Lookmalasin
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,457
- 1,829
Wahuni hawajui nguvu kubwa iliyotumika kumdhibiti Nyerere. Nyerere aliondoa ukabila, udini, ukanda, matabaka.Hii habari yaweza kuwa ya kutunga au laah, ila ukweli mchungu ni kwamba, rasilimali isipolindwa itaporwa na wenye nguvu. Rasilimali kama ardhi, madini, maji, mafuta, gas misitu na sasa carbon, vyote wenye nguvu wanavitaka. Na wajinga na wanyenyekevu wakiwa na rasilimali hizi hawastahili hata kuishi. Wataondoshwa ama wanataka au hawataki ili wenye nguvu wabebe. America kwa red Indies, wazungu kwa Muamar Gaddafi, wazungu kwa DRC Kongo kupitia Rwanda na Uganda. West Africa na Msumbiji kwenye gas kote wenye nguvu wanapora kibabe. Tanganyika hajui kulinda chochote mbali na Mwl Nyerere aliyejenga kambi za jeshi juu ya ardhi za madini kututunzia sisi mazuzu tunaoachia kila kitu bila hata kuhoji. Shame on us.
Aliunganisha Taifa. Mtu amekaa kama Rais zaidi ya miaka 25 hajaiba hata senti tano. Leo analinganishwa na Samia.