Muungano na mazonge yake: Sukari ya Zanzibar hairuhusiwi kuuzwa Tanzania Bara

Lakini kuna mtu anaweza kuniambia wapi Zanzibar wanalima miwa? Hii sukari sio ya kutoka Pakistani au China?
Zanzibar tunalima sana Miwa.
Ukiachilia Karafuu, Mwani na Nazi, kilimo kingine kikubwa cha biashara kwa Zanzibar ni Miwa.

Njoo Zanzibar ujionee mwenyewe.
Zanzibar ni level nyingine, huu muungano wa kihuni na Tanganyika ndio unaoturudisha sana nyuma sisi wazanzibar.
 
Ni upuuzi kuamini kile unachokisema wewe tu ndio sahihi maana unang'ang'ania kwamba hiyo sukari wanayotaka kuja kuuza bara inaagizwa kutoka nje wakati imeelezwa hapo kwamba kiwanda kipo na hata kuna viongozi wa serikali ya muungano wamewahi kukitembelea hicho kiwanda na kama unafikiria hivyo ndio unataka tuamini hizo bidhaa zinazopelekwa kuuzwa Znz zikitokea huku bara nazo zote zinaagizwa kutoka nje huku wakidai zinatengenezwa hapa sio!
Kama kinazalisha lakini Zenji tu haitoshi sasa unaanzaje kuwalisha majirani wakati watoto ndani bado wananjaa na mkome kufunga wazee na kushangalia ni utovu wa nidhamu
 
Sukari yenyewe tank 8000, matumizi yao tani 17000, sasa wanataka Ku export kwa nini. Biashara ni ushindani, hao wahindi wajitahidi kuzalisha kwa bei nafuu ili waweza kuliahikilia soko la Zanzibar, NA serekali ipige marufuku uingizaji wa sukari.
Uwe unasoma mada na kuelewa vyema badala ya kurukia hoja.

Zanzibar ni nchi ya kibiashara, walioanzisha Kiwanda cha Sukari huko Zanzibar walilenga kufanya biashara kwa kuuza popote duniani na target yao ilikuwa ni kuuza Tanzania bara, Comoro, Ngazija na kwenye meli zinazotia nanga hapa Zanzibar kuelekea ulaya, Asia na Marekani.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haikuwapangia wapi pa kuuza, SMZ ilikuwa inataka Kupata Kodi, Pesa za kigeni na Ajira ya kudumu kwa wazanzibar kupitia uwepo wa hicho kiwanda na mashamba ya miwa.

Kwanini pia hujiulizi hivi ni kwanini Viwanda vya Tanzania bara vinavyozalisha sukari havitoleshelezi mahitaji ya Tanzania bara lakini hapo hapo vinauza sukari nje ya nchi ikiwemo Zanzibar?
 
Meneja mwenyewe wa kiwanda anaitwa Rajesh Kumar unategemea nini Mkuu? Hiyo ya Lahore tu hapo wanapack kwa mifuko!!
Kwani unamjua meneja wa kiwanda cha Mtibwa Sugar, Kilombero au Mtibws Sugar anaitwa nani?
Ni vizuri ukauliza ili uambiwe

Wamiliki wa karibu viwanda vyote vya sukari hapa Tanzania ni raia wa kigeni (wana Asili ya kiasia) na hiyo ni asili yao katika hiyo biashara. Na hicho kitu ni karibu Afrika Nzima. Huwezi ukakiepuka.

Biashara ya Sukari ina mila, desturi na utamaduni wake, na duniani kuna koo fulani fulani tu za kiasia ndio zinaweza kuisimamia. Ni kitu cha ajabu sana.
 
Huyo waziri mbona anachanganya lugha wakati anaongea?
Amekaa zaidi Marekani na Ulaya.
Uzungu unamsumbua kidogo kiasi cha kuchanganya Lugha. Otherwise ni mbwembwe tu katika kumzingua mwandishi aliyekuwa anamuhoji.
 
Nimekuelewa Isaa. Lakini ninyi wa Wazenj mlipata fursa nzuri sana ya kuukataa huu Muungano feki ktk Rasimu ya Katiba. Pale Bungeni kura zenu za kuukataa Muungano huenda mngepata Uhuru wenu. Sasa ninyi mnaumia na sisi tunaumia. Poleni sana
Wabunge wa ccm kutoka zrnji ni vibuyu kabisa, wana maneno ya shombo sana wakati wanajua fika wanawakandamiza wazenji wenzao.
 
Hata hivyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo alisema hana taarifa hadi awaulize wasaidizi wake.

Mimi ni waziri wa Viwanda na Biashara, nina manaibu waziri wawili, makatibu wakuu, manaibu katibu na nina wakurugenzi na mashirika 19 chini yangu. Ninasikia mambo mengi, nikikwambia nina majibu vidoleni nitakudanganya, hadi niwasikilize wasaidizi wangu,” alisema Mwijage kwa njia ya simu.

Huwezi kunijibu hivyo mimi!!!!!!
 
Wabunge wa ccm kutoka zrnji ni vibuyu kabisa, wana maneno ya shombo sana wakati wanajua fika wanawakandamiza wazenji wenzao.


Huu si muungano ni uvamizi. Tanganyika chini ya Nyerere' iliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte pamoja na mawaziri wake na kuwafunga katika magereza ya Tanganyika bila kuwafikisha mahakamani kabla hata huo uitwao Muungano haujafikiriwa
 
Watanzania mtakua mmerogwa mnaruhusu kaburu aje awekeze hapo kwenye sukari huku mlieungana nae mnampa vikwazo sio bure...
 
Miwa inalimwa Sana Zanzibar na kiwanda kiko mahonda lakini serikali ya bara ni kawaida yao kutuwekea vikwazo bara hawanahaja na cc wao wanaangalia maslahi yao tu si jengine lakini cc wazenj hasa viongozi wetu ndio wasiojitambu au llabda ni kulinda maslahi yao tu.
Si mnawatukana ati wa bara machogo
 
Kwa hiyo mnataka sukari inayozalishwa Zanzibar tuuziwe Bara kwa bei kubwa halafu nyie muwe mnatumia ya nje kwa bei ndogo.

Huu ni ufisadi wa waziwazi kwa kuwabeba wafanyabishara wa Zanzibar na mzigo kuwatwisha Wabara...
Kwani Tanganyika wamezuiwa na nani kuagiza kutoka nje na kuuza bei rahisi kama si roho mbaya zenu tu!
 
Sukari haiwatoshi lakini wanalazimisha wauze Bara ili faida itumike kuagiza sukari nyingine nje ya nchi. Wazanzibar wana akili sana.
Zanzibar Mfuko wa 50 Kg ni 60,000. Bara ni 90,000 Elfu 30,000 waitumie kuagiza ya ziada kwa kuwa Bara ni mazoba?
Hata ardhi Zanzibar haiwatoshi lakini munalazimisha kupeleka wapiga kura hewa!
 
Naomba kueleweshwa Kuna haja gani ya kuweka sheria au taratibu za sukari? Kwani ina tofauti gani na chumvi after all watumiaji was chumvi ni wengi zaidi kuliko was sukari
Hii sheria ya kipuuzi ya sukari ndio inasababisha tunanunua sukari kwa bei ya juu,, mbona hawatungi sheria ya chumvi na Sembe,,
 
Si mnawatukana ati wa bara machogo
masihara nayo wamekuwa siasa,wabara si wanawaita wazanzibari wanywa urojo wameregea??sasa hii imehusiana na nini katika kuendeleza biashara katika nchi mbili zilizoungana
 
Nimekuelewa Isaa. Lakini ninyi wa Wazenj mlipata fursa nzuri sana ya kuukataa huu Muungano feki ktk Rasimu ya Katiba. Pale Bungeni kura zenu za kuukataa Muungano huenda mngepata Uhuru wenu. Sasa ninyi mnaumia na sisi tunaumia. Poleni sana
Sasa wakiukataa hio sukar watauza wapi?
 
Back
Top Bottom