Murtaza Mangungu nakushauri mtafute Wakili Msomi Llyod Nchunga akueleze aliondokaje Yanga ili na wewe uondoke kwa amani

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
576
2,400
Njia wanazotumia wanasimba kukutaka ujiuzulu ni kelele za chura tu, pressure imekuwa kubwa kukufosi uachie uenyekiti kwa sababu umeshindwa kuleta furaha kwa wanasimba.

Halafu umewaongezea machungu sana pale ulipokuwa ukihojiwa na waandishi wachovu wa Mawingu kwani ulikuwa ukiongea na jeuri, ubishi, kujiamini kulikopitiliza.

Sikikiza Mangungu, wanasimba ndio walikuchagua uwaongoze, ulianza kushindana na Juma Nkamia na baadae Wakili Msomi Mosses Kaluwa ukamshinda kwa kile wanachokidai ni hila.

Sasa hao waliokuchagua wanakuona wewe hufai kwanini unang'ang'ania Bw.Mangungu.

We unapata nini hapo unapopang'ang'ania wakati unaowaongoza hawakutaki?

Utafanya kazi na nani sasa wakati wanachama wote hawakutaki, hawakutaki.

Mtafute Lloyd Nchunga Wakili Msomi ambaye alikuwa na michongo kama yako, akajifanya mjuaji siku tulipokutana na Yanga mzee Akilimali akatangaza kabisa kuwa simba hafungwi hiyo mechi na kweli tukaibamiza yanga mabao 5 kwa nunge.

Nchunga aliondoka kwa aibu Yanga, mambo aliyotendewa hadi akadiriki kujiuzulu hayakuwa mazuri.

Nchunga hana hamu hadi leo.Wewe unaposema huwezi kujiuzulu unawakosea heshima wanachama.Hao hao ndio walikuona wewe unafaa na ss hv wameona hapana, wajibika tu ili kuiokoa Simba.

Nikikumbuka ya Nchunga naona yale yale yanajirudia tena kwetu.Wape wengine waendeleze kijiti baba.
 
Aondoke kwa kosa gani?

Hebu eleza majukumu yake kikatiba kisha yachambuliwe ili tujuwe makosa yake na tuungane tupaaze makelele kwa pamoja ya yeye kujiuzulu!
 
Hana mda ataondoka,ameifelisha Sana team yet,mfano Jana nimemsikia akisema par omary jobe hawawezi kuvunja mkataba wake eti kwasababu Ni mrefu,hivi inaingia akilini unamsainisha mkataba mrefu mchezaji ambae hakuwa na timu kwa mda mrefu,inaumiza sana,jobe tutaendelea kuwa nae msimu ujao,tujiandae kwa maumivu msimu ujao
 
Kwa akiri za kawaida mangungu na uzeen wake atoke Simba wewe uta muajiri? Kuweni na huruma na wazee wenu mlimchagua wenyewe Kwa mbwembwe zote halafu mmeanza majungu.

Jambo la msingi kasema atasajiri Kwa Hela zake shida Iko wapi?
 
Mangungu usiachie timu kaka, mbona Chadema wanamponda Samia kuwa hafai kuwa Rais na still anaendelea na urais? Ushauri wangu kwako usisikilize wajinga wanaotaka ujiuzulu, hao ni wabaya wako uliowashinda kwenye uchaguzi na wasiokutakia mema, hakuna timu isiyofanya vibaya, Kaizer Chiefs wameshika nafasi ya 7 kule PSL mbona hawafukuzani iweje kwako una makombe mawili msimu huu ngao na muungano na bado timu imeshika nafasi ya 3 tena kwa kulingana points na aliyeshika nafasi ya pili.
Kaza kaka sisi tupo nyuma yako.
 
Hana mda ataondoka,ameifelisha Sana team yet,mfano Jana nimemsikia akisema par omary jobe hawawezi kuvunja mkataba wake eti kwasababu Ni mrefu,hivi inaingia akilini unamsainisha mkataba mrefu mchezaji ambae hakuwa na timu kwa mda mrefu,inaumiza sana,jobe tutaendelea kuwa nae msimu ujao,tujiandae kwa maumivu msimu ujao
Yaan mpaka sasa hamumujui aliyewafelisha .

Kweli Maskin hana kiapo
 
Mangungu hamjaanza kumsema leo kabla ya uchaguzi mlimsema sana lkn mlipoingia kwenye box mangungu kaibuka kidedea usiwaaminishe wengine kuwa hawamtaki sema kwa nafsi yako
 
Back
Top Bottom