m) za maji limejengwa Mlimani Bharima (angalia picha iliyoambatanishwa hapa) kwa ajili ya usambazaji wa maji ya bomba ndani na nje ya Mji wa Musoma.

Serikali imeipa MUWASA jukumu la kusambaza maji ya bomba kutoka Tenki la Bharima kwenda vijiji jirani na Mji wa Musoma, vikiwemo vijiji vya Musoma Vijijini na Butiama.

Maji ya MUWASA kusambazwa Musoma Vijijini:

Kata ambazo zimepangwa kusambaziwa maji ya MUWASA ni nne, ambazo ni Kata ya Etaro (vijiji 3), Nyegina (vijiji 3), Nyakatende (vijiji 4) na Ifulifu (vijiji 3).

MUWASA wameishafanikiwa kusambaza maji ya bomba kwenye baadhi ya vijiji vya Kata ya Etaro (vijiji vya Busamba, Etaro na Mmahare) na Nyegina (kijiji cha Mkirira). Usambazaji unaendelea.

Bomba kuu la Nyegina linatandazwa:

Kazi ya kutandaza bomba kuu la maji kuelekea Nyegina Senta inafanyika wakati huu - angali picha zilizoambatanishwa hapa

Vilevile, tukumbuke kwamba baadhi ya vijiji vya Kata nne zilizotajwa hapo juu, vimeanza kutumia maji ya bomba kutoka vyanzo vilivyojengwa na RUWASA, na BADEA (maji kutoka Mugango).

Miradi ya maji ya bomba Jimboni mwetu:

Vijiji vyetu vyote 68 vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Vijiji 53 kati ya 68 vimeanza kutumia maji ya bomba (77.94% ya vijiji vyote), na vingine miradi yao iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Vilevile, kuna vijiji vinachimbiwa visima virefu vya maji, na kazi hiyo inaendelea vizuri ndani ya Kata ya Bugwema.

Kazi nzuri na kubwa ya usambazaji wa maji ya bomba vijijini mwetu inafanywa na RUWASA, MUWASA, na BADEA (bomba la maji la Mugango-Kiabakari-Butiama).

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
(i) Tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni tatu (lita 3m). Limejengwa Mlimani Bharima

(ii) Utandazaji ya bomba kuu la maji kuelekea Nyegina Senta, Kata ya Nyegina, Musoma Vijijini.

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wote tunaendelea kuishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo vijijini mwetu, ikiwemo miradi ya maji safi na salama ya bomba - Ahsante sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumanne, 24.9.2024
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.30.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.30.jpeg
    51.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.30(1).jpeg
    58.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.31.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.31.jpeg
    137.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.32.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-24 at 11.09.32.jpeg
    139 KB · Views: 2
Back
Top Bottom