Muungano: Dkt. Mpango na Waziri wa Afya, hili si la Muungano. Msiliingize kinyemela!

WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA TANZANIA BARA KWENDA ZANZIBAR (II)
KATIBU MKUU ABEIDA ''ATHIBITISHA'' KAULI ZA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MASOUD OTHMAN


Hapo juu tumeeleza kisa cha Watoto 66 '' Wahamiaji haramu'' kutoka Bara kwenda Zanzibar
Ni habari liyozizima mitandaoni kwa mshtuko kwamba tuna tofauti za mipaka na Uhamiaji.

Uhamiaji ni idara katika Wizara ya mambo ya ndani. Mwaka 2024 Uhamiaji ilikamilisha ujenzi wa jengo Zanzibar.
Watumishi wa Uhamiaji wanafunzwa katika Chuo cha Uhamiaji Tanga na Moshi kwa gharama za JMT

Rais SSH aliagiza Watumishi wa Zanzibar wabadilishane na wa Bara kuimarisha utendaji

Gazeti la Mwananchi ( Rejea bandiko#38) lilimkariri makamu wa Rais Mh Othman Masoud Othman akisema Uhamiaj imeondolewa katika Muungano bila kueleza lini na kwa utaratibu gani, ilikuwa ni SIRI

Gharama za uendeshaji ni jukumu la JMT ambaybajeti ni kutoka Tanganyika.
Kilichoondolewa Uhamiaji ni uwezo wa kukusanya mapato kama JMT na sasa SMZ inakusanya .

Gharama za uendeshaji wa idara ya Uhamiaji zikiwemo mishahara, majengo n.k. zinalipwa kutoka bajeti ya JMT ambayo ni ya Tanganyika. Bajeti ya SMZ 2024/2025 haina kipengele cha Uhamiaji.

Kauli ya Katibu mkuu Bi Abeida Rashid kuhusu 'Watoto wahamiaji haramu' inashabihiana na ile ya makamu wa wa Rais Mh OMO kwamba Uhamiaji imeondolewa kinyemela kama ilivyo ondolewa gesi/mafuta . Bandari n.k. ingawa gharama za uendeshaji idara ya Uhamiaji Zanzibar ni za JMT au Tanganyika.

Haiwezekani kukawa na watoto wahamiaji haramu kama sisi ni Nchi moja.
Mtoto akitoka Mbeya kwenda Tanga hawezi kuwa mhamiaji haramu, iweje wa Tanganyika kwenda Zanzibar awe hivyo? Je watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika nao ni 'Wahamiaji haramu'' ?

Hoja inayojengwa ni kwamba Watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika ni ''Watanzania'' kwasababu kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar.

Ni kwa mintaarafu hiyo Watoto wa Wazanzibar wanaoishi Tanganyika wanahaki na kila fursa kama Watanzania, lakini Watoto wa Tanzania Bara wanaokwenda Zanzibar wanapoteza Utanzania na kuwa Watanganyika na hapo hupachikwa jina la Wahamiaji haramu. Mbunge aliyetaka Watanganyika waende Zanzibar kwa passport alikuwa na hoja kama ya Bi Rashid na Makamu wa Rais OMO. Mbunge aliyeukana Utanzania alikuwa na hoja kama ya Bi Rashid.

Kauli ya Bi Abeida Rashid inapaswa kukemewa. Ni kauli inayoleta hisia na chuki

Bi Abeida Rashid amewadhalilisha Watanganyika!

Ikiwa Uhamiaji si jambo la Muungano kama wanavyodai Wazanzibar, mipaka iwekwe na hoja ya passport irudi mezani ili Watanganyika waende kwa passport na Wazanzibar nao waishi Tanganyika kama Wageni!
 
ZANZIBAR INAONEWA, IPEWE NAFASI YA KUKOPA
OMO ATAKA ''FULL AUTONOMY''
MANSOUR ATAKA ' FULL AUTHORITY'

Taarifa ni kwa hisani na shukrani kwa gazeti la The Citizen

Ziara ya viongozi wa ACT Kkisiwani Pemba inatuelezamengi. Ukifuatilia kauli za kiongozi Othman Masoud Othman (OMO) katika mikutano utabaini jipya kuhusu muungano.

OMO amemsifia Rais mstaafu Karume kwa kuongoza mageuzi ya katiba tunayojua yalikiuka taratibu na katiba ya JMT. Ni mageuzi yaliyoondoa Zanzibar katika Muungano kiaina ingawa katika ''mafao'' bado ipo.

Kwa wanaosema ACT wanataka Muungano uvunjike wanawaonea! CCM ni washirika pia

Tofauti ya ACT na CCM ni kutoaminiana kutokana na tofauti za kihistoria na kinasaba. Kwamba nje ya Muungano nini kitafuata!!!. CCM wana hofu ya historia wakiwa na mtazamo mmoja wa kutotaka Muungano.

Katika mkutano OMO anasema Wazanzibar wanataka '' Full autonomy''. Kwa tafsiri isiyo rasmi '' huru na inayojitegemea'' , Zanzibar isiyofungamana na Tanganyika Kiulinzi na Usalama, Uchumi, kijaamii na Utamaduni. OMO anachosema ni Zanzibar nje ya Muungano

Kiongozi, Mansour Himid aliyekuwa CCM anasema '' Zanzibar inataka Full authority'' akimaanisha Zanzibar yenye mamlaka kamili yaliyo na mipaka! kwamba kuna mambo itahitaji kushirikiana au kuhusisha Tanganyika.

Mansour Himid anaamini katika 'mapinduzi daima' na full authority. OMO haamini 'mapinduzi' anataka 'full autonomy'. Hizi ndizo tofauti tulizoleza mwanzoni za ACT na CCM zikijengwa katika kutoaminiana

Suala lingine aliloongea ni Mikopo. OMO anasema Zanzibar haiendelei kiuchumi kwasababu haina uwezo wa kukopa ikifungwa mikono na JMT au Tanganyika.

Kwa utaratibu, SMZ inakopa kwa kudhaminiwa na JMT na kuna mikopo ya Zanzibar inayolipwa na JMT

Hoja ya OMO ina mantiki. Hakuna sababu za kuzuia Zanzibar isikope.
Ikiwa watakopa na kulipa deni ni 'KERO' kuwaweka katika udhamini wa Tanganyika.

Kuna kila sababu za kuiacha Zanzibar au kuisaidia bila udhamini ikope matrilioni ya fedha kokote duniani ili mradi tu ukopaji huo hautamhusisha Mtanganyika.

OMO anapaswa kulieleza hilo wazi na pia atamke kwamba Zanzibar haihitaji udhamini wa Tanganyika na katika hili Tanganyika imuunge mkono OMO na ACT
 
KITUKO KINGINE CHA MUUNGANO WA ''TANZANIA NA ZANZIBAR''
MAKUBALIANO (MoU) KATI YA NCHI YA ''TANZANIA NA NCHI YA ZANZIBAR'' KUHUSU USAFIRI MAJINI


Mabandiko yaiyopita tulieza tukio la makubaliano '' memorandum of understanding' au 'MoU' kati ya Nchi ya ''Tanzania na Nchi ya Zanzibar'' katika Nishati. Makubaliano hayo yalisainiwa

Hakuna kumbumbu za kuonyesha liliwahi kufanyika huko na hata kama lilifanyika ilikuwa ni makubaliano tu ya uendeshaji. Tofauti na sasa , MoU ni tukio kubwa kama yale yanayohusisha mataifa.

Kwa hisaini ya Gazeti la Mwananchi

kuna maafikiano ya Wakala wa meli wa JMT (TASAC) na Mamlaka ya usafiri ya nchi ya Zanzibar (ZMA)
Maafikiano yataleta Makubaliano (MoU) katika wiki zijazo kati ya '' Nchi ya Tanzania na Nchi ya Zanzibar'' .

TASAC ni wakala wa usimamizi wa usalama, biashara, na usafirishaji wa majini ''Nchini Tanzania''.
TASAC ilianzishwa 2018 kwa sheria ya Bunge ya Wakala wa meli no. 415 na ilianza majukumu Feb 23 2018

Uanzishwaji TASAC ulijadiliwa Bungeni wakiwemo Wabunge kutoka Zanzibar. Sheria iliridhiwa na Rais wa JMT kama chombo cha JMT chenye mamlaka ya usalama, biashara, usafirishaji na uwakala wa Meli

Katika mazingira ya utata wa Muungano zama hizi, Zanzibar wameanzisha chombo chao ZMA.

kwa mantiki kwamba kuna mipaka ya bahari kati ya 'Tanzania na Zanzibar''.
Si tatizo Zanzibar kuwa na taasisi,si mara ya kwanza, na hakuna! mamlaka/taasisi isiyo na mbadala Zanzibar.

Ni haki kusema TASAC si chombo cha Muungano, ni cha Tanganyika lakini kwa jina la Tanzania.
Sheria zinazotekelezwa na TASAC zimetaja ''Tanzania Bara'', nchi isiyokuwepo na wala haijawahi kuwepo

Jina Tanzania linawanyima Watanganyika fursa ya chombo chao kama ilivyo kwa Wazanzibar.

TASAC ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi isiyo ya Muungano. Na hapa ndipo tatizo linapoanza.

1. Kwa muundo wa TASAC , Rais wa JMT anaweza kumteua yoyote midhali ni Mtanzania kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Hili linawahusu Wazanzibar kwasababu '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania, lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''
2. Mkurugenzi wa TASAC anaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Mtanzania.
3. Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC anaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Mtanzania
4. Wajumbe wote wa Bodi wanaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile, ni Watanzania.
5. Watumishi wote wanaweza kutoka Zanzibar kwasababu zile zile ni Watanzania

Mantiki ni kwamba, TASAC ni ya Tanganyika kisheria,, lakini, inaweza kumilikiwa na kuendeshwa na Wazanzibar kwa 100%, kwasababu nao ni Watanzania. Hakuna Mtanganyika anayeweza kutumikia ZMA kwa nafasi yoyote! kwasababu si Mzanzibar!

Kwa namba 1-5 hapo juu hakuna sheria itakayovunjwa. Wazanzibar ni Watanzania, ingawa TASAC ni chombo cha Tanzania japo hakifanyika kazi Zanzibar.

Hapa ndipo hoja ya Tanganyika kukasimu madaraka yake katika muungano inapojitokeza'.

Wazanzibar wana haki katika TASAC walishiriki sheria ya kuanzishwa kwake Bungeni
Maswali ya kujiuliza, kwanini chombo cha Tanganyika kitungiwe sheria, Wazanzibar wakishiriki?

Kwanini chombo kilichotungiwa sheria na Wazanzibar hakitambuliwi Zanzibar lakini kinaitwa cha Muungano?

Na kwanini chombo kinachofanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya Tanzania kina mipaka ndani ya Tanzania?
Ikiwa Zanzibar si Tanzania, Tanzania inayotajwa na sheria iliyoanzisha TASAC ipo wapi?

Kwanini tunaita vyombo au taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania ikiwa hazitambuliwi na Wazanzibar?

Yote haya yanatokea kwasababu vyombo na taasisi za Tanganyika hazina usimamizi na mwenyewe.
Je, kuna sababu ya kujiuliza tena iwapo Tanganyika inahitajika?

Kuwa na taasisi Tanganyika tukizificha kwa jina la Tanzania hakusaidii.
Turejee katika Rasimu ya Warioba, mambo 7 tu! na kama haiwezekani tusijidanganye tuna muungano!
 
Back
Top Bottom